Bw. Sam Kutessa, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. |
Na Mwandishi Maalum,
New York
Jumuiya ya Kimataifa inajiaanda
kwa mkutano maalum na wa aina yake kufanyika, ambapo nchi wanachama watakutana na
kujadiliana kwa kina kuhusu
changamoto na adhari kubwa
zitokanazo na biashara haramu na
matumizi ya dawa za kulevya.
Mapema wiki iliyopita, wajumbe wanaoziwakilisha nchi zao hapa
Umoja wa Mataifa, walikuwa na mkutano wa siku moja ambao ulikuwa ni
sehemu ya maandalizi ya mkutano huo maalum utakaofanyika mwezi Aprili 2016.
Mkutano huo wa maandalizi uliofanyika
hapa Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na
wadau mbalimbali wakiwamo mawaziri kadhaa kutoka nchi hasa za Amerika ya Kati ambako nchi nyingi zinakabiliwa na changamoto kubwa ya biashara hiyo, uliandaliwa na Bw. Sam
Kutessa, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa.
Katika majadiliano ya mkutano huo ,
ilidhihirika wazi kwamba hakuna nchi hata moja duniani
iwe tajiri au maskini ambayo haijakumbwa na
janga la biashara na matumizi ya dawa za kulevya.
“ Hakuna nchi ambayo imepona kutokana
na biashara hii yenye thamani ya
mabilioni ya dola. Licha ya juhudi kubwa
na raslimali nyingi ambazo mataifa yanatumia
kukabiliana na janga hili, lakini tatizo
linaendelea kukua” akasema Bw. Sam Kutessa wakati akifungua mkutano huo.
Naye Naibu Katibu Mkuu Bw, Jan
Eliason naye akizugumza kwenye
mkutano huo. Pamoja na mambo mengine alieleza kwamba, mitandao ya
kihalifu inazidi kustawi kutokana na biashara hiyo na kuongeza
kuwa mitandao hiyo
inaharibu mifumo imara ya
ustawi wa kijamii, pamoja na kuyumbisha
utawala wa kidemokrasia.
Kama hiyo
haitoshi Naibu Katibu Mkuu, ameongeza kuwa biashara haramu ya dawa za kulevya inatumika kama vyanzo vya
mapato kwa makundi ya wanagambo wenyenye silaha na hivyo
kuwa tisho kubwa katika mataifa ambayo yanamigogoro.
Kwa sababu hizo na nyingine nyingi
zilizobainishwa na wajumbe walioshirikia mkutano huo, wameshauri na
kupendekeza kwamba, kwa kuwa tatizo la
dawa za kulevya ni la dunia nzima, basi
utashi wa kisiasa, ushirikiano, uwazi na
ukweli utahitajika sana katika mkutano
huo maalum utakaofanyika mwakani.
Baadhi ya wachangiaji walikwenda
mbali Zaidi kwa kubainisha kuwa, katika kulikabili tatizo la dawa za kulevya
haitoshi nguvu kuelekezwa kule
zinakozalishwa dawa hizo bali nguvu hizo pia zinatakiwa kuelekezwa pia
katika nchi ambazo zina matumizi makubwa ya dawa.
Aidha
wachangiaji wengine walitaka pia
uwazi na uwajibikaji katika
udhibiti wa vyanzo vya
fedha chafu ambazo zinatumika
katika biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya. Ikiwa ni pamoja na udhibiti wa magenge ya wahalifu wanaomiliki na kuendesha biashara
hiyo.
Vile vile wazungumzaji
wengi pia walizungumzia namna gani
biashara na matumizi ya dawa za
kulevya inavyoendelea kushamiri licha ya
juhudi mbalimali za kimataifa na
kimataifa za kuikabili. Na kwamba
kuendelea kwa biashara hiyo ambayo
tayari imeshaathiri na kuendelea kuathiri maisha ya watu wengi hususani vijana, wanawake na watoto ni janga la dunia.
Wengi wamekiri bayana kwamba si rahisi sana kumaliza tatizo
na biashara haramu
na matumizi ya dawa hizo kutokana
na ukweli kwamba linawashirika na wadau
wengi na ni biashara yenye kubeba uzito mkubwa kiasi kwamba si rahisi kuimaliza
mara moja.
Wapo baadhi ya wajumbe waliogusia
kuhusu adhabu kali zikiwamo za kuuawa
kwa watu wanaokamatwa wakisafirisha au
kuuza dawa hizo, na kwamba adhabu kama za
kifo licha ya kwamba ni
ukiukwaji ya haki ya mtu kuishi lakini pia ni ukiukwaji wa haki za
binadamu na kwamba hukumu ya adhabu ya
kifo haijapunguza kasi ya biashara hiyo
au matumizi yake.
Wengine walielezea haja na umuhimu ya
kutowanyanyapaa watu ambao wameathirika
na dawa hizo au hata kuwatenga kwa kile walichosema wanachohitaji
waathirika hao ni msaada wa matibabu yatakayowawezesha kuondoka na dhahama
hiyo.
Akichangia majadiliano hayo, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,
alisema kama ilivyo kwa nchi nyingine, Tanzania nayo haijapona
na janga
la biashara na matumzi ya dawa za
kulevya.
Akasema Tanzania imekuwa njia ya kupitishia dawa hizo
kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine,
na kwamba katika usafirishaji huo, kiasi cha dawa hizo hubakia nchini na hivyo kuathiri sehemu kubwa ya jamii ya watanzania
ambao tayari wanakabiliwa na umaskini wa kila aina.
Akaongeza kuwa, tatizo la dawa za kulevya limekuwa
kikwazo katika jitihada za kuwapatia watanzania maisha yenye hadhi
kutokana na kwamba tatizo hilo linaathiri nguvu kazi inayohitajika katika ujenzi na uendeshaji wa maendeleo ya
jamii na ukuaji wa uchumi.
Kama hiyo haitoshi, Balozi Manongi
ameeleza kwamba, dawa za kulevya
zimekuwa kichocheo cha ongezeko la vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na uhalifu wa wanyamapori na
misitu, ugaidi na pia kuongeza mzigo katika huduma za afya.
“Lengo letu ni kuzuia uingiaji wa dawa za kulevya kwenye ndani ya
nchi yetu, lakini uzoefu umetuonyesha hii ni kazi kubwa na ngumu na hasa kutokana na
muingiliano baina ya mataifa ni kwa sababu hii, tunashirikiana na nchi
jirani nasi na washirika wengine katika kuboresha jitihada za
kukabiliana na changamoto hii” akasema Balozi Manongi.
Akatilia mkazo umuhimu wa
ushirikiano wa kimataifa, pamoja na mipango
mbadala inayoweza kutoa fursa
kwa jamii kufanya shughuli nyingine
badala ya kutegemea biashara ya dawa za kulevya
Mkutano wa mwakani unafanyika ikiwa
miaka kadhaa imepita tangu ulipofanyika mkutano mwaka 2008 huko Vienna, ambapo kulipitishwa Tamko
la Kisiasa na Mpango wa Utekelezaji juu ya ushirikiano wa uwiano ili kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya. Mkutano huo wa
mwakani utafanya tathmini ya tamko hilo
pamoja na masuala mengine.
No comments:
Post a Comment