Wednesday, June 10, 2015

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA) WALIVYOADHIMISHA WIKI YA MAZINGIRA

Baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)wakipanda mti ofsini kwao Banana Ukonga jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira iliyofanyika hivi karibuni kitaifa mkoani Tanga.
Makamu wa rais Mohammed Ghalib Bilal akikaribishwa na Katibu Mkuu wa wizara ya uchukuzi Dk. Shaban Mwinjaka wakati alipotembelea banda TCAA wakati wa maadhimisho ya wiki ya mazingira yaliyofanyika hivi karibuni mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk. Shaban Mwinjaka akiwa kwenye picha ya pamojana wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) wakati alipotembelea banda la hilo wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Mazingira yaliyofanyika hivi karibuni Mkoani Tanga.
Wanafunizi wa shule za msingi mbalimbali mkoani Tanga waliotembelea kwenye banda la Mamlka ya Usafiri wa Anga Tanzania ,(TCAA) wakigawiwa vipeperushi vyenye ujumbe mbalimbali na Mkurugenzi mazingira wizara ya Uchukuzi Tumpe Mwaijunde wakati maadhimisho ya wiki ya Mazingira mkoani Tanga.
Wanafunzi wa shule za msingi mkoani Tanga wakiwa kwenye banda la TCAA wakijionea mambo mbalimbali yaliyokuwa yakionyweshwa hapo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira yaliyofanyika mkoani hapo.

No comments: