Wednesday, June 10, 2015

Balozi Seif Iddi afunga mafunzo elekezi ya siku Tano ya Viongozi na watendaji wa CCM, Zanzibar

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif akikaribishwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Nd. Moh’d Omar Nyawenga kuyafunga Mafunzo elekezi ya siku 5 kwa Viongozi na watendaji wa CCM kuanzia ngazi ya Matawi hadi Mkoa Mjini yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Dolfin By Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.
Katibu wa UWT Wilaya ya Mjini Bibi ASHA Mzee Khamis akizoa maazimio ya washiriki wa mafunzo elekezi ya Viongozi na watendaji wa CCM kuanzia ngazi ya Matawi hadi Mkoa Mjini mbele ya mgenzi rasmi Balozi Seif.
Katibu wa CCM Jimbo la Magomeni Nd. Makame Khamis Ame akiwa miongoni mwa washiriki wa mafunzo elekezi ya Viongozi na watendaji wa CCM kuanzia ngazi ya Matawi hadi Mkoa Mjini akipokea cheti kutoka kwa Balozi Seif mara baada ya kumaliza mafunzo yao hapo Dolfin Bay Hoteli Kizimkazi.
Washiriki wa elekezi wa Matawi hadi Mkoa Mjini wakila kiapo kukitumikia vyema chama cha Mapindizi mara baada ya kumaliza mafunzo yao yaliyohitimishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif hapo Dolfin Bay Hoteli Kizimkazi.
Balozi Seif akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Chama cha Mapinduzi kuanzia ngaz\i ya Matawi hado Mkoa Mjini wakati akiyafunga mafunzo yao elekezi yaliyofanyika Dolfin Bay Hoteli Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unaguja. Kushoto ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kusini ambae pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Nd. Vuai Mwinyi na kulia ya Balozi ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Nd. Moh’d Omar Nyawenga.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo elekezi ya chama cha Mapinduzi kutoka Matawi hadi Mkoa wa Mjini Magharibi yaliyofanyika Dolfin Bay Hoteli Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja. Kulia ya Balozi Seif ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Nd. Moh’d Omar Nyawenga na kushoto yake ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kusini Vuai Mwinyi na mwenzake wa kamati ya SIsa Wilaya ya Mjini Kanal Mstaafu Abdi Mahmoud Mzee. Picha na – OPMR – ZNZ.

Viongozi na Watendaji wa Chama cha Mapinduzi wana jukumu kubwa wanalopaswa kulisimamia katika kuwaelimisha Wananchi juu ya kuwachagua Viongozi wanaozingatia maadili, nidhamu pamoja na upendo wa kuwatumikia vizuri.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akiyafunga mafunzo elekezi ya siku Tano yaliyoshirikisha Viongozi na watendaji wa CCM kuanzia ngazi ya Matawi hadi Mkoa wa Mjini  yaliyofanyika katika Hoteli ya Dolfin Bay Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.

Balozi Seif alisema kuchaguwa Viongozi matapeli na wababaishaji ni tabia chafu ya kuipelekea jamii mazonge na matatizo yanayochangia kuvuruga mikakati na harakati zao za kujiletea maendeleo.

Alisema Tabia ya baadhi ya Viongozi pamoja na Watendaji wa Chama kuanzia ngazi ya Matawi hadi Mikoa ya kuwabeba  mapema watu walioamuwa kuomba nafasi ya kugombea kuteuliwa kushika nyadhifa mbali mbali ni kwenda kinyume na Katiba pamoja na kanuni za Chama hicho.

Alitahadharisha kwamba Wanachama wa chama cha Mapinduzi hasa wakati huu wa kuelekea kwenye harakati za uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba lazima wasimame imara katika kukichunga chama chao kuvamiwa na watu wanaoangalia maslahi yao zaidi.

Akimkaribisha Mgeni rasmi kufunga mafunzo hayo Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Ndugu Moh’d  Omar Nyawenga alisema washiriki wa mafunzo hayo wamejipanga kuanzisha miradi ya kiuchumi ili kujenga uwezo wa utendaji ndani ya maeneo yao.

Mafunzo  Hayo elekezi ya siku Tano yaliyowashirikisha Viongozi na watendaji  116 wa CCM kuanzia ngazi ya Matawi hadi Mkoa wa Mjini yalijumisha masomo 12 ambayo ni pamoja na kuhakikisha CCM Inaendelea kushika dola kwenye uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
10/6/2015.

No comments: