Wednesday, April 22, 2015

NHC NA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM ZATILIANA SAINI MKATABA WA MANUNUZI YA ENEO LA OFISI JENGO LA MOROCCO SQUARE

hc1Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. (Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii) hc2Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo. hc3Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo. hc4Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudua NHC na DSE wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. hc5Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudua NHC na DSE wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea
hc6Watendaji wa NHC na DSE wakibadilishana mawazo wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. hc7 
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa Tuntufye Mwambusi na Meneja wa Uendelezaji Biashara wa NHC, Willia Genya wakibadiliashana mawazo katika hafla hiyo. hc8Mchechu akibadilishana mawazo na watendaji wa DSE wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. hc9 Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa, David Misonge Shambwe akiwakaribisha wageni katika hafla hiyo.
hc10 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa wakifuatilia jambo katika hafla hiyo ya utiaji saini. hc11 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza katika hafla hiyo. hc12 Watendaji wa DSE wakibadilishana mawazo wakati wa utiaji saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. hc13Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa akizungumza katika hafla hiyo. hc14 hc15 Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo. hc16Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo. hc17Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo.

..............................................................................................
Kwa mara nyingine Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Jumatano, 22 Aprili 2015 tumefikia makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.

Mkataba unaosainiwa leo baina ya pande hizi mbili utagharimu kiasi cha dola za kimarekani 1,800,000 (bila VAT) kiasi cha shilingi za kitanzania 3.366 bilioni malipo yatakayofanyika kwa awamu nne katika kipindi cha miaka mitatu.

Mradi wa kipee na wa kwanza Tanzania wa Morocco Square wenye ukubwa wa mita za mraba 105,000 unaotarajia kukamilika ndani ya kipindi cha Miaka Mitatu, ni unaotekelezwa kwa kutumia mfumo mpya kabisa wa ujenzi wa (Design and Building). 

Umebuniwa kwa makini kabisa kulingana na mahitaji ya majengo ya sasa na ya baadae na vile vile unajengwa na mkandarasi wa kitanzania. Sambamba na haya, utekelezaji wa mradi huu umezingatia uwepo wa huduma zote muhimu sambamba na miundo mbadala yakujitosheleza.

Sifa nyingine za ziada za mradi huu ni pamoja na uwepo wa majengo pacha mawili makubwa ya ghorofa, moja likiwa na ghorofa 17 na 19.
Jengo hili limebiniwa likiwa na mahitaji muhimu yakiwa sehemu moja (Mixed Development) ikiwepo maeneo maalum ya Maofisi ya kimataifa, Sehemu ya hotel kwa ajili ya wafanyabiashara, nyumba za makazi (Residential apartment), maeneo ya maegesho ya magari, huduma za kibenki, pamoja na sehemu ya huduma za masoko ( shopping mall).

Mradi huu unatarajiwa kuboresha mazingira ya biashara katika jiji la Dar Es Salaam vile vile ukizingatia mahitaji ya ukuaji na upanukaji wa jiji la Dar Es Salaam. Jengo la Morocco Square lipo karibu kabisa na kitovu cha jiji likiwa limezungukwa na maofisi na makazi muhimu kabisa. 

Eneo la Morocco Square linatoa fursa kwa mkazi kuweza kufika kwa karibu kabisa sehemu mbalimbali muhimu za jiji la Dar Es Salaam kama vile Mikocheni, Oystebay, Masaki,Mikocheni, katikati ya jiji la Dar Es Salaam,Kinondoni, Kawe na Mlimani City.

Makubaliano haya kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na Soko la Hisa la Dar Es Salaam ( Dar Es Salaam Stock Exchange (DSE) yanatoa fursa za kipekee kwa (DSE) pamoja na mawakala wake wa soko la mitaji na tunapenda kulipongeza soko la hisa kwa kuwahi kabla ya mashirika yote ili kuweza kupata fursa ya kipekee katika jengo hili la kisasa kabisa na la kwanza Tanzania.

Tunapenda kutoa wito kwa Mashirika ya kimataifa, yakati ( Medium Enterprises) kuchanmkia fursa hii ya kipekee ususani ukizingatia kwamba miji yote Duniani soko la hisa huwa chachu ya maendeleo ya wadau wote wanaofanya biashara kuzunguka eneo husika.

Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo maalumu linalowezesha kutua helikopta, eneo kubwa la maegesho ya magari ya ziada, Ofisi ya Meneja wa Usimamizi wa Milki, eneo maalumu la kukusanyia taka, nyumba ya mlinzi, umeme wa uhakika, miundombinu ya zimamoto, mfumo wa vipoza joto, kebo za mtandao wa mawasiliano, lifti, ulinzi wa saa 24 wa Kamera za CCTV na kisima kirefu cha maji chenye mfumo wa kusukuma maji ya kutosha.

Tunawahamasisha wenye kuhitaji maeneo ya ofisi, biashara na nyumba za kuishi wafanye mawasiliano na Makao Makuu ya Shirika na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi.

Ukiwa mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayetamani kununua ofisi au kuwekeza katika mradi huu, tafadhali wasiliana na Kitengo cha Mauzo, Makao Makuu ya NHC au piga simu namba 0754 444 333; baruapepe: sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti ya Shirika www.nhctz.com kwa maelezo zaidi.

No comments: