Monday, May 25, 2015

UNFPA WAKABIDHI MSAADA WA GARI LA WAGONJWA, JENGO NA VIFAA VYA UPASUAJI GEITA

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA) limekabidhi msaada wa gari la wagonjwa lenye thamani ya shilingi milioni 80 katika kituo cha afya cha Masumbwe kilichopo katika Wilaya mpya ya Mbogwe Mkoani Geita.

Shirika hilo limetoa vifaa vya kutoa huduma ya upasuaji vyenye thamani ya shilingi milioni 250 katika kituo hicho mbali na kutumia shilingi zaidi ya shilingi milioni 100 kusadia ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho.

Misaada hiyo kwa pamoja ilikabidhiwa Jumamosi iliyopita katika halfa ambaye mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.

Majaliwa alishuruku UNFPA kwa msaada huo na kutaka utumike vizuri ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

“ Nimeona vifaa vya hospitali vingi na vya gharama kubwa, sasa ni wajibu wetu kuvitunza na kuvitumia vizuri. Mfano gari tu limegharimu shilingi milioni 80. Huu ni msaada mkubwa sana na kwa niaba ya serikali nawashukuru sana UNPFA, tutaendelea kushirikiana”, alisema Majaliwa .

Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwaagiza vingozi wa Halmashuri ya Wilaya ya Mbogwe kuhakikisha kuwa gari hilo linatumika kusafirisha wagonjwa tu na sio vinginevyo.
DSC_0062
Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla (kushoto) na Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt.Rutasha Dadi wakipitia ratiba ya sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ambapo kitaifa yamefanyika katika Wilaya Mbogwe, Geita.

“ Gari hili litumike kwa matumizi ya wagonjwa tu. Sitegemei kusikia kuwa linapeleka wafanyakazi sokoni kununua nyanya. Na Mkurugenzi atenge bajeti ya mafuta ya gari hili muda wote”, aliagiza Majaliwa.

Hafla ya makabidhiano ya misaada hiyo ilienda sambamba na maadhimisho ya siku ya kutokomeza tatizo la ugonjwa wa Fistula duniani yaliyofanyakia kitaifa katika viwanja vya shule ya msingi Masumbwe katika Wilaya ya Mbogwe , Mkoani Geita.

Akizungumuza katika hafla hiyo Mwakilishi msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dkt. Rutosha Dadi alisema msaada wa vifaa walivyotoa utasadia kumaliza tatizo la Fistula na kuboresha huduma zingine za afya .

“ Tumefanya ukarabati mkubwa sana katika jengo la upasuaji na kutoa vifaa vya kisasa kama vile Ultrasound”, alisema Dkt. Dadi.
DSC_0072
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha (wa nne kulia) akitoa salamu na kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na umati wa wakazi wa Mbogwe waliokusanyika kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Meneja wa miradi ya AMREF, kanda ya ziwa Dkt. Awene Gavyole, Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi, Katibu Tawala wa mkoa wa Geita, Charles Palanjo, mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa, Mganga Mkuu wa mkoa wa Geita, Joseph Kisalla, Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon pamoja na Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Mh. Augustino Masele.
DSC_0204
Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa yamefanyika wilayani Mbogwe mkoa wa Geita.
IMG_1150
Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akisisitiza jambo wakati wa kutoa salamu za Umoja wa Mataifa.
DSC_0149
Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla akizungumza na wakazi wa Mbogwe ambapo aliwataka kufika katika vituo vya afya vilivyokaribu na makazi yao kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa Fistula pindi wanaonapo dalili na moja kwa moja kuwasiliana na Hospitali yake inayotoa huduma za matibabu bure ikiwemo usafiri na malazi mpaka mgonjwa anapopona na kumrejesha anakoishi.
IMG_1089
Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon akitoa salamu za Vodacom ilivyobega bega katika kupamba na ugonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 100/- kutoka Taasisi ya Vodacom Foundation kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa Fistula nchini wakati wa maadhimisho yanayofanyika kila mwaka Mei 23.
DSC_0248
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh. Kassim Majaliwa (kulia) akikabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon, kwa niaba ya hospitali ya CCBRT kwa ajili ya kampeni ya kutokomeza Fistula nchini wakati wa maadhimisho ya Kimataifa ya Fistula yaliyofanyika kitaifa katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita mwishoni mwa wiki, Katikati ni Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla.
DSC_0254
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- kwa Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla (kushoto) na anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon.
DSC_0182
Bi. Esther Ernest akitoa ushuhuda wake baada ya kuteseka na ugonjwa wa Fistula kwa takribani miaka 8 na jinsi jamii ilivyomnyanyapaa akiwemo mume wake hadi alipopatiwa matibabu na kupona kabisa hali iliyompelekea kurudisha furaha na nuru katika uso wake wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa imefanyika wilayani Mbogwe mkoani Geita.
IMG_0928
Kikundi cha maigizo cha Mrisho Mpoto kikitoa elimu kwa njia ya maigizo jinsi Wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Fistula wanavyonyanyapaliwa na waume zao na kudhalilishwa kwa jamii ikiwemo kuitwa majina ya kila aina kutoka na kutokwa na haja ndogo muda wote bila breki.
IMG_0947
Mwigizaji wa kikundi cha sanaa za maigizo cha Mrisho Mpoto akilia kwa uchungu kutokana na kuugua ugonjwa wa Fistula na kunyanyapaliwa na mumewe wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa imefanyika wilayani Mbogwe mkoani Geita.
IMG_0969
Msanii mahiri wa sanaa ya kughani mashairi nchini Mrisho Mpoto akimliwaza Mwanamke anayenyanyapaliwa na mumewe kutokana na kuugua ugonjwa wa Fistula ambao unatibika bure kabisa bila gharama yoyote na Hospitali ya CCBRT.
IMG_1006
Mume wa mwanamke anayeumwa Fistula wakisoma vipeperushi vya CCBRT vinavyotoa elimu, dalili na nini cha kufanya pindi unapojigundua ni Fistula pamoja na jirani yake wakati wa mchezo wa maigizo kwenye maadhimisho hayo.
IMG_1009
Mrisho Mpoto akiendelea kutumia sanaa ya maigizo kuelemisha umati wa wakazi wa wilaya ya Mbogwe waliohudhuria maadhimisho hayo.
IMG_1030
Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kushoto) na Mganga Mkuu wa wilaya ya Geita, Dkt. Joseph Kisalla wakifuatilia igizo la unyanyapaa kwenye jamii kwa wanawake wanaougua Fistula wakati wa maadhimisho hayo.
DSC_0170
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akifurahi jambo kwenye maadhimisho hayo.
DSC_0235
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akimpongeza Balozi wa Fistula CCBRT, Elizabeth Jacob na kumkabidhi pesa taslimu Sh. 20,000/- kama motisha ya kazi anazofanya za kuwasafirisha wagonjwa wa Fistula jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
DSC_0238
Balozi wa Fistula CCRT, Elizabeth Jacob akionyesha pesa alizokabidhiwa kama zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0241
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akimpongeza na kumkabidhi pesa taslimu sh. 100,000/ kama motisha ya kazi anazofanya za kuelimisha jamii kwa kutumia sanaa na maigizo Mrisho Mpoto aliyekuwa akisheresha sherehe hizo.
DSC_0023
Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla ( kushoto) na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kulia) wakimuangalia mtoto Nyambole Kulubone mwenye tatizo la mdomo wa Sungura akiwa amebebwa na mama yake Mariam Sanda (22) Mzazi huyo aliyehudhuria katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula aliahidiwa na Bi. Haika Mawalla (kushoto) mtoto wake atatibiwa bure katika hospitali CCBRT baada ya kusikia matangazo jirani na eneo liliofanyika sherehe hizo ambapo kitaifa katika Wilaya Mbogwe Geita.
DSC_0025
Mariam Sanda (22) akiwa amembeba mwanae mwenye mdomo wa Sungura.
DSC_0098
Baadhi ya umati wa wakazi wa Mbongwe waliohudhuria maadhimisho hayo.
IMG_0958
DSC_0101
IMG_0897
IMG_0891
IMG_1359
Burudani kutoka kwenye kikundi cha Mrisho Mpoto.
IMG_1393
DSC_0272
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Petr Shilogile (kushoto) akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa uliofadhiliwa na Shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania na ujenzi kusimamiwa na AMREF kabla ya kuzinduliwa rasmi. Kulia ni Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Mh. Augustino Masele.
DSC_0275
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akifunua kitambaa kuzindua cha jiwe la msingi huku Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi (kulia) akishuhudia tukio hilo.
DSC_0277
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye jiwe la msingi.
DSC_0281
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua jengo la upasuaji huku Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akishuhudia tukio hilo.
DSC_0282
Sasa limezinduliwa rasmi.
DSC_0287
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile (kulia) akitoa maelezo kwenye chumba cha kujifungulia kina mama kilichowekwa vifaa vyote muhimu kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto). Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
DSC_0289
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akitoa maelezo ya mashine ya kisasa ya kuongezea damu wakina mama watakaokua wakijifungulia kwenye kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0318
Wafadhali wa ujenzi na vifaa kwenye kituo hicho Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akifafanua jambo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa baada ya kuzinduliwa kituo hicho cha afya. Kulia ni Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile.
DSC_0340
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akielezea changamoto waliozokuwa nazo hapo awali za kipimo cha "Ultra sound" kilichonunuliwa na UNFPA ambacho hivi sasa kitapatikana kituoni hapo kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0360
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua gari la wagonjwa (Ambulance) lenye thamani ya Tsh. Milioni 80 kwa ajili ya kubebea wakinamama wajawazito na watoto wanaohitaji huduma za dharula za upasuaji kutoka vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika wilaya ya Mbogwe kwa ufadhili wa Shirika la UNFPA. Kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
DSC_0362
Mh. Kassim Majaliwa na Dkt. Rutasha Dadi wakipiga makofi.
DSC_0373
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akijaribu gari hilo.
DSC_0386
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akitoa angalizo la matumizi mabovu kwa DED wa Mbogwe na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya.
DSC_0388
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi funguo za gari hilo la kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, Abdala Idd Mfaume.
DSC_0411
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe mara baada ya makabidhiano hayo.
DSC_0421
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Muhanga wa Fistula, Bi. Ester Ernest (walioketi kulia), Balozi wa Fistula CCBRT, Bi. Elizabeth Jacob (wa pili kushoto), Katibu Tawala mkoa wa Geita, Charles Palanjo (kushoto) na waliosimama kutoka kushoto ni Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi, MC pamoja na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

No comments: