Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI), Jaji Mstaafu, Mark Bomani akifungua warsha ya siku moja kwa wadau na wandishi wa habari za biashara, mkutano uliofanyika Ledger Plaza Bahari Beach Hotel jijini Dar es Salaam, Mei 7, mwaka huu.
Na Andrew Chale, Modewji blog
Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi Asilia na Mafuta (TEITI) Jaji Mark Boman amewataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi zenye lengo la kuielimisha jamii hasa pindi wanaporipoti habari za sekta ya madini hapa nchini.
Akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari za biashara na uchumi ya siku moja iliyofanyika hivi karibuni Ledger Plaza Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam, Jaji Bomani alisema taarifa sahihi hasa za masuala ya uchumi zinahitajika kwani zikitolewa tofauti zinaweza kusababisha mkanganyiko kwa wananchi.
Alisema taasisi hiyo ilianzishwa kuwa lengo la kufuatilia sekta ya madini kwani hapo awali ilionekana kutowanufaisha wananchi.
“Awali kuliwa na mkanganyiko wa kwamba sekta ya madini haiwanufaishi wazawa hivyo Serikali ilichukua hatua na kuunda kamati ya kushughulikia tatizo hilo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hiyo ya madini,”alisema.
Alisema chombo hicho kilianza kutoa ripoti za ufuatiliaji wa sekta za Serikali kwa makini na fedha zinazolipwa. Alisema Ripoti ya nne ambayo ni ya mwaka 2014 inaonyesha kwamba mapato ya Serikali yamekuwa yakiongezeka kila mwaka tofauti na ripoti ya kwanza iliyokuwa na hitilafu ya Dola milioni 30.
Alisema mafanikio ya utaratibu huo umesaidia taasisi za Serikali kuhakikisha kwamba kila fedha inayotoka au kulipwa inakuwa ya maandishi ili kuwa na taarifa sahihi.
Afisa mahusiano Mkuu wa TEITI, Catherine Mbatia akimkaribisha rasmi Mwenyekit wa TEITI, Jaji Mark Boman kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Warsha hiyo iliyowakutanisha wandishi wa habari za biashara na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa madini.
Naye Mjumbe wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) George Kibakaya alieleza kuwa, kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa ni futi za ujazo tirioni 55 hivyo ni vyema kujipanga vizuri ili kuhakikisha kinakuza uchumi wa nchi.
Aidha, katika semina hiyo wandishi wa habari walipata pia fursa ya kujifunza namna ya upatikanaji wa data kwa njia ya mtandao huku wakishahuriwa kuwa pindi wanahabari watafutapo data, kuweza kuwasiliana na wataalam husika iliondoa mkanganyiko ikiwemo idara za kifedha, wataalamu wa hesabu pamoja na mifumo sahihi ya data hasa kupitia mifumo ya inteneti.
Mafunzo hayo ya kuripoti habari kwa kutumia uchambuzi wa data, yalitolewa na Samuel Osei Bekoe kutoka taasisi ya NRGI ya nchini Ghana ambaye alitoa wito kwa wandishi wa habari wa Tanzania hasa wanaotaka kuandika habari za kiuchunguzi katika uripoti wa mahesabu na data kuzingatia vyanzo vya taarifa vya kina na vyenye uhakika.
Ambapo alishahuri kuwa licha ya upatikanaji wa data hizo kuwa mgumu na wa sili kwa baadhi ya sekta, aliwataka wandishi kutumia vipengele muhimu na kwa ufupi bila kuweka mambo mengi ambayo yataweza kumchanganya msomaji.
Akitolea mfano wa taarifa za kiuchumi kwa Tanzania ama nchi zingine, ambapo endapo wataingia kwenye mitandao ya taasisi ya kifedha, Ikiwemo IMF, Benki kuu na zingine zimekuwa na uwazi hivyo wanaweza kupata huko taarifa ambazo zinaweza kuwasaidia kuripoti na kuleta changamoto katika nchi huku akisisitiza kutaja chanzo cha taarifa ama ripoti hiyo.
Pia wadau mbalimbali wakiwemo wataalamu wa madini na wandishi wa habari walitoa mada mbalimbali zilizojadiliwa kwa kina katika semina hiyo kwa mfumo wa mdaharo.
