Thursday, May 14, 2015

WIZARA YA FEDHA YAWAPA SEMINA WAANDISHI WA HABARI JUU YA MRADI WA MABORESHO YA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma akifafanua jambo wakati wa warsha ya siku tano kuhusu mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli Njuweni Kibaha. Bi.Ingiahedi alisema kuwa Serikali ya Tanzania ilianzisha mradi huo kwa madhumuni ya kuimarisha mifumo ya matumizi ya fedha katika ngazi zote.  Mradi huu umekuwa wa awamu 4 kutokana na mafanikio yanayojitokeza na changamoto.

Alisema kuwa Mpaka sasa mradi huo umepata mafanikio makubwa hasa ya  kuweka mfumo mzuri wa malipo, muda wa kupitishwa kwa bajeti ya Taifa umeimarika na fedha zinatoka kwa  wakati,Alibainisha kuwa bajeti ya mwananchi inatangazwa katika Tovuti ya Wizara ya fedha na kuwa mfumo wa malipo umefika mpaka katika Serikali za Mitaa.
Washiriki wa warsha kuhusu maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli ya Njuweni Kibaha.
 Baadhi ya waandishi wakiwa katika warsha ya siku tano kuhusu kuhusu mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli ya Njuweni Kibaha. 

===========  =======  ========
Serikali ya Tanzania ilianzisha mradi huo kwa madhumuni ya kuimarisha mifumo ya matumizi ya fedha katika ngazi zote.  Mradi huu umekuwa wa awamu 4 kutokana na mafanikio yanayojitokeza na changamoto.

Awamu ya kwanza (I) ilikuwa kutoka mwaka
1998 – 2004 huu ulikuwa na malengo ya kudhibiti matumizi,
kuweka nidhamu ya fedha pamoja na kukuzana kuimarisha uchumi mpana.

Awamu ya pili (II)
ilikuwa kutoka mwaka 2004 – 2008 malengo ya mradi huo yalikuwa ni kuimarisha na kuendeleza mifumo na njia zinazotumika katika malipo ya fedha za umma kwa kutumia njia rahisi na nyepesi. Aidha awamu hiyo ilizingatia pia uimarishaji wa njia ya ukusanyaji mapato na jinsi ya kuweka mbinu ya kuzitumia rasilimali fedha na kuweka mikakati ya kipi kianze kwanza.

Awamu ya tatu (III)
ilikua kuanzia 2008 – 2011, mradi huu ulikua na malengo ya kuhakikisha kuna kuwa na upatikanaji rasilimali fedha kutoka katikaTaasisi mbalimbali za kifedha.

Awamu ya nne (IV)
ya mradi ni kuanzia June 2012, mradi ulizinduliwa na kuanza rasmi tarehe 1 Julai, 2012. Madhumuni ya mradi huu katika awamu ya nne umelenga katika kuonge za nguvu ambayo itawezesha kufikia malengo ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, 
 hiyo inaenda sanjari na mpango wa maendeleo wa miaka mitano yaani 2011/2012 – 2015/2016 na MKUKUTA (MkakatiwaKukuzauchumi Tanzania)/ MKUZA (Mkakati wa Kukuza uchumi Zanzibar), ili kufika malengo ya ukuaji wa uchumi.

Mafanikio ya mradi huu katika kuimarisha matumizi mazuri ya fedha za umma yatafikiwa kwa kuwa na matokeo ya maeneo makuu matanokama vile, usimaiziwaukusanyajikodi, mpangowabajeti,  usimamizi wa bajeti, uwazi na uwajibikaji,  usimamizi wa matumizi ya fedha zilizopangwa kutumika na kugundua matumizi ya nayoweza kujitokeza baadae na mabadiliko ya Uongozi pamoja na uangalizi na mawasiliano kwenye mambo yafedha. 

Maboresho ya fedha za umma yanaenda sanjari na maboresho katika sekta za umma ambayo yanalenga kuimarisha utendaji bora na makini katika kutoa huduma  ambazo zinakuza uchumi ulioimara.

Mpango wa maboresho ya fedha za umma awamu ya nne (IV) pia utaangalia/utalenga kwenye kuwajengea uwezo wale wote wanaofanya shughuli za maboresho ya fedha za umma katika Nyanja tofauti tofauti. Kufuatilia na kufanya tathmini katIka uwigo uliowekwa kwa kuangalia vipau mbele ambavyo vitatoa muelekeo na kufikia matokeo mazuri.

Kuhakikisha kuwa ripoti za fedha zinazotolewa zinakuwa za aina moja bila kuwa na utofauti wa aina yoyote. Kuwa na uongozi mzuri ambao umepanga vizuri Taasisi za fedha.  Kuzilenga na kuzipa nguvu wakala ambazo zinaguswa moja kwa moja katika mifumo ya fedha za umma. Mradi huu unafadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB na Bank ya Dunia (WB),DfID, CIDA, DENMARK, IRELAND na KFW. Hawawote walisaini makubaliano ya kuchangia katika mradi huo.

Mpaka sasa hivi mradi huu umepata mafanikio makubwa hasa ya  kuweka mfumo mzuri wa malipo, muda wa kupitishwa kwa bajeti ya Taifa umeimarika na fedha zinatoka kwa  wakati.  Aidha bajeti ya mwananchi inatangazwa katika Tovuti ya Wizara ya fedha.Mtandao wa malipo umefika mpaka katika Serikali za Mitaa.

No comments: