Saturday, April 11, 2015

UN. TAASISI IMARA KATIKA UTATUZI WA MIGOGORO

Kutoka kushoto ni Reginald Munisi, Mwenyekiti, United Nations Association of Tazania, Mr. Alvaro Rodriguez, Mratibu Mkazi, Umoja wa Mataifa Tanzania, Balozi Dr. Agustine Mahiga, Balozi Mstaafu wa Tazania Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wakiwa katika Maadhimisho ya Miaka 50 Taasisi ya Umoja wa Matifa (UNA) pamoja na maadhimisho ya miaka 70 ya umoja wa Mataifa (UN) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Reginald Munisi, Mwenyekiti wa UNA Tanzania akitoa maneno ya ufunguzi katika mkutano mkuu wa UNA Tanzania.
Washiriki katika mkutano mkuu wa UNA Tanzania.
 Washiriki katika picha ya pamoja.
Mr. Alvaro Rodriguez, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa, na Mgeni Rasmi, Tanzania akifungua mkutano mkuu wa UNA Tanzania.
 Balozi Dr. Agustine Mahiga akizungumza na waandiahi wa habari.
Reginald Munisi, Mwenyekiti wa UNA Tanzania, akizungumza na waandishi wa habari.
Mr. Alvaro Rodriguez, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mgeni Rasmi akizindua kipengele cha "Ask the UN RC" katika wavuti ya UNA Tanzania - www.una.or.tz
---
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
UMOJA wa Mataifa (UN) ni taasisi imara katika kusimamia maendeleo ya wananchi pamoja na kutatua migogoro mbalimbali ya nchi ya vita kwa nchi wanachama wa umoja huo.

Hayo ameyasema leo Balozi Agustine Mahija wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 Taasisi ya Umoja wa Matifa (UNA) pamoja na maadhimisho ya miaka 70 ya umoja wa Mataifa (UN) iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mahija alisema Umoja wa Mataifa (UN) umekuwa mstari wa mbele katika kutatua migogoro ikiwa ni kufanya wananchi waishi maisha ya amani kwa kuanzisha baraza la usalama wa Umoja wa Matiafa ambalo limekuwa likishughulikia migogoro mbalimbali.

Amesema UN imeweza kuweka malengo mbalimbali ya kiuchumi kwa nchi 195 zilizo katika umoja huo katika kuweza kuondokana na umasikini kwa kubuni miradi ambayo yameleta tija kwa mataifa mbalimbali.

Naye Mwenyekiti waTaasisi ya Umoja wa Mataifa UNA Tanzania. Reginald Munisi amesema katika kuelekea uchaguzi vyombo vinavyoshughulikia ulinzi visijihusishe na siasa ili wananchi waweze bkupiga kura kwa amani.
Munisi amesema vyombo vya ulinzi vikijihusisha na siasa wananchi watashindwa kushirika katika uchaguzi wa kuchagua viongozi wao ambao ndio wanawategemea katika maendeleo ya nchi.

Aidha alisema UNA Tanzania itatoa eli kwa vyombo vya ulinzi katika kuelekea uchaguzi ikiwa ni lengo la kuwafanya wananchi waweze kupiga kura kwa amini na kuweza kuwapata viongozi wao.

No comments: