Shirika la fedha la kimataifa (IMF) hujishughulisha na kutoa ushauri wa kisera kwa nchi wanachama na kutoa mikopo na misaada ya kifedha. Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum aliyaeleza hayo mjini hapa.
Akishiriki kikao cha kundi la Africa(African Group one Constituency). Kundi hili hukutana kila kunapokuwa na mikutano ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia kwa lengo la kuwezesha nchi za Afrika kuwa na sauti moja na kujua hatua ambazo Nchi za Afrika zimefikia kuhusiana na Taasisi zake za kifedha.
Mhe. Mkuya alichangia mada mbalimbali zilizohusu kundi hilo akilenga zaidi maendeleo na muelekeo mzuri wa mafanikio ya kifedha katika nchi ya Tanzania.
Waziri wa Fedha wa Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuya ni Gavana katika mkutano huu akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni Gavana msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia (WB), aidha Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Katika Mkutano huu Magavana hawa ndio wenye maamuzi ya juu na nguvu kubwa ya kuweza kuyashawishi mashirika ya kifedha kuhusu nini kifanyike. Mkutano huu uliofanyika leo, umeangalia uhalisia na vigezo vinavyotolewa na Shirika la Fedha la kimataifa katika kuimarisha taasisi za kifedha katika nchi wanachama Afrika.
Katika mkutano huu, mambo muhimu yaliyojadiliwani pamoja na maendeleo katika kundi hilo na mabadiliko ya maboresho katika Benki ya Dunia. Wakijadiliana katika mkutano huo wajumbe hao wameshauri Shirika la fedha la kimataifa pamoja na taratibu zake, liangalie namna ya kulegeza masharti ya mikopo ili nchi wanachama ziweze kufanya mabadiliko ya kifedha kwa urahisi.
Mikutano hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. na nchi wanachama wanaendelea kufika kwa wingi.
Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia kwa karibu mkutano huu. (African Group one Constituency
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akishiriki katika mkutano huu wa kundi la Afrika. (African Group one Constituency)
Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia kwa karibu mkutano huu. (African Group one Constituency)
Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu akifuatilia kwa makini mkutano wa kundi la Afrika unavyoendelea. (African Group one Constituency)
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akifuatilia kwa karibu majadiliano ya mkutano huu wa kundi laAfrika. (African Group one Constituency).
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akichangia Mada katika mkutano huu wa kundi laAfrika. (African Group one Constituency).
Imetolewa na Msemaji :Wizara ya fedha
Ingiahedi C.Mduma
Washington DC
15/04/2015.
No comments:
Post a Comment