Sunday, May 10, 2015

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI(MUWSA)YANASA MWIZI WA MAJI ENEO LA MAJENGO MJI MPYA.

Mmiliki wa nyumba moja katika eneo la Majengo kwa mtei mjini Moshi amekutwa akiwa amejiunganishia maji kinyemela na kufunika na gunia eneo ambalo alikuwa amejiunganishia.
Afisa wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,Jacob Ulotu akiondoa gunia lililokuwa limefunika sehemu hiyo ambayo kiutaratibu ilitakiwa kuwa na meta ya kusoma matumizi ya maji.
Hivi ndivyo ilivyokuwa ikionekana baada ya kuondolewa gunia.
Na maji alikuwa akitumia kama inayoonekana .
Baadhi ya maofisa wa MUWSA waliofika katika nyumba hiyo ambayo hata hivyo walifanikiwa kumkuta mmiliki wa nyumba hiyo anbaye alijitetea kuwa waliofanya wizi huo ni vijana wanaoishi katika nyumba hiyo.
Hii ndio nyumba ambayo imekutwa wiozi wa maji ukiwa unafanyika.
Fundi wa MUWSA akijaribu kukata bomba lililokuwa likipeleka maji ndani ya nyumba hiyo.
Zoezi la ukataji wa maji hayo lilisimamiwa na Afisa Uhusiano wa mamlaka hiyo Florah Nguma.
Mafundi wakifukia eneo hilo.
Eneo la nje ya nyumba hiyo ambayo wizi wa maji ulikuwa ukifanyika.

Na Dixon Busagaga wa 

Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: