Sunday, April 19, 2015

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA AZINDUA IBADA YA MAKUNDI MAALUMU KATIKA KANISA LA KILUTHERI USHARIKA WA KIGOGO JIJINI DAR

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akizungumza na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kigogo na vijana waliopo katika kundi maalumu kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya wakati akizindua ibada makundi maalumu iliyoanzishwa katika kanisa hilo Dar es Salaam jana.
 Msaidizi mstaafu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), George Fute (kulia), akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika nafasi hiyo.
 Mchungaji wa kanisa hilo usharika wa Kigogo ambaye ndio muasisi wa ibada hiyo ya makundi maalumu,  Richard Ananja akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Msaidizi mstaafu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), George Fute
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiteta na Thomas Alfred kijana ambaye yupo katika kundi maalumu la waathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya wakati wa uzinduzi huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda(kulia), akiimba sanjari na wanakwaya ya usharika huo.
 Vijana waliopo katika kundi maalumu wakiwa kwenye uzinduzi huo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliyekaa.
 Vijana waliokuwa katika kundi maalumu wakiwa katika uzinduzi wa ibada hiyo pamoja na waumini wengine.
 DC Makonda akisalimiana na waumini wa kanisa hilo.
 Mwenyekiti wa kundi hilo, Paul Njoole akitoa neno la shukuru kwa uongozi wa kanisa hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliokuwa katika kundi hilo pamoja na viongozi wa kanisa hilo.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, Paul Makonda ameahidi kushirikiana na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Kigogo kuhakikisha anapambana wa waingiza na wauzaji wa dawa za kulevya katika wilaya hiyo.

Makonda alitoa ahadi hiyo Dar es Salaam juzi katika uzinduzi wa ibada ya makundi maalumu hasa kwa wale walioathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ambapo alikuwa mgeni rasmi.

" Kwa upande wetu wa Serikali kazi yetu ya kwanza ni kushirikiana na watu wote wenye nia njema kutoa elimu juu ya dawa za kulevya kama siyo kulipunguza jambo hilo basi kulimaliza kabisa katika wilaya yetu" alisema Makonda.

Alisema wakuu wawilaya wote wapya tayari wamepata mafunzo ya kushughulikia suala hilo hivyo kila anayejishughulisha na dawa hizo atafikiwa na kufikishwa kwenye mkono wa dola.

Makonda alitumia nafasi hiyo kuupongeza uongozi wa kanisa hilo kwa kuanzisha huduma ya kuwahudumia vijana hao walioathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuingia mtaani bila ya kuona haya na kuzungumza na kuwa nao.

Katika hatua nyingine Makonda aliwaambia waumini wa kanisa hilo kuwa waachane na viongozi wa dini wanaofanyakazi ya kutoa matamko mbalimbali badala ya kufanyakazi ya kuisaidia serikali katika shughuli za maendeleo kwani matamko siyo kazi yao.

"Kazi ya kanisa siyo kunung'unika kuwa nchi haina huduma mbalimbali bali ni kushirikiana na waumini kulisaidia taifa katika shughuli za maendeleo" alisema Makonda.

Mchungaji wa usharika huo ambaye ameanzisha huduma hiyo Richard Ananja aliitaka jamii kujitokeza kusaidia kundi hilo lenye mahitaji maalumu badala ya kuwatenga na kuwa kwa kufanya hivyo ni kutimiza agizo la mungu.

Alisema kwa pamoja tukishirikiana jambo hilo linaeweza kuisha kwa watumiaji na kuwaambia wanaouza dawa hizo kuacha kufanya hivyo kwani wanafahamika ni ndugu na jamaa zetu na tunaishi nao.

Mchunguji Ananja alisema kuwa usharika wake unatoa huduma hiyo kwa vijana zaidi ya 100 ambao walikuwa wakitumia dawa hizo ingawa changamoto kubwa waliyonayo ni ofisi na mahitaji ya chakula.

Mwenyekiti wa vijana hao Paul Njoole aliushukuru uongozi wa kanisa hilo kwa msaada unaowapa na akawaomba wadau wengine wajitokeze ili wawezeshwe kwani wengi wao wanaujuzi mbalimbali ambapo wataweza kujitegemea na kurejea katika maisha waliyokuwa wakiishi hapo awali. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com)

No comments: