Wanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho,Mariam Rajabu na Faraja Abdallah wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza (kulia) akiwafafanulia jambo kuhusiana na matumizi ya kompyuta mpakato zilizokabidhiwa na mfuko huo kwa kushirikiana na Samsung ikiwa ni msaada kwa wanafunzi wa shule hiyo kuweza kupata mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia kompyuta .
Baadhi ya wanafunzi wa wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam,Juma Hassan, Fadhil Komba na Francis Mwaimbamba wakijifunza masomo mbalimbali kupitia kompyuta mpakato zilizokabidhiwa na mfuko huo kwa kushirikiana na Samsung ikiwa ni msaada kwa wanafunzi wa shule hiyo kuweza kupata mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia kompyuta.
Mkuu wa Biashara Endelevu wa Kampuni ya Vodacom Suraya Hamdulay(kushoto) akifafanuliwa jambo na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam, Bernard Yohana, kuhusiana na somo la kompyuta wakati wa kukabidhiwa rasmi kompyuta hizo pamoja na vifaa vya maabara ya kompyuta ikiwa ni msaada uliotolewa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung kwa ajili ya kupata mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia kompyuta shuleni hapo.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam, Bernard Yohana, akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Biashara Endelevu wa Kampuni ya Vodacom Suraya Hamdulay(kushoto)akimsisitiza jambo kuhusiana na somo la kompyuta wakati wa kukabidhiwa rasmi kompyuta hizo pamoja na vifaa vya maabara ya kompyuta ikiwa ni msaada uliotolewa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung kwa ajili ya kupata mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia kompyuta shuleni hapo.
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam Deogratias Haule, akiongea na wanafunzi wa kidato cha tatu kuhusiana na kufuata matumizi yaliyo bora ya kompyuta mpakato na vifaa vingine vilivyokabidhiwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung kwa ajili ya kupata mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia kompyuta shuleni hapo.
Benard Yohane mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Makumbusho jijini Dar es Salaam alionekana kuwa na mshangao wa furaha kwa mara ya kwanza kusoma somo la bailojia kwa vitendo kwa njia ya kompyuta wakati taasisi ya Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung ilipotoa msaada wa kompyuta 25,Screen kubwa ya kufundishia na printer 1 kwa shule hiyo kwa ajili ya darasa maalumu la kufundishia kompyuta mwishoni mwa wiki.
Wanafunzi hao wameungana na wenzao wapatao 5000 kutoka shule nyingine za msingi jijini Dar es Salaam ambao wanapata wanapata elimu ya matumizi ya kompyuta kwa vitendo na kuweza kujfunza masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao wa internet.Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung zilizindua mradi huu mwaka 2013 unaojulikana kama Smart na tayari umeanza kuleta mafanikio kwa kuwawezesha baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari jijini Dar es Salaam kuingia katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.Shule ambazo zimenufaika na mradi huu ni Makumbusho,Kinyerezi,Mtakuja na Kambangwa.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo,Mkuu wa taasisi ya Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza alisema “ Siku zote tutakuwa mstari wa mbele kuhakikisha vijana wa kitanzania wanapata elimu bora kupitia mawasiliano na teknolojia.Mpango huu unawawezesha vijana kupata elimu bora na kuwaunganisha na wenzao sehemu mbalimbali duniani kote ambapo wanaweza kupata taarifa mbalimbali na maarifa kwa urahisi.
Alisema Vodacom inafanya kila jitihada kuhakikisha inaendeleza jamii katika nyanja mbalimbali kupitia mawasiliano na teknolojia hususani kwa vijana ambao wanapaswa kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambayo ndiyo yanatawala katika ulimwengu wa sasa wa Sayansi na Teknolojia.
“Mawasiliano mazuri huwezesha watu kupata taarifa mbalimbali zinazotokea katika mazingira yao walipo na sehemu za mbali kwa urahisi.Kwa wanafunzi kompyuta zinasaidia sana kupata maarifa kupitia mtandao wa internet.Nawahasa wanafunzi wa Makumbusho msome kwa bidii na mtumie vizuri fursa hii kutafuta elimu na msiogope kusoma masomo ya sayansi maana mambo yote hivi sasa yamerahisishwa kupitia teknolojia hii ya kompyuta”.Alisema.
Mwalimu Mkuu wa sekondari ya Makumbusho,Bw.Deogratias Haule ameshukuru kwa msaada huo na kusema kuwa mradi huu ni muhimu na utawawezesha wanafunzi katika shule yake kuingia katika ulimwengu wa kompyuta na hivi sasa wanaweza kumudu vizuri somo hilo kwa kuwa wanalisoma kwa nadharia na vitendo.
Naye Afisa Mwandamizi anayesimamia shughuli za kijamii kutoka Vodacom Group,Suraya Hamdulay, alisema mradi wa Smart wa kuwawezesha wanafunzi kupata elimu kwa njia ya kompyuta ni ukombozi mkubwa na utawawezesha wanafunzi wengi kutobaki nyuma katika ulimwegu huu wa sayansi na teknolojia.”Tunaelewa umuhimu wa kuendeleza jamii tunazofanyia kazi ndio maana leo tumetoa msaada huu kwa shule ya Makumbusho na tuna imani wanafunzi watafaidika kwa msaada huu na tutafanya jitihada kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wananufaika”.Alisema.
Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake wenzake Benard Yohane alishukuru kwa msaada na kusema utawasaidia kujua somo la kompyuta,“Tumekuwa tukijifunza somo la kompyuta kwa nadharia na kwa kuwa tumepata kompyuta hivi sasa tutasoma somo hilo kwa vitendo na ndoto yetu ya kuingia katika ulimwegu wa sayansi na teknolojia imetimia”.
Mwanafunzi mwingine Subira Suleimani aisema mradi huu ni wa muhimu na unaweza kuleta mapinduzi makubwa ya kuwawezesha wanafunzi wengi wanaosoma shule za kawaida hususani zinazomilikiwa na serikali na zilizopo katika mazingira ya vijijini kuweza kupata elimu kwa njia ya kompyuta na ktobaki nyuma katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia “Shule nyingi za serikali hazina kompyuta na nyenzo za kisasa za kufundishia kama zlivyo shule ningi za binafsi”.Alisema.
No comments:
Post a Comment