Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (akiwakilisha Tanzania) katika picha ya pamoja
na washiriki wa kikosi kazi cha “African Ministerial
Conference on Meteorology (AMCOMET) Technical Task Force on African Regional
Space Programme on Meteorology” Geneva, Uswisi tarehe 10 juni 2015.
Tanzania ambayo ni
mwenyekiti wa kikosi kazi cha “African Ministerial Conference on Meteorology
(AMCOMET) Technical Task Force on African Regional Space Programme on
Meteorology” iliongoza kikao cha kikosi kazi hicho kilichofanyika tarehe 10
Juni 2015 sambamba na Mkutano Mkuu wa 17 wa Shrikika la Hali Duniani (WMO-CONGRESS-17)
huko Geneva nchini Uswisi. Kikao
kiliendeshwa chini ya Dkt. Agnes Kijazi kwa mafanikio makubwa.
Mkutano huo wa kikosi
kazi ulifanyika kwa kutumia fursa ya kuwepo washiriki katika Mkutano Mkuu wa 17
wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO Congress-17). Lengo la mkutano lilikuwa kubadilishana
uzoefu na nchi ambazo zimepiga hatua katika masuala ya hali ya hewa katika anga
za juu (Space Meteorology). Aidha kikao pia kilijadili upatikanaji wa vyanzo
vya mapato ambavyo vitasaidia kufanikisha programu hii na miradi itakayofanyika
wakati wa utekelezaji wa program hii.
Dkt.
Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ambaye pia ni
mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)
na mwenyekiti wa mkutano huo akiendesha Mkutano wa Kamati ya Kikosi Kazi cha
Programu ya anga za juu ya AMCOMET, Geneva, Uswisi. Kulia kwake ni Dkt. Joseph
Kanyanga kutoka Zambia akiwakilisha AMCOMET Bureau na Dkt. Amosi Makarau, Rais
wa RA1; Kushoto kwake ni wawakilishi wawili wa Sekretarieti ya Shirika la Hali
ya Hewa Duniani (WMO Secretariat).
Katika ufunguzi wa
mkutano huo, Dkt. Agnes Kijazi alirejea kwa kifupi makubaliano yaliyofanyika katika
mkutano wa tatu wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya hali ya hewa Afrika (AMCOMET)
uliofanyika huko Praia, Cabo Verde, ambapo kikosi kazi kiliongezewa jukumu la
kuendelea na upembuzi yakinifu wa mpango mkakati wa utekelezaji wa programu ya hali
ya hewa ya anga za juu barani Afrika. Dkt. Kijazi aliongezea kusema kuwa kikosi
kazi kupitia mwenyekiti Tanzania kilishiriki kikamilifu katika kuandaa rasimu
za sera na mpango mkakati wa anga za juu wa Umoja wa Afrika (Space Policy and
Implementation Plan). Ushiriki huu ulihakikisha kuwa masuala ya hali ya hewa
yanaingizwa katika rasimu hizi. Pia alifahamisha kikao kuwa mkutano wa tatu (3)
wa Mawaziri uliofanyika Cabo Verde ulipitisha rasimu hizo.
Aidha Dkt. Kijazi aliwashukuru
wajumbe wa kikosi kazi hiki kwa kuiamini Tanzania kuwa Mwenyekiti wake. Kwa upande wake Dr. Joseph Kanyanga (Zambia)
kama mwakilishi wa ‘AMCOMET Bureau’ alisema makubaliano ya kikao hicho
yatajadiliwa katika kikao kijacho cha Bureau. Dr. Amosi Makarau (Zimbabwe) ambaye
ni Rais wa Africa katika masuala ya hali ya hewa alikishukuru kikosi kazi kwa
hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa majukumu yake.
Katika kikao
hicho baadhi ya mashirika na nchi zilizopiga hatua katika eneo la teknonojia ya
anga za juu ziliwasilisha mada zenye lengo la kubadilishana uzoefu. Nchi hizo
ni China, Nigeria, Afika ya Kusini pamoja na Taasisi ya Umoja wa Ulaya ya “European
Meteorological Satellite Agency (EUMETSAT)” na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).
WMO waliwasilisha mada kuonyesha hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa
program hii.
Mkutano ulikuwa
na maazimio kadhaa ikiwa ni pamoja na
kuharakisha utekelezaji wa program hiyo ya anga za juu. Kuboresha rasimu ya
utekelezaji inayoandaliwa kwa kujumuisha uzoefu wanchi zilizowasilisha mada
katika kikao hicho. Aidha suala la kujengewa uwezo (capacity Building)
lilionekana kuwa la muhimu hasa katika kuamua hatua ya kuanza kutekeleza
program hiyo kati ya hatua tatu zilizoainishwa ambazo ni “Ground Segment, Application Segment and Space segment”
Kikosi kazi cha program ya
Anga za juu cha AMCOMET (AMCOMET task force on African Meteorological Space Programme) kinaundwa na Tanzania (Mwenyekiti), Afrika ya
Kusini (Rapporteur), Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Nigeria na
Algeria.
IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI-AFISA MAHUSIANO TMA
No comments:
Post a Comment