Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Dkt. Seif Rashid, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Bw. Keneth Kaseke, Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti
wa Dawa za Kulevya, kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na wakuu wa Wilaya za mkoa wa Pwani , kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete salimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa TAYOA Bw. Peter Msika, kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiakisalimiana na afisa wa Benki ya NMB kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugwnai wa Mashitaka nchini Bw. Biswalo Mganga kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Afisa wa habari wa UNDP Bi, Usia Nkhoma ndiye aliyekuwa mshereheshaji mkuu wa maadhimisho hayo
Maandamano kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani

Rais Kikwete akipokea Maandamano kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Maandamano kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Maandamano kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Meza kuu na wote waliohudhuria wanasimama kuimba wimbo wa Taifa
Wadau wakiimba wimbo wa Taifa
Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani

Wataalamu wa kurusha matangazo wa TBC wakirusha maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Kikundi cha muziki na utamaduni cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) kikitumbuiza Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Eng. Everist Ndikilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, akitoa muhtasari wa shughuli
Mary Kibwana na Christa Komba Walimu wakongwe na magwiji wa sanaa za maonesho wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakiongoza kikundi cha maigizo tumbuiza Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Hassan Salum, Msanii mahiri ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) akiigiza kama 'Teja' mbele ya Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Wanafunzi wa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakiigiza kama 'Mateja' mbele ya Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Wanafunzi wa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakiigiza mbele ya Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Meza kuu wakiangalia mchezo wa kuigiza unaohusu athari za dawa za kulevya
Hassan Salum, Msanii mahiri ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) akiigiza kama 'Teja'
Hassan Salum, Msanii mahiri ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) akiigiza kama 'Teja'
Wanafunzi wa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakiigiza mbele ya Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Wanafunzi wa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakicheza ngoma za utamaduni mbele ya Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Wanafunzi wa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakiigiza mbele ya Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) akiigiza mbele ya Wananchi
Bw. Keneth Kaseke, Kamishna wa Tume ya Kuratibu
Udhibiti wa Dawa za Kulevya, akisoma risala kwa mgeni rasmi
Rais Kikwete akimpongeza Bw. Keneth Kaseke, Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, akosma risala kwa mgeni rasmi
Salum Maziabi na Dotto Mohamed wakitoa ushuhuda wao wa njinsi walivyofanikiwa kupambana na dawa za kulevya na kufanikiwa kuacha nazo kwa kutumia Methadone na kuzingatia ushauri wa wataalamu
Rais Kikwete akiwapongeza Salum Maziabi na Dotto Mohamed baada ya kutoa ushuhuda wao wa njinsi walivyofanikiwa kupambana na dawa za kulevya na kufanikiwa kuacha nazo kwa kutumia Methanol na kuzingatia ushauri wa wataalamu
Rais Kikwete akicheza na mtoto wa Dotto Mohamed ambaye alitoa ushuhuda wa njinsi walivyofanikiwa kupambana na dawa za kulevya na kufanikiwa kuacha nazo kwa kutumia Methanol na kuzingatia ushauri wa wataalamu
Wataalamu wa afya ya akili waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Wataalamu wa afya ya akili waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Dkt. Bwijo Bwijo, kutoka UNDP, akitoa salamu za taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa
Rais Kikwete na meza kuu wakisalimiana na baadhi ya wanamichezo wa timu michezo mbalimbali zilizoshindana katika kuadhimisha siku hiyo

Rais Kikwete akimkabidhi zawadi kwa ajili ya wachezaji wa timu zilizoshinda daktari mtaalamu wa afya ya akili kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Rais Kikwete akipokea zawadi maalumu ya saa kutoka kwa Bw. Keneth Kaseke, Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya.
Rais Kikwete akipokea zawadi maalumu ya saa kutoka kwa Bw. Keneth Kaseke, Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya
Dkt. Seif Rashid, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, akimkaribisha Rais Kikwete kuhutubia wananchi kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani
Rais Kikwete akizindua mpango wa kupasha habari kwa njia ya mtandao na simu ya mkononi akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TAYOA Bw. Peter Msika
Rais Kikwete akihutubia wananchi kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE,
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENYE MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU
YA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA DUNIANI - BAGAMOYO, MKOANI PWANI,TAREHE 26 JUNI
2015
Mheshimiwa Dkt. Seif Rashid, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii;
Mheshimiwa Eng. Everist Ndikilo, Mkuu wa Mkoa wa
Pwani,
Ndugu Keneth Kaseke, Kamishna wa Tume ya Kuratibu
Udhibiti wa Dawa za Kulevya;
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;
Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali;
Viongozi wa Vyama vya Siasa wakiongozwa na Chama
Tawala;
Dkt. Bwijo Bwijo, kutoka UNDP na Wawakilishi wa
Jumuiya na Taasisi za Kimataifa;
Viongozi wa Dini na Asasi za Kiraia;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Ndugu
wananchi;
Salamu na Shukrani
Nakushukuru sana Mheshimiwa Dkt. Seif Rashid,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na waandazi wa shughuli hii kwa kunialika na
kunishirikisha katika Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani. Natoa
pongezi nyingi kwa wananchi na viongozi wa Mkoa wa Pwani wakiongozwa na Mkuu wa
Mkoa Mhe. Eng. Evarist Ndikilo kwa kukubali kuwa wenyeji wa sherehe hizi. Baada ya kuona mabango na kusikia kauli
kadhaa kutoka wasanii mmejidhihirishia ni jinsi gani mlivyojitayarisha kufanikisha
hafla ya leo. Nawapongeza kwa
kushirikiana vyema na Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya na
kufanikisha maadhimisho haya. Mwisho nitoe pongezi zangu kwa TAYOA kutokana na
ubunifu wao mzuri wa mawasiliano miongoni mwa vijana. Hongereni sana! Hakika
mambo yamefana sana.
Aidha, nawashukuru kwa zawadi nzuri ya saa ambayo
itakuwa inanikumbusha wakati wa kulala na kuamka.
Kuadhimisha kupiga Vita Matumizi na Biashara
Haramu ya Dawa za Kulevya
Ndugu wananchi;
Kama alivyoeleza Mwakilishi kutoka UNDP, Dkt.
Bwijo Bwijo tarehe 26 Juni ya kila mwaka ni siku maalum ya kuadhimisha kupiga
vita matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya duniani. Maadhimisho haya
hutupa fursa ya kutafakari hatua tunazopiga katika jitihada zetu za kudhibiti
biashara na matumizi ya dawa za kulevya katika jamii zetu na nchi yetu kwa
jumla. Katika siku hii pia, pamoja na kufanya tathmini ya mafanikio na
changamoto za mapambano hayo tunapanga
mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizopo kwa ufanisi zaidi.
Tujenge Jamii, Maisha na Utu wetu bila Dawa za
Kulevya.
Ndugu wananchi;
Kila mwaka maadhimisho haya yanapofanyika huwepo kauli mbiu ambayo
hutoa ujumbe unaosisitiza jambo lililokusudiwa wakati huo. Kauli mbiu ya mwaka
huu ya, “Tujenge jamii, maisha na utu wetu bila dawa za kulevya” inatukumbusha
sote kukaa mbali na matumizi na biashara ya dawa za kulevya. Dawa za kulevya ni
hatari kwa maisha ya mwanadamu, utu wake
na ustawi wa jamii yake. Kauli mbiu hii
inatutaka tujenge jamii, maisha na utu wetu bila kujihusisha kwa namna yoyote
ile na dawa za kulevya. Dawa za kulevya hazina manufaa yo yote bali hasara
tele. Mapambano haya dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya yanamhusu
kila mmoja wetu wadogo kwa wakubwa, viongozi na wananchi wa kawaida, matajiri
na maskini, Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kwani athari zake humgusa kila
mmoja wetu.
Madhara ya dawa za Kulevya
Ndugu Wananchi;
Ni jambo lililo dhahiri kuwa dawa za kulevya zina
madhara makubwa sana. Matumizi na biashara ya dawa za kulevya inaathiri ustawi
wa binadamu. Hudhoofisha afya za watumiaji, na huchochea kuenea kwa maambukizi
ya virusi vya UKIMWI, homa ya ini na mara nyingi husababisha vifo. Hali
kadhalika, huchochea rushwa miongoni mwa watumishi wa umma hasa wale
wanaotegemewa kuongoza mapambano dhidi yake. Kwa mujibu wa tamko la Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Uhalifu na Dawa za Kulevya
alilolitoa tarehe 5 Juni, 2013 kwenye Mkutano wa mwaka wa Vyombo vya Udhibiti
wa Dawa za Kulevya uliofanyika Moscow, watu wapatao 200,000 hupoteza maisha kila mwaka duniani kutokana na matumizi ya
dawa za kulevya. Biashara ya dawa za kulevya imeleta changamoto kubwa kwa
jumuiya ya kimataifa. Kwa baadhi ya nchi, biashara hii imekuwa ni janga kubwa
ambalo limesababisha kuharibika kwa mifumo ya kiutawala na kisheria, uvunjifu
wa amani na usalama, kudorora kwa maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi. Biashara
hii huchochea kuwepo kwa magenge ya kihalifu yanayojihusisha na mauaji, wizi na
ujambazi. Hali kadhalika, mapato yake
yanafahamika kugharamia shughuli za ugaidi, usafirishaji haramu wa binadamu,
biashara ya fedha haramu, biashara haramu ya silaha na uporaji wa nyara za
taifa - vitendo ambavyo ni tishio kwa usalama wa dunia.
