Baadhi ya ndugu wakichukua mwili wa ndugu yao baada ya kuutambua |
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Bi Mboni Mhita (kushoto)
akimfariji mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya basi la Another G na
lori iliyoua 23 na kujeruhi 34 jana ,wengine pichani ni wajumbe wa
kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Mufindi
Habari na picha na
MatukiodaimaBlog
MIILI yote 23 ya ajali ya basi aina Coster mali
ya kampuni ya Another G lenye namba
za usajili T 927 CEF aina ya mitsubishi fuso iliyokuw3a ikifanya safari
zake kati ya Iringa – Njombe ambalo liligoganga na uso kwa
uso na lori lenye namba za
usajili T 916AQM likiwa na Tela lenye namba za usajili T 965 BEH
Scania imetambuliwa na ndugu zao.
Kwa
mujibu wa mkuu wa wilaya ya Mufindi ambae ni mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama ya wilaya Bi Mboni Mhita kuwa ndugu wa
marehemu hao waliokufa katika ajali waliweza kutambua miili ya
ndugu zao jana na leo na kuwa hadi sasa hakuna mwili ambao bado
kutambulia na hivyo kuvishukuru vyombo vya habari kwa kushiriki
kuhabarisha juu ya ajali hiyo na wananchi ambao waliitikia na
kufika kutambua miili hiyo .
Akizungumza
na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz leo mkuu huyo wa wilaya Bi Mboni
alisema kuwa jitihada kubwa zimeonyeshwa na vyombo vya habari vya
ndani ya mkoa wa Iringa na nje ya mkoa ikiwemo mitandao ya kijamii
katika kuhabarisha umma na ndio sababu ya utambuzi wa miili hiyo
kufanikiwa mapema baada ya habari kuenezwa vilivyo.
Pia
mkuu huyo wa wilaya alipongeza uongozi wa JKT Mafinga na
uongozi wa kitaifa wa jeshi hilo kwa kujitolea kusaidia mazishi
ya vijana wake ambao walikuwa wakielekea JKT Mafinga kwa ajili ya
kuripoti kwa kuanza mafunzo ya jeshi na baadhi yao kufa katika ajali
hiyo huku baadhi wakijeruhiwa kwani alisema ni vigumu kwa taasisi
kujitolea kusaidia mtu ambae hana mkataba nae.
Aidha
mkuu huyo wa wilaya aliwaomba wananchi wote nchini ambao ndugu
zao walipoteza maisha katika ajali ya basi la Majinja lililoua watu
zaidi ya 50 katika eneo la Changalawe mjini Mafinga kufika kituo
cha polisi Mafinga kwa ajili ya kutambua na kuchukua mizigo ya ndugu
zao waliopoteza maisha katika ajali hiyo na kuwa mali zote za
marehemu hao zimehifadhiwa salama.
Hata
hivyo mkuu huyo wa wilaya ya Mufindi Bi Mboni alivitaka vyombo
vya usalama barabarani katika wilaya ya Mufindi kuendelea na
mkakati wake wa kuwabana madereva wanaovunja sheria za barabarani
na kuwachukulia hatu kali kama njia ya kupunguza ajali hiyo.
Alisema
askari hao pia wanapaswa kukagua ubora wa vyombo vya usafiri
vyote na vile ambavyo havina ubora ni heri kuvifungia hadi
vitakapoboreshwa kuliko kuruhusu vyombo vya usafiri chakavu
kufanya kazi ya usafirishaji wa abiria .
Kuhusiana
na wajibu wa shirika la viwango Tanzania (TBS) mkuu huyo wa wilaya
alishauri kuwepo na mkakati makini wa TBS kukagua ubora wa vyombo
vya usafiri vinavyoingizwa nchini kwani mabasi mengi ya abiria siti
zake zimeshikiliwa na ngundi ya mbao na baada ya kutokea ajali siti
hizo hung'oka na kama abiria amefunga mkanda hulazimika kuchomoka na
siti yake .
Alisema
katika ripoti ya ajali ya kwanza ya basi la Majinja iliyotokea Machi
mwaka huu na kuua watu zaidi ya 50 kamati ya uchunguzi ilibaini hilo
na kuwa mwenye uwezo wa kukagua viwango vya vyombo hivyo vya
usafiri ni TBS kwa kushirikiana na wadau wengine kama Sumatra na jeshi
la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani.
Wakati
serikali ya wilaya ya Mufindi kupitia mkuu huyo wa wilaya ikishauri
TBS na washirika wake kuweka mkakati wa kukagua viwango vya
vyombo hivyo vya usafiri baadhi ya wananchi wilaya ya Mufindi na
mkoa wa Iringa wamekuwa na maoni tofauti kwa kulitaka jeshi la polisi
kitendo cha askari wa usalama barabarani kuanza kusindikiza mabasi hayo
yanayotoka usiku mkoani Njombe na Iringa ili kuhakikisha abiria
hawazidi katika mabasi hayo ya usiku.
Zacharia
Sanga mkazi wa Mafinga wilaya ya Mufindi na John Lumwesa mkazi wa
Iringa mjini walisema kuwa kimsingi mabasi hayo yanajaza abiria
kupita kiasi na kutembea kwa mwendo mkali zaidi kutokana na nyakati za
usiku askari wa usalama barabara kutokuwepo.
Hivyo
walitaka askari wa usalama barabarani kuendelea kuwepo na tochi hadi
usiku ili kuthibiti ajali mbaya kama hiyo ambayo mbali ya kuwa ni
uzembe wa dereva wa basi ila kukosekana kwa askari wa usalama
barabarani usiku ni moja ya sababu.
Mganga mkuu wa
Hospitali ya wilaya ya
Mufindi Dr Godluck Mlimbila alisema
kuwa hali za majeruhi 34 waliokuwa wamelazwa katika Hospitali hiyo
zinaendelea vizuri na kuwa mbali ya wale wanne ambao hali zao
zilikuwa mbaya zaidi na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa
wa Iringa
katika Hospitali hiyo hadi jana majira ya saa 8 mchana ni majeruhi
kati ya 8 na 10 pekee ndio ambao walikuwa wakiendelea na matibabu
huku wengi wao wakiwa wameruhusiwa baada ya hali zao kuendelea
vema .
No comments:
Post a Comment