Monday, April 13, 2015

MFUKO WA GEPF WAFANYA MKUTANO NA WADAU ARUSHA WAJADILI MASWALA MBALIMBALI YA MFUKO HUO

SAM_1775
MKUU  wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda akiwa anafungua mkutano ulioandaliwa na mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF kwa wadau wake jijini Arusha uliolenga kujadili maswala mbalimbali ya mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko katika mfuko huo.(Habari Picha na Pamela Mollel wa http://jamiiblog.co.tz/)
SAM_1760 
Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina akizungumza katika mkutano na wadau kutoka sekta mbalimbali uliofanyika jijini Arusha uliolenga kujadili maswala mbalimbali ya mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko katika mfuko huo.
SAM_1759
MKUU  wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda akiwa anasoma kipeperushi chenye maelezo kuhusu mfuko wa GEPF,kushoto Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina,kulia ni meneja kanda ya kaskazini Dennis Kaitwa
SAM_1765
Kushoto Mwalimu Jonuis Lowassa kutoka idara ya utumishi wa walimu(KTSD)wilaya ya Mounduli na Longido SAM_1779
Afisa masoko GEPF Clement Oning'o ambaye alikuwa Mc wa shughuli hiyo akitoa utaratibu katika mkutano huo
SAM_1769
Afisa muajiri Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Siraji Msophe akifurahia jambo katika mkutano huo
SAM_1770
MKUU  wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda wakiwa wanateta jambo na Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina
SAM_1761
Wadau wakiwa katika mkutano huo
SAM_1762
Kushoto Afisa rasilimali watu na utawala Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Isaial Bayege akiwa ananukuu baadhi ya mambo katika mkutano huo ulioandaliwa na mfuko wa GEPF jijini Arusha
SAM_1763
Kulia ni Afisa Rasilimali watu katika chuo cha Nelson Mandela Bi.Honorina Mashingia
SAM_1783
Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina akizungumza na waandishi wa habari kutoka  vyombo mbalimbali kuhusu mfuko wa GEPF jijini Arusha
SAM_1785
Meneja kanda ya kaskazini kutoka mfuko wa GEPF Dennis Kaitwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha
SAM_1780
Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika picha ya Pamoja na mgeni Rasmi MKUU  wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda
MKUU wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda ameitaka mifuko ya jamii kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi kujiunga na mifuko hiyo ili kuweka akiba ambayo itasawasaidia kwa maisha yao ya baadaye.
Aliyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa wadau kutoka sekta mbalimbali uliofanyika mjini hapa uliolenga kujadili maswala mbalimbali ya mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) sambamba na mabadiliko katika mfuko huo
.
Alisema kuwa, mifuko hiyo ina manufaa makubwa sana kwa jamii hususan kipindi cha kustaafu ambacho huwa ni kipindi kigumu sana kwa asilimia kubwa ya wastaafu ambapo wengi wao mifuko hiyo huwasaidia sana kuondokana na maisha magumu yanayowakabili.

Ntibenda alisema kuwa, kuna idadi kubwa sana ya wastaafu ambao wangependa kujiunga na mifuko hiyo ila kinachowawia ugumu ni kutopata elimu ya kutosha juu ya kujiunga na mifuko hiyo ambayo ina manufaa makubwa sana kwao.

 Meneja masoko wa mfuko wa GEPF Aloyce Ntukamazina alisema kuwa ,mfuko huo umeanza kutoa elimu nchi nzima juu ya mabadiliko ya mfuko huo ambapo wamezindua mafao mapya manne ambayo ni fao la elimu,uzazi,fao la kuanza maisha ,na fao la kujikimu ambapo mafao hayo yote ni yataanza kutumika katika mfuko huo hivi sasa.

Aloyce amesema kuwa,mfuko huo wamekuwa wakijitahidi sana na kukabiliana na changamoto ya wajiri kutofikisha mafao ya wafanyakazi kwenye mifuko kwa wakati ambapo mfuko huo wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha makato hayo yanafika kwa wakati na muda ulipangwa .

Aidha washiriki wa mkutano huo, wakizungumza kwa nyakati tofauti waliutaka usimamizi wa mifuko hiyo kuongeza mifuko zaidi ili wananchi wawe katika hali nzuri ya kiuchumi kwa kutumia mifuko mbalimbali na kuondokana na kusongamana kwenye mifuko michache iliyopo .

Meneja wa mfuko huo kanda ya kaskazini ,Denis Kaitwa amesema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya kutoa elimu kutokana na asilimia kubwa ya wananchi kuwa wagumu kujiunga na mifuko hiyo ambayo ina manufaa makubwa kwa maisha yao.

Kaitwa alisema kuwa,kupitia mkutano huo utawawezesha wadau hao kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi wao na hatimaye kuweza kutambua umuhimu wa kujiunga na mfuko huo wa GEPF ambao una manufaa makubwa kwa jamii.

No comments: