Sunday, May 10, 2015

Dkt. Shein aongoza mamia ya waombolezaji kwenye Maziko ya WANA CCM Waliopata ajali jana

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akishiriki katika swala ya maiti kumswalia Bi Mwanaidi Zamir Haji miaka 28 mkaazi wa Magogoni Mjini Unguja katika msikiti wa marehemu aliyefariki kwa ajali ya gari iliyopinduka huko Mtowapwani Kaskazini jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitia udongo katika kaburi la Marehemu Bi Mwanaidi Zamir Haji miaka 28 mkaazi wa Magogoni Mjini Unguja aliyefariki kwa ajali ya gari iliyopinduka huko Mtowapwani Kaskazini jana na kuzikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu walioshiriki katika maziko ya Marehemu Bi Mwanaidi Zamir Haji miaka 28 mkaazi wa Magogoni Mjini Unguja aliyefariki kwa ajali ya gari iliyopinduka huko Mtowapwani Kaskazini jana na kuzikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na ndugu wa Marehemu Bi Mwanaidi Zamir Haji miaka 28 mkaazi wa Magogoni Mjini Unguja baada ya mazishi yaliyofanyika leo makaburi ya Mwanakwerekwe marehemu alifariki kwa ajali ya gari iliyopinduka jana huko Mtowapwani Kaskazini A Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akimfariji Salhia Sheha Khamis mkaazi wa Kwamtipura aliyelazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja jana baada ya kupata ajali ya kupinduka kwa gari iliyobeba wanaCCM wakitokea Nungwi katika shuhuli za kichama katika ajali hiyo watatu wamefariki Dunia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akimfariji Bi Mauwa Ali Khamis mkaazi wa Kwamtipura aliyelazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja jana baada ya kupata mshtuko wa ajali ya kupinduka kwa gari iliyobeba wanaCCM wakitokea Nungwi katika shuhuli za kichama katika ajali hiyo watatu wamefariki Dunia.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipokuwa akitoa maelekezo kwa watendaji wa Chama katika Hospitali ya Mnazi Mmoja jana alipoungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein kuwafariji Wanachama wa CCM waliolazwa katika baada ya kupata ajali ya kupinduka kwa gari walilopanda wakitokea Nungwi katika shuhuli za kichama katika ajali hiyo watatu wamefariki Dunia.
Baadhi ya Wananchi na wanaCCM wakibeba jeneza la Marehemu Bi Munira Abdalla Mkaazi wa Mkele Mjini Unguja aliyefariki kwa Ajali iliyotokea jana Mkokotoni Mtowapwani kwa kupinduka Waliokuwa wamepanda wanachama wa CCM wakitokea Nungwi Marehemu amezikwa leo makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi vuai Nahodha waliongana na Wananchi na wanaCCM katika maziko ya Marehemu Bi Munira Abdalla Mkaazi wa Mkele aliyefariki kwa Ajali iliyotokea jana Mkokotoni Mtowapwani kwa kupinduka Waliokuwa wamepanda wanachama wa CCM wakitokea Nungwi Marehemu amezikwa leo makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi vuai Nahodha waliongana na Wananchi na wanaCCM katika kumuombea Dua Marehemu Bi Munira Abdalla Mkaazi wa Mkele aliyefariki kwa Ajali iliyotokea jana Mkokotoni Mtowapwani kwa kupinduka Waliokuwa wamepanda wanachama wa CCM wakitokea Nungwi, Marehemu amezikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.]

No comments: