Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga katika kikao na baadhi ya vijana hao
KIU
ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa kukomboa jimbo la Iringa Mjini
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu inazidi kuongezeka, baada ya umoja wake
wa vijana (UVCCM Manispaa ya Iringa) kuahidi kuongeza nguvu ili kuufanikisha mkakati
huo.
CCM
ililipoteza jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa Mchungaji Msigwa wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayekaribia kumaliza muda wake.
Katika
kikao kilichozikutanisha sekretarieti za umoja huo kutoka katika kata zote 18
za manispaa ya Iringa, Mwenyekiti wa UVCCM wa manispaa hiyo, Kaunda Mwaipyana
alisema; “katika kukisaidia chama kushinda uchaguzi huo, kauli mbiu yetu ni
chama kwanza mtu baadaye.”
“Tutapita
katika matawi na kata zetu zote, tutafanya vikao, mikutano ya hadhara na
kuwakumbusha vijana wajibu wa kukipigania chama chao ili mkakati wa kulikomboa
jimbo ufanikiwe,” alisema.
Katibu
wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga aliwaongezea hamasa vijana hao kwa
kuwapa seti 60 za jezi na mipira watakazozitumia kuwahamasisha vijana hao kupitia mchezo
wa soka.
“CCM
ina vijana wengi sana katika jimbo hili, mnahitaji kukutana na kujipanga,
tumieni mbinu zote za kukutana, iwe
vikao, mikutano na hata michezo na ndio maana nimewapa msaada huu,” alisema.
Aliwataka
vijana wa chama hicho kujitokeza kwenye vikao visivyo rasmi vya maeneo yao wanayoishi
na kuitetea CCM kwasababu majibu ya hoja nyingi za wapinzani wanayo.
Akiwakabidhi
jezi hizo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM Mkoa wa Iringa, Ephraim Mhekwa
alisema CCM inayo nafasi ya kulikomboa
jimbo hilo kama itajipanga vizuri.
“Pamoja
na kwamba wapinzani walipata viti 65 katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa
mwaka jana, wasisahau kwamba CCM ilipata viti 126; hesabu hiyo inadhihirisha
chama chetu kinaungwa mkono mara mbili yao,” alisema.
Aliwataka
vijana hao kuweka bendera za chama hicho kila panapostahili katika mitaa yote
na akawasihi wasikubali kutumika na kukigawa chama kwa maslai ya wachache.
Naye
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mahamudu Madenge alisema CCM itaendelea
kuwepo hata kama watu wasiotaka kufuata utaratibu wataondoka.
“Wameondoka
wengi, wengine hii leo ni viongozi wa vyama vikubwa vya siasa. Pamoja na
kuondoka kwao CCM ipo pale pale na inaendelea kupata wanachama,” alisema
No comments:
Post a Comment