Na Mwandishi wetu
Serikali ya Uingereza imebuni mbinu ya kuwasiadia vijana wa
kitanzania kukabiliana na vikwazo katika soko la ajira na pia kuwapa maarifa ya
kujiajiri wenyewe .
Vikwazo vinavyowakabili vinaja
katika soko la ajira ni kutokuwa na maarifa ya kupata kazi maarifa a na tabia ambazo zitamwezesha
mfanyakazi kuwa karibu na wafanyakazi
wenzake , kutoa maamuzi magumu , kutatua matatizo , kuweka heshima na mwisho
kuwa mwakilishi wa taasisi.
Kwa kutambua changamoto zinazowakabili vijana serikali ya
Uingereza imetuma walimu wa kujitolea kutoka taasisi ya Resstless Development organization(ICS) kwa
ajili ya kuwafundisha namna ya kupata ajira endelevu .
Wakizungumza katika mafunzo waliyoyatoa katika chuo cha
Kilimanjaro Institute of Technology and Management (KITM) walimu hao wa
kujitolea wamesema wanawafundisha vijana namna ya kuandika maelezo ya mtu
binafsi kuhusu elimu , ujuzi na kujiajiri wenyewe .
Kiongozi wa
walimu wa kujitolea (ICS ) Gemma Bunn ameliambia gazeti hili kwamba sababu ya wao kuwepo nchini ni kwa kutambua
kuwa Tanzania asilimia hamsini ya vijana hawawezi kupata ajira na wengi
wanakwamishwa kutokana na vigezo hivyo .
‘’Tunatoa mafunzo kuhusu maarifa ya kupata ajira ikiwemo
namna ya kuandika maelezo ya mtu binafsi
kuhusu elimu , ujuzi , kujiajiri mwenyewe na namna ya kujiweka wakati wa
kufanya usaili , kujiajiri mwenyewe pamoja na namna ya kuanzisha biashara
pamoja na kutengeneza bajeti ‘’alisema Gemma .
Naye Wendy Morrissey , mwalimu wa kujitolea kutoka taasisi
hiyo amesema CV ni nyaraka muhimu kwa
wanafunzi na mtu yoyote kuiandika . Ni nyaraka itakayokusaidia kupata ajira .
Amesema mambo ya kuyazingatia kuyaweka katika nyaraka hiyo ni
pamoja ni pamoja na ujuzi na maarifa kwa nafasi ya kazi unayoombea .
CV haitakiwi iwe ndefu zaidi ya ukurasa mmoja kwasababu
mwajiri anachukua muda wa sekunde nane kuiangalia . Kwa hiyo unatakiwa kumvutia
mwajiri kwa kutumia muda mfupi kuisoma
Wakati ukiandika nyaraka hiyo unatakiwa uandike kwa weledi na
usiandike kwa kutumia maneno ya mtaani .
Mambo mengine ambayo hayatakiwi kuandikwa ni sarufi ambazo
sio sahihi kwenye maelezo hayo . Pitia
kwanza maeezo yote pamoja na sarufi kabla ya kuikabidhi .
Jambo lingine ambalo ni muhimu ni kuandika maelezo kwa
matakwa yako ambayo hayaendani na kazi unayoomba .
Jonathan Aqulina ,
mwalimu wa kujitolea anayefundisha namna ya kujiajiri mwenywe alisema njia
rahisi ya kukabiliana na changamoto ya mikopo ni kujiunga katika vikundi .
‘’ Inaweza kuwa ni kikundi cha marafiki au familia . Kikundi
kinapokuwa kikubwa hatari inakuwa ndogo . Hiyo ndio njia rahisi ya kupata
mikopo ‘’ alisema Aqulina.
Amesema njia rahisi ya kujiajiri mwenywe ni kulifahamu soko
lako . Lazima umjue unaye muuzia bidhaa zako . Lazima ufahamu wanahitaji nini
. Kama hautahamu hutaweza kuuza chechote
. Unatakiwa kufanya utafiti wa soko na
kufahamu washindani ni akina nani na bei wanazouza bidhaa .
Jambo lingine ni kutangaza bidhaa zako ili watu wafahamu
bidhaa unazouza . Na pia ushauri wangu ni kwamba hakikisha kwamba
gharama zako ziko chini kuliko faida unayopata . Kama gharama zitakuwa juu
zaidi ya faida hutaweza kutengeneza pesa biashara yako itakufa .
Na pia siku zote tathmini biashara yako . Tathimini uimara na
udhaifu na pia ufahamu kinachoendelea kwenye soko .
Nao
Philip Luke , mratibu wa mafunzo wa chuo hicho cha KITM na mwezeshaji wa
mafunzo Dani Kishimbo walisema mafunzo yamekuwa na umuhimu mkubwa kwa
wafanyakazi na wanafunzi kwa sababu wamepata maarifa mapya namna ya kuandika CV
na kuanzisha biashara zao.
‘’ Tumepata maarifa mapya ya namna
ya kuanzisha biashara zetu wenywe na pia namna ya kujiweka na kujibu maswali
wakati wa usaili . Tunafahamu namna ya kujiweka kujibu maswali inavyotakiwa ‘’
alisema Philip Luke.
Dani Kishimbo, mratibu wa mafunzo
alisema mafunzo yamekuwa na umuhimu mkubwa na maarifa waliyoyapata wanafunzi
watayatumia kuomba mazoezi kwa vitendo au ajira.
Mwishoni
mwa mafunzo hayo washiriki walipewa vyeti na mmoja wao Abdala Kipinga
aliwashukuru walimu wa mafunzo na kusema amejifunza mengi ikiwemo namna ya kuandaa
mikutano , CV pamoja na kuanzisha biashara.
Restless Development Tanzania (ICS) mtazamo wao ni kusaidia
vijana kuchukua jukumu la kuwa viongozi kwa kutatua changamoto zinazokabili
nchi zao na dunia kwa ujumla.
Taasisi hiyo inatekeleza mtazamo huo kwa kuwajengea uwezo
vijana kimaarifa , kimsukumo na raslimali kuchukua nafasi za kazi ambazo
zinachangia sio tu katika kipato cha
familia bali pia uchumi wa jamii pamoja nan chi zao.
Mafunzo hayo yamekuja huku kukiwa
na ripoti ya baraza la vyuo vikuu vya
Afrika ya mashariki ikisema karibia nusu ya wahitimu wanaozalishwa na vyuo vya
nchi hizo hawana uzoefu katika soko la ajira.Ripoti hiyo inasema wakati maelfu ya vijana wanamaliza kila mwaka
, sifa walizokuwa nazo vijana wengi haziwezi kuwasaidia kuwapa kazi na waajiri wanawaacha
wanawachukua wenye ujuzi jambo linaloleta changamoto la ukosefu wa ajira katika
ukanda huu.
Kwa mujubu wa Katibu wa baraza hilo
, Professor Mayunga Nkunya a, waajiri
wanasema wahitimu wengi wa vyuo wanakosa kujiamini , hawawezi kujieleza vizuri
na hawana ujuzi wa kitaalam unaotakiwa katika kazi wanazotafuta .
No comments:
Post a Comment