Hivi basi kupiga vita biashara na matumizi ya dawa za kulevya ni vita vya haki
na ni wajibu kwa kila mtu kushiriki.
Lazima tushinde vita hii.
Juhudi za Mapambano
Kimataifa
Ndugu wananchi;
Mataifa mengi duniani yametambua madhara ya
matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya. Pia watu wengi wanauona umuhimu
wa kufanya juhudi za pamoja ndani ya nchi, kikanda na kimataifa kukabiliana na uhalifu huu. Matokeo
yake ni kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Uhalifu na Dawa
za Kulevya. Pia, ni kufanyika kwa operesheni za pamoja za kupambana na biashara
ya dawa za kulevya zinazofanywa na mataifa mbalimbali kikanda na kimataifa.
Jambo lingine ni pamoja na kuwepo kwa mikutano ya pamoja kimataifa na kikanda
kwa ajili kupanga mikakati ya pamoja.
Naungana na viongozi wenzangu wa nchi mbalimbali
duniani na mashirika wa kimataifa katika mapambano haya. Nakemea vikali
matumizi na biashara ya dawa za kulevya na kuwaonya wananchi wajiepushe kabisa
kujihusisha nazo. Ni imani yangu kuwa, Watanzania wenzangu mtafanya kila
liwezekanalo kujiepusha na kuwaepusha watu wengine hasa vijana na watoto
kujihusisha na balaa hili. Watanzania wenzangu tuongozwe
na kauli mbiu ya TANU wakati wa kudai uhuru na kujenga nchi inasema, “Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu”. Na
kwa sasa kauli ya CCM isemayo, ”Umoja ni
Ushindi”. Hakika umoja wetu ndio utakaotuhakikishia ushindi katika
mapambano haya.
Vyombo vyetu Viko Macho
Ndugu wananchi;
Naomba niwahakikishie kuwa Serikali
itaendelea kutimiza wajibu wake katika mapambano dhidi ya biashara na matumizi
ya dawa ya kulevya bila kuchoka na bila kigugumizi au ajizi yoyote. Lengo letu ni kudhibiti hali ili kuzuia
isizidi kuwa mbaya zaidi ya ilivyo sasa na kubadili mwelekeo ili hatimaye
tulikomeshe kabisa tatizo hili hapa nchini.
Kwa ajili hiyo, tumekuwa tunafanya mambo makuu matatu.
Kwanza, kuimarisha vyombo vya
dola vinavyoongoza mapambano dhidi ya uhalifu huo. Tunayo Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya ambayo imefanya kazi kubwa ya kuelimisha
jamii kujiepusha na matumizi na biashara ya dawa za kulevya. Tumeendelea kuijengea uwezo Tume hiyo pamoja
na Jeshi la Polisi ambalo ndilo linalokamata wafanya biashara na watumiaji na
kuwafikisha katika vyombo vya Sheria. Pamoja
na hayo nikaamua kuunda Kikosi Kazi kilichojumuisha Polisi, Idara ya Usalama wa
Taifa na Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya. Kikosi Kazi hicho kimefanya kazi
kubwa na nzuri. Kimeongeza nguvu na
uwezo wa kupambana na uhalifu huu na wahalifu wanaojihusisha na biashara hii
haramu na wanaotumia dawa za kulevya.
Wafanya biashara wengi wadogo, wa kati na wakubwa wamekamtwa na
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Ukamataji wa Dawa za Kulevya nao
umeongezeka sana na hivyo kunusuru taifa na hata dunia na madhara ambayo dawa
hizo zingefanya. Tumezisikia takwimu zilizotolewa na Ndugu Keneth Kaseke,
Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa
Dawa za Kulevya.
Hiki ni kiwango kikubwa cha
mafanikio hivyo vyombo vinastahili pongezi nyingi kutoka kwetu sote. Takwimu hizi zinatuonesha kuwa tatizo ni
kubwa hivyo lazima tuwe katika hali ya
tahadhari wakati wote (saa 24 kwa siku zote saba za wiki).
Pili, ili kuongeza nguvu,
mbinu na maarifa ya kupambana na uhalifu huu wa hatari na kutisha, tumetunga
Sheria (mpya) ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Mwaka 2015.
Sheria hii imejengeka juu ya hali ilivyo sasa katika mapambano haya. Mafanikio na changamoto zilizopo imezingatiwa
hivyo ni Sheria inayoimarisha mafanikio tuliyoyapata na kuyapatia ufumbuzi
matatizo yaliyopo. Sheria inaunda chombo
maalum cha kupambana na Dawa za Kulevya.
Chombo hiki kitakuwa na nguvu kubwa zaidi ya kuratibu udhibiti wa dawa
za kulevya nchini. Kimepewa mamlaka ya
kupeleleza, kupekua na kukamata wafanya biashara na watumiaji wa dawa za
kulevya. Nina imani kubwa kwamba chombo
hiki kitasaidia sana kupunguza tatizo hili nchini. Natanguliza kuwaomba wananchi na vyombo
vingine vyote vya Serikali kutoa ushirikiano wa kutosha kwa chombo hiki mara kitakapoanza kazi ili tuweze kulinusuru
taifa letu na tatizo hili.
Huduma za Matibabu
Ndugu wananchi;
Kwa kuzingatia hekima na
busara za usemi wa Wahenga, ”Kinga ni bora kuliko tiba”, mkakati
wa kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya unasisitiza sana kuelimisha jamii
kuhusu kuepukana na kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya. Kwa
wale waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya, mkakati ni wa Serikali
kuendeleza jitihada za kuwapatia ushauri nasaha na matibabu. Hilo ndilo jambo
letu la tatu. Kwa sasa huduma hizi
zinapatikana katika vitengo vya magonjwa ya akili katika hospitali za baadhi
ya mikoa na wilaya hata nchini. Hata hivyo, idadi ya watumiaji wanaopata nafasi
ya kupata huduma za tiba bado ni ndogo sana. Takwimu zinaonesha kuwa kuna
watumiaji wa heroin wanaokadiriwa kuwa
kati ya 200,000 na 425,000 nchini. Idadi ya watumiaji wa heroin
wanaopata matibabu kwa kutumia tiba ya methadone mpaka kufikia Mei, 2015 ni
2,300 tu. Watu hawajitokezi kwa
wingi. Tafadhalini ndugu zangu jitokezeni mpate uponyaji.
Ninaiagiza mikoa yote hasa
ile yenye matatizo makubwa ya matumizi ya dawa za kulevya hususani Dar es Salaam, Tanga, Arusha,
Mwanza, Mbeya, Pwani na Shinyanga kuchukua hatua thabiti za kuanzisha na
kuendeleza huduma hizi. Lazima tutambue pia, kwamba hakuna Mkoa ambao uko
salama, tofauti ni kiwango cha athari. Hivyo basi kila Mkoa ujiandae ipasavyo.
Tahadhari kabla ya hatari. Nawataka
Viongozi wa Mikoa na Wilaya kote nchini wafuatilie utekelezaji wa jambo hili.
Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya ziliweke suala la dawa za kuleya
kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyao.
Napenda kutumia nafasi hii
kuwashukuru wale wote waliosaidia katika kuanzisha na kuendeleza huduma ya methadone
na huduma nyingine za matibabu nchini. Niruhusuni nitoe shukrani maalum kwa
Rais Barack Obama na Serikali ya Watu wa
Marekani kwa msaada mkubwa wnaotupatia kwa upande wa matibabu.
Tusiharibu Taswira ya Nchi yetu
Ndugu wananchi;
Narudia kuelezea masikitiko
kuhusu baadhi ya Watanzania wenzetu wanaojihusisha na biashara ya dawa za
kulevya nje ya nchi. Hawa ni chachu ya kuendelea kwa tatizo hapa nchini. Pia, wanaharibu
taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa na kuhatarisha maisha yao. Zipo taarifa kuwa kati ya Januari 2012 na
Desemba 2014, kwa mfano, jumla ya Watanzania 111 walikamatwa kwa kujihusisha biashara hiyo katika nchi za Brazil na China. Hii ni
fedheha kubwa. Pia, naomba niwakumbushe na kuwatahadharisha kuwa baadhi ya nchi
hutoa adhabu kali ikiwemo ya kifo kwa watu
watakaokamatwa na kutiwa hatiani. Mfano mmoja wapo ni wa yale
yaliyotokea Indonesia kati ya Januari na
Aprili 2015 ilipowanyonga wasafirishaji wa dawa za kulevya 12 kutoka nchi mbalimbali zikiwemo za Afrika. Nchi hiyo ilikataa
maombi ya nchi zao kutaka adhabu hiyo
isitekelezwe dhidi ya raia wao.
Akitetea uamuzi wa nchi yake
Mwanasheria Mkuu wa Indonesia Muhammad Prasetyo baada ya hukumu kutekelezwa
alisema;
‘Tunapigana vita dhidi ya uhalifu wa kutisha wa
dawa za kulevya ambao unatishia mustakabali wa taifa letu. Napenda kusema kwamba kuua si jambo jema, si jambo
la kufurahisha. Lakini lazima tufanye hivyo kwa ajili ya kuliokoa taifa na
hatari ya dawa za kulevya. Hatufanyi uadui na nchi ambazo raia wake
walihukumiwa kifo.’
Nawaasa Watanzania wenzangu
watambue ukweli huu na kuachana na
biashara ya dawa za kulevya ndani
na nje ya nchi yetu. Ni hatari kwao na taifa pia. Ingawa hapa nchini adhabu ya
kifo haitolewi kwa kosa la kujihusisha na dawa za kulevya, Sheria
ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya 2015 ambayo itaanza
kutumika hivi karibuni inatoa adhabu kali hadi kifungo cha maisha.
Tahadhari Dhidi ya Matumizi ya Shisha
Ndugu wananchi;
Kwa masikitiko makubwa, Serikali imepokea
malalamiko mengi kuhusu matumizi ya shisha nchini. Matumizi haya yameenea kwa
haraka katika maeneo mengi ya starehe na huwavutia vijana wengi wa kiume na wa
kike. Watumiaji wa kilevi hiki huonyesha dalili zinazofanana na za utumiaji wa
dawa za kulevya. Hivyo, kuna hofu kuwa kilevi hiki kinachanganywa na dawa za
kulevya. Kama hiyo ni kweli ni jambo
hili ni la kusikitisha sana, halikubaliki na kwamba hatuna budi kuhakikisha
kuwa haliachwi kuendelea. Nichukue
nafasi hii kuziagiza mamlaka husika kufanya uchunguzi haraka iwezekanavyo ili
kupata majibu yatakayosaidia kutatua tatizo hili na hatimaye kuinusuru jamii yetu.
Tusiruhusu Rushwa Ijipenyeze
Ndugu wananchi;
Mapambano dhidi ya biashara
na matumizi ya dawa za kulevya si lelemama. Kuna changamoto kadhaa ikiwa ni
pamoja na vishawishi vya rushwa. Vitendo
vya rushwa kwa baadhi ya watendaji wasiokuwa waaminifu vinachangia sana katika
kurudisha nyuma mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya. Natoa agizo
kwa mamlaka husika kuhakikisha kuwa
suala la rushwa linadhibitiwa kikamilifu katika mapambano haya kwa kuwachukulia hatua stahiki wote
watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.
Mjitokeze kwa Wingi Kujiandikisha
Ndugu wananchi;
Wote mnatambua vema kuwa
mwaka huu tutakuwa na uchaguzi wa
viongozi katika ngazi mbalimbali katika Taifa letu. Nawaasa wananchi wenzangu
muendelee kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha
katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. Wakati wa kupiga kura utakapofika,
mtumie haki yenu ya kikatiba kuchagua viongozi waadilifu ambao kwa namna yoyote
ile hawajihusishi na biashara au matumizi ya dawa za kulevya. Aidha, nawaasa
wazazi na walezi, viongozi wa dini, viongozi wa asasi za kijamii, watambue kuwa
hivi ni vita vyetu sote. Tatizo la dawa za kulevya likiachiwa bila kudhibitiwa
kwa dhati litaleta maafa makubwa kwa kizazi cha sasa na kijacho. Kwa sababu
hiyo, tunao wajibu wa kupambana kila mtu kwa nafasi yake. Tuwalee watoto wetu
kwa misingi ya maadili mema ili kujenga Taifa lisilokuwa na matumizi wala biashara ya dawa za kulevya. Inawezekana Timiza Wajibu wako.
Tujenge jamii, maisha na utu
wetu bila dawa za kulevya
Asanteni kwa kunisikiliza.
No comments:
Post a Comment