Monday, May 4, 2015

MGOMO WA MABASI...ABIRIA MJINI MOSHI WAKWAMA STENDI, WAIGEUZA UKUMBI WA SINEMA...

Hivi ndivyo kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi kilivyoonekana.
Mdereva wa Hiece za kuelekea maeneo mbali mbali ya nje ya mji wa Moshi pia wameungana na madereva wengine kufanya mgomo huo.
Madereva wa Noah pia walikuwa likizo.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa magari ya abiria baada ya madereva wa mabasi hayo kugomea kusafirisha abiria hadi pale serikali takapo sikiliza matatizo yao.
Jeshi la Polisi lilikuwa likiranda huku na huko kuhakikisha hali ya usalama inakuwepo katika kituo hicho cha mabasi cha mjini Moshi/
Licha ya kwamba madereva walitagaza kufanya mgomo bado baadhi ya abiria walikatiwa tiketi wakitumaini kufanya safari.
Abiria wakiwa wamekaa wasijue la kufanya baada ya kukosa usafiri wa kuelekea mikoa mbalimbali.
Baadhi ya abiria wakiwa wamekaa kitako katika maegesho ya magari huku wakitizama Big Screen iliyopo jirani na kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
Baadhi ya abiria wakitizama kwa mbali screen hiyo.
Screen kubwa kwa ajili ya matangazo ya biashara iliyoko jirani na kituo kikuu cha mabasi ikionesha picha ya mashindano ya magari ambayo ilikuwa burudani kwa abiria baada ya kukosa usafiri kutokana na mgomo wa madereva uliotikisa nchi nzima.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

No comments: