Mkurugenzi
wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully
Mwambapa akifungua mkutano wa wanahisa wa benki hiyo katika Hoteli ya
Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
Katibu
wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akizungumza wakati wa mkutano wa
wanahisa uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi yaWakurugenzi ya
Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza katika
mkutano huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na baadhi ya wanahisa
wa benki hiyo kuhusu kuanza rasmi kwa mchakato wa uuzaji wa hisa stahili za
benki hiyo unaoanza Juni 26 hadi Julai 16. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na baadhi ya
wanahisa wa benki hiyo kuhusu kuanza rasmi kwa mchakato wa uuzaji wa
hisa stahili za benki hiyo unaoanza Juni 26 hadi Julai 16. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa benki hiyo pamoja na wanahisa wakimsikiliza Dk. Charles Kimei.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB na wanahisa wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB na mameneja wa matawi wakiwa katika mkutano huo.
Meza Kuu.
Dar es Salaam, Tanzania
BENKI
ya CRDB, imetangaza kuanza rasmi kwa mchakato wa uuzaji wa Hista Stahili kwa
wanahisa wake, unaofunguliwa Juni 26 na kuhitimishwa Julai 16, ili kuongeza
mtaji wake wa uendeshaji.
Hisa Stahili ni zile za
ongezeko zinazotolewa au kuuzwa kwa wanahisa wa benki hiyo kwa mfumo wa hisa
moja mpya kwa kila hisa tano anazomiliki.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa mauzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema
kuwa baada ya maazimio ya wanahisa wake wote katika Mkutano Mkuu uliopita.
“Bodi ya Wakurugenzi wa Benki
ya CRDB, imeidhinisha kuingiza sokoni hisa mpya 435,306,432 kwa ajili ya
wanahisa wake ambapo kila hisa moja itauzwa kwa shilingi 350, hivyo kusanyo
tarajiwa la mtaji mpya litakuwa ni sh. 152,357,251,200,” alisema Dk. Kimei.
Alibainisha kuwa fedha hizo
zitakazopatikana baada ya mauzo ya hisa zitatumika kwa mambo kadhaa, ikiwamo
uboreshaji wa njia za kutolea huduma kwa wateja wa benki hiyo.
“Mwanahisa atakayekuwa na sifa
za kupokea kupokea hisa hizi ni yule tu atakayekuwa kwenye kumbukumbu za vitabu
vya benki mpaka kufikia Alhamisi Juni 18 mwaka huu ambayo ilikuwa siku ya
mwisho ukusanyaji kumbukumbu hizo,” alifafanua Dk. Kimei.
Aliongeza kuwa CRDB inahitaji
kuongeza mtaji wake ili kufikia malengo yake ya kibiashara, ikiwamo upanuzi wa
mtandao na ununuzi mitambo ya uendeshaji.
“CRDB imeona hii ndio njia
sahihi na bora zaidi, kwani licha ya kuongeza mtaji, pia inatoa fursa kwa
wanahisa wetu kuongeza hisa zao sambamba na umiliki wao wa benki hii,” alibainisha
Dk. Kimei.
No comments:
Post a Comment