Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (kushoto) akizungumza na wandishi wa Habari (pichani hawapo) baada ya hitimisho la Mkutano wa nne wa mafunzo ya Upasuaji wa Ubongo , uti wa mgongo na mishipa ya fahamu, Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid, uliomalizika hivi karibuni. ambapo wakishirikiana na Wataalamu madaktari bingwa wa Chuo cha Weill Cornell toka Marekani kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya kisasa, ambapo Watanzania 21 wamefanyiwa upasuaji wa magonjwa hayo wakishirikiana na madaktari toka Tanzania , Uganda, Rwanda, Southi Afrika, Marekani na Ulaya. Dokta Othman Kiloloma, alimshukuru Rais Jakaya Kikwete ambaye aliye waweka karibu na wenzao wa Chuo cha Marekani na kuwashukuru wenzao wa chuo cha marekani kwa kuwawezesha kufanyika upasuaji huo. (wakwanza kulia) ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dk.Hamisi Shabani,ambaye aliwaeleza waandishi hao kua mgonjwa mmoja kufanyiwa upasuaji anagharimu kiasi cha dola elfu moja za upasuaji huo nahaihusiani na mambo mengine.na katikati ni Profesa Philip Steg toka Chuo cha Marekani nayeye alipata nafasi ya kuongea na waandishi hao na kuwashukuru Wataalamu wa Moi (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa
Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (wapili) kushoto na kuanzia kulia ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dk.Hamisi Shabani anaye fatia ni Profesa Philip Steg toka Chuo cha Weill Cornell Marekani na kushoto ni Menneja ea Taasisi ta Moi Almas Jumaa.
Madaktari wakiwakatika Upasuaji na ikiongozwa Dk, Japhet Ngerageza
Mashine ya kisasa yenye thamani shilingi mil. 700 iliyotolewa msaada na Weill Cornell toka Marekani ikikumika kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania kwa Muungano wa jitihada za Rais Jakaya Kikwete
Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) wakishirikiana na madaktari bingwa wa Chuo cha Weill Cornell toka Marekani kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya kisasa ambapo wagonjwa 21 wamefanyiwa upasuaji wa magonjwa hayo. Dar es Salaam
Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa
ya Fahamu (MOI) wakishirikiana na madaktari bingwa wa Chuo cha Weill
Cornell toka Marekani wakionyeshana jambo wakati walipokuwa wafanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya
kisasa ambapo wagonjwa 21 wamefanyiwa upasuaji wa magonjwa hayo. Dar
es Salaam
Madaktari wakiwa katika chumba cha Upasuaji
No comments:
Post a Comment