Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Pombe Magufuli (wakwanza kulia) akifanya ukaguzi katika mradi wa ujenzi wa Daraja
la Kigamboni. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mfuko wa Hifadhii ya Jamii
(NSSF), Dkt. Ramadhan Dau. Mradi wa Ujenzi wa Daraja hilo umefikia Asilimia 85,
na unatarajiwa kukamilika mwezi wa tisa mwaka huu.
Taswira ya mbele ya Daraja la Kigamboni ambalo
linatajajiwa kumamilika mwezi wa Tisa.
Kazi za Ujenzi wa Daraja la Kigamboni ukiendelea kwa
kasi
Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli akikagua moja ya nguzo za barabara za juu flyovers katika maingilio ya Daraja la Kigamboni. Katika eneo hilo
kutajengwa barabara za juu ili kuruhusu magari kupita kwa urahisi wakati wa
kuingia na kutoka katika daraja hilo.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli akiwa ameambatana na Watendaji mbalimbali wa Wizara ya Ujenzi pamoja
na NSSF wakifanya ukaguzi wa ghafla
katika mradi wa ujenzi wa daraja la
Kigamboni.
Meneja Mradi wa Ujenzi
Daraja la Kigamboni kutoka NSSF, Karim Mataka wakwanza kulia akitoa maelezo ya
Ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli (wapili kulia) akikagua eneo la barabara za kuingia katika Daraja la
Kigamboni.
Sehemu ya barabara za
Maingilio ya Daraja la Kigamboni zikiwa katika hatua za mwisho kukamilika.
Sehemu ya Katikati ya
Daraja la Kigamboni kama inavyoonekana. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha
Mawasiliano Wizara ya Ujenzi
No comments:
Post a Comment