Meneja Mahusiano, Alex Modest, (kulia)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika semina hiyo watatu kulia ni Meneja mikakati kutoka (TBDC) George Kibakaya (kushoto) Mwenyekiti TEITI,Jaji Bomani,wa pili kushoto mwandishi mchambuzi, John Bwire,(katikati) ni Halfani Halfani kutoka (Oil Gas Association Tanzania-OGAT).
Afisa mahusiano Mkuu wa TEITI, Catherine Mbatia akielezea juu ya TEITI, wakati wa Warsha hiyo iliyowakutanisha wandishi wa habari za biashara na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa madini.
Mwenyekiti TEITI, Jaji Bomani (kushoto ) akichangia mada katika warsha hiyo, wengine ni Mwanahabari na mchambuzi John Bwire, akifuatiwa na Halfani Halfani wa OGAT, Meneja mikakati kutoka (TBDC) George Kibakaya pamoja na Godvictor kutoka kampuni ya madini ya Geita.
Wadau wa sekta ya madini na wanahabari wakifuatilia mada katika warsha hiyo
Mwandishi Mwandamizi wa Mtandao wa Modewji blog, Andrew Chale (kushoto) akifuatiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Business Times, Damas Makangale, pamoja na wandishi wengine waki 'note' vitu muhimu kwenye warsha hiyo.
Mwandishi wa habari na mchambuzi, John Bwire akitoa mada katika warsha hiyo juu ya umuhimu wa kuwajengea uwezo wajasiliamari wa ndani ili kunufaika na sekta ya madini tuliyonayo
Godvictor kutoka kampuni ya Madini Geita, akitoa mada juu ya uwazi wa makampuni hapa nchini hasa katika sualala ulipaji wa kodi na mifumo ya kisheria ya biashara hiyo ya sekta ya madini ambapo alibainisha kuwa baadhi ya makampuni yamekua yakitumia sheria ya Kimataifa hivyo uwepo wa baadhi ya makapuni hayo kutoweka wazi mikataba yao ni kuogopa ushindani katika soko la Kimataifa.
Mwanahabari mwandamizi Joseph Mwamunyange (kushoto) akiwa na wadau wa sekta ya madin, Kulia ni mtaalam wa uchambuzi wa data katika sekta ya madini kutoka taasisi ya Global Witness Rachel Owens wakati wa warsha hiyo
Picha juu na chini Wanahabari wakiendelea na majukumu yao .. kwenye warsha hiyo
Mwanahabari Joseph Mwamunyange akiendesha mjadala juu ya uwazi katika masuala ya upatikanaji wa habari kwa uwazi hasa za sekta nyeti za madini na fedha.
Prof. Handley Mwafenga (TMAA) akitoa mada juu ya uwajibikaji na uwazi katika sekta ya madini katika warsha hiyo..
Mjumbe wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) George Kibakaya ali
Wadau wa sekta ya madini wakichangia mada katika warsha hiyo..
Dr. Camillius Kasalla kutoka (CSO) akitoa mada namna ya vyama vya kijamii NGOs juu ya umuhimu wake katika ufuatiliaji wa mambi ya uwazi katika sekta ya madini..
Samuel Osei Bekoe kutoka taasisi ya NRGI ya nchini Ghana akitoa mafunzo kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) ya namna ya kupata habari kupitia mitandao ya intaneti hasa ya takwimu na mahesabu ya masuala ya fedha na madini.
..mafunzo hayo
Samuel Osei Bekoe kutoka taasisi ya NRGI ya nchini Ghana akitoa mafunzo kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) ya namna ya kupata habari kupitia mitandao ya intaneti hasa ya takwimu na mahesabu ya masuala ya fedha na madini.
Mwenyekiti wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI), Jaji Mstaafu, Mark Bomani akiwa na vitabu vya ripoti ya nne, vikiwa katika lugha mbili ya kiswahili na kiingereza akivionesha kwa wadau na wandishi wa habari za biashara, mkutano uliofanyika Ledger Plaza Bahari Beach Hotel jijini Dar es Salaam, Mei 7, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment