Tuesday, April 28, 2015

WANAFUNZI WA CHUO CHA UALIMU PATANDI WAZUIA BARABARA YA ARUSHA MOSHI KWA SAA MBILI

kamanda wa polisi mkoa wa Arusha
Hali ya Sintofahamu imeukumba mji wa Tengeru leo Asubuhi baada ya wanafunzi wa chuo cha ualimu Patandi Kufunga barabara kwa muda wa masaa mawili na kuacha shughuli za maendeleo kusimama kwa muda huku magari  ya abiria yanayokwenda katika mikoa ya Kilimanjaro,Tanga na Dar es salaam na mji mdogo wa usa river na maeneo mengine kupata adha hiyo.

Wanafunzi hao walizuia bara bara hiyo  wakishinikiza madai yao kusikiliza kwani wameshatoa malalamiko yao kwa uongozi wa chuo hicho bila ya kushughulikiwa kwa muda sasa wakiainisha kuwa wamekuwa wakipatiwa adhabu zisizo stahiki ikiwemo kurushwa kichura kuchapwa makofi huku kanuni za utumishi zikivunjwa na uongozi wa chuo hicho cha ualimu Patandi kilichopo wilayani Meru..

Wakizungumza kwa nyakati Tofauti na libeneke la kaskazini  blog  Mmoja wa wanafunzi  Jenny Mlay  alisema kuwa leo Asubuhi mkuu wa chuo alimkuta mwanafunzi mwenzao amelala bwenini akiumwa na kuacha taa ikiwa inawaka na ndipo alimpiga makofi na wao kwa umoja wao wakaamua kuingia barabarani ilikufikisha kilio chao cha muda mrefu.

Alisema kuwa kumekuwepo na unyanyasaji wa wanafunzi kwa kupewa adhabu zisizoendana na maadili ya vyuo ikiwemo kupiga magoti,kuruka kichura, na nyingine kama hizo ambazo ni kinyume na haki za binadamu na kanuni za chuo.

“Utakuta mtu anarukishwa kichura tena muajiriwa ambaye amekuja kuongeza daraja hapa chuoni huyu sio mwanafunzi wa darasa la kwanza hivyo tumefikisha ujumbe wetu mara nyingi kwa uongozi lakini hatupatiwi majibu ndio tukaamua kufunga barabara ilikufikisha ujumbe wetu kuwafikia walengwa”alisema Mlay

Mlay alisema kuwa kufuatia malalamiko yao kupuuzwa na tukio la Asubuhi la kupigwa kwa mwenzao wao wanautaka uongozi akiwemo mkuu wa chuo hicho kuachia ngazi kwani amekuwa ndio tatizo la migogoro hapo chuoni.

Nae Mkuu wa chuo hicho cha ualimu patandi Zaina Kabelwa akijibu hoja zilizotolewa na wanafunzi hao alisema kuwa ualimu wao unaishia Geti la chuo na wakishaingia chuoni hapo wanakuwa kama wanafunzi wengine wa vyuo na wanatakiwa kufuata kanuni na sheria za chuo.

Kabelwa alisema kuwa matumizi ya vifaa vya chuo yakiwemo majengo na usafi wa mazingira ni kwa kila mwanafunzi bila ya kujali huyu ni mwajiriwa au la wote wananafasi sawa kwa mujibu wa kanuni za chuo hicho

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wale wote wenye kuvunja sheria kufuata mikondo ya sheria ikiwemo kufuata mamlaka husika ili malalamiko yao yaeweze kupatiwa ufumbuzi na sio kuchukuwa sheria mkononi.

Kamanda Sabas alisema kuwa wanafunzi hao walisimamisha msafara wa magari kwa saa mbili hadi walipotawanya na askari wake wa kituo cha usa river baada ya kukaidi amri ya mkuu wa chuo hicho aliewataka warudi chuoni hapo iliwaweze kukaa na kujadili mamalamiko yao.

"Nawasihi wote wanajichukulia sheria mikononi kufuata sheria bila shuruti kwani jeshi hilo lipo macho kwa wote wanaovunja sheria kwani sheria itachukuwa mkondo wake bila ya kumuonea mtu"alisisitiza Sabas

No comments: