Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ambapo jumla ya washindi watatu kila mwezi wanapatikana na kila mmoja kujishindia jumla ya Sh Milioni moja. Kulia ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa taasisi hiyo, Gladys John, huku kushoto akiwa ni bwana Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania. Picha zote na Mpiga Picha wetu.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHINDANO la Kopa Bayport kwa njia ya mtandao linaloendeshwa na taasisi ya
Kifedha ya Bayport Financial Services, limezidi kuchanja mbuga, baada ya wateja
watatu wa mwezi Mei kuibuka na Sh Milioni moja kwa kila mmoja, huku mikoa ya
Bukoba, Njombe na Dar es Salaam ikichanua katika droo iliyochezeshwa jana,
jijini Dar es Salaam.
Wateja hao walioshinda katika shindano hilo ni Tryphone Mashamba mkoani
(Njombe), Kisa Mboya (Dar es Salaam) na Oscar Gadawu (Bukoba) ambao wote kwa
pamoja wameibuka na Sh Milioni moja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa
www.kopabayport.co.tz, ikiwa ni huduma nzuri kutoka kwenye taasisi hiyo ya
Bayport Financial Services.
Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Gladys John katikati akichagua koponi ya mmoja wa washindi wa shindano la Kopa Bayport linaloendelea ambapo washindi watatu wamepatikana na kila mmoja kupata bahati ya kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz. Kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, wakati kushoto ni Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.
Akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema
shindano lao limepokewa vizuri na wateja wao, waliopata urahisi wa upatikanaji
wa huduma za mikopo kutoka kwenye taasisi hiyo.
Tunatafuta washindi wa kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja kwa washindi watatu kutoka Bayport Financial Services. Ndivyo wanavyoonekana kusema katika droo hiyo ambapo washindi kutoka Njombe, Dar es Salaam na Bukoba wamechanua.
Alisema awali wateja walilazimika kusafiri kuelekea kwenye tawi lao, lakini
kuanzishwa kwa tovuti hiyo, kumetoa urahisi wa ukopaji kwa kiasi kikubwa mno,
huku kila mmoja akiwa na uwezo wa kushinda endapo ataamua kutumia huduma hiyo.
“Tunashukuru kuona Watanzania wenzetu wameendelea kupata urahisi wa huduma zetu
za mikopo, maana anaweza kukopa mahala popote alipokuwapo, endapo ana kifaa
kitachomuwezesha kuingia katika mtandao wetu wa www.kopabayport.co.tz, kama
vile simu ya mkononi na kompyuta” alisema Cheyo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial
Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza
jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa
www.kopabayport.co.tz, ambapo jumla ya washindi watatu kila mwezi
wanapatikana na kila mmoja kujishindia jumla ya Sh Milioni moja. Kulia
ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa taasisi hiyo, Gladys John, huku kushoto
akiwa ni bwana Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya
kubahatisha Tanzania.
Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha,
Humud Abdulhussein, alisema promosheni hiyo ya kopabayport ni nzuri kwa wateja
na Watanzania wote wanaoweza kujikwamua kwa kupata mikopo isiyokuwa na dhamana
wala amana kutoka Bayport.
“Sisi Bodi tunachoangalia ni kanuni na vigezo vya michezo ya kubahatisha
kufuatwa, ikiwa ni upatikanaji wa washindi na namna walivyoweza kujiunga kwenye
huduma hii ambayo kila mtu anaweza kuingia anapohitaji huduma yoyote,” alisema
Abdulhussein.
Naye Meneja Huduma kwa Watejanwa Bayport Financial Services, Gladys John,
aliwataka Watanzania kuendelea kuiunga mkono Bayport kwa ajili ya kujikwamua
kiuchumi kutokana na fursa mbalimbali za mikopo isiyokuwa na amana wala
dhamana, bila kusahau Kopa Bayport inayoendelea kutolewa kwa ajili ya
kuwapongeza wanaomua kutumia huduma hiyo nzuri.
Wateja hao watatu waliojinyakulia sh Milioni moja kila mmoja, wanaungana na
Hyasint Mbunda Songea, Phaustine Mbilinyi Dar es Salaam na Allen Bishubo Bukoba
ambao walishinda katika droo ya mwezi wa nne, ambapo Bayport Financial
Services, imeshawapatia fedha zao za ushindi.
No comments:
Post a Comment