mbunge wa jimbo la ludewa Deo Filikunjombe akishiriki ibada ya pasaka na waumini wa kanisa la RC MAVANGA |
MBUNGE WA LUDEWA DEO FILIKUNJOMBE AKITOA SALAM ZA PASAKA KWA WAUMINI WA KANISA LA RC MAVANGA |
PAROKO WA MAVANGA AKIMKABIDHI MBUNGE FILIKUNJMBE ZAWADI YA KUKU BAADA YA MBUNGE HUYO KUTOA ZAWADI MBALI MBALI KATIKA MAKANISA YA LUDEWA ZIKIWEMO BATI 300 NA VITI |
WAUMINI WA MAVANGA WAKIMKABIDHI MBUNGE FILIKUNJOMBE KUSHOTO NDIZI |
MBUNGE WA LUDEWA DEO FILIKUNJ0MBE KATIKATI AKIWAELEKEZA JAMBO WAUMINI JAMBO |
WAUMINI MAVANGA WAKIMPONGEZA MBUNGE FILIKUNJOMBE KWA MISAADA YAKE |
MZEE WA KANISA LA KKKT LUDEWA MJINI AKIWA AMEBEBA KINANDA KILICHOTOLEWA NA MBUNGE DEO FILIKUNJOMBE |
VIONGOZI WA KKKT LUDEWA MJINI WAKIONYESHA VIFAA VYA MSAADA TOKA KWA MBUNGE |
WAUMINI KKKT WAKISHIRIKI UBATIZO |
DIWANI WA KATA YA MLANGALI FARAJA MLELWA AKISHIRIKI KUBATIZA MTOTO WAKE |
WAUMINI KKKT LUDEWA MJINI WAKIWA KATIKA IBADA YA PASAKA |
MBUNGE wa
Ludewa Deo
Filikunjombe aipongeza tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) Kwa kusogeza
mbele zoezi la upigaji kura za maoni kwa katiba inayopendekezwa na
kuwa hatua iliyofikiwa katika mchakato huo ni kubwa na kumbukumbu
kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete anapoondoka madakarani na urithi kwa Rais
ajaye kuendeleza mchakato huo.
Filikunjombe alitoa pongezi hizo wakati akitoa salamu zake za pasaka jana kwa waumini wa madhehebu mbali mbali ya Kikristo
katika wilaya ya
Ludewa salam zilizoambatana na
msaada wa viti ,bati ,vinada na saruji katika
makanisa hayo kama moja ya utekelezaji wa ahadi
zake kwa madhehebu hayo kama ambavyo walivyomuomba .
Alisema
kuwa hatua ya tume ya taifa ya uchaguzi kuongeza muda katika zoezi
hilo la kura za maoni kwa katiba inayopendekezwa mbali
yakuwapunguzia majukumu watanzania ya kufanya mambo mengi kwa wakati
mmoja bado kusogezwa huko mbele kutawafanya watanzania hasa wananchi
wake wa ludewa kuendelea na shughuli nyingine za uzalishaji mali.
'hakuna
uharaka wa kuharakisha zoezi la upigaji kura za maoni katika
katiba inayopendekezwa kwani hadi sasa hatua iliyofikiwa ni nzuri na
kumbukumbu kubwa kwa rais Jakaya kikwete anapomaliza muda wake kuwa
amefanya jambo hilo kubwa hadi lilipoishia na Rais ajaye ataanzia
alipoishia kikwete kwa kukamilisha katiba hiyo kuliko kukimbizana
kama ilivyopangwa awali kabla ya tume kusogeza mbele zoezi hilo kwa
muda usiofahamika'
pia
mbunge huyo aliwataka vijana kuwa wazalendo na nchi yao badala ya
kukubali kutumika na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi na kuwa
hatari ya vijana kutumika ni mwanzo wa nchi kuja kuingia katika
machafuko kama zilivyonchi nyingine ambazo kila uchwao ni machafuko na
chimbuko ni vijana wao kukosa uzalendo .
Hata
hivyo alisema kuwa wakati Taifa likijiandaa kuelekea katika uchaguzi
mkuu mwezi octoba mwaka huu kuna matukio makubwa ya kitaifa
yanayoendelea likiwemo la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura na kuwa ni kipimo kwa watanzania hasa vijana kuanza
kuonyesha uzalendo kwa kuwa waaminifu katika zoezi hilo badala ya
kutumiwa na baadhi ya watu wanaotaka uongozi kwa kupitia njia za panya
kwa maana ya kuwaandaa vikundi vya vijana kujiandikisha zaidi ya
mara moja katika vituo tofauti jambo ambalo ni hatari katika nchi na
kufanya hivyo ni kosa la jinai kisheria.
Huku
akiwaonya vijana kuepuka kufanya udanganyifu wa kujiandikisha mara
mbili katika daftari la kudumu la wapiga kura zoezi linaloendelea na
kuwa hadi sasa kata ya mlangali ludewa kuna kijana mmoja ambae
anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kujiandikisha zaidi ya mara moja
Filikunjombe amewataka waumini
wa dini ya kikristo
wilayani Ludewani mkoani Njombe kusherekea sikukuu ya
kufufuka kwa Yesu kristo kwa
kuendelea kuliombea Taifa
kuondokanana mabalaa mbali mbali
kwa mwaka huu
tunapoelekea kuingia katika uchaguzi
mkuu Octoba
Makanisa
hayo yalitoa kauli hiyo baada ya kusoma wakara wa amani wa
salam za Pasaka uliosambazwa katika makanisa yote na mbunge wa
jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe .
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Tafuteni Mwasonya wakati akitoa
salam za pasaka na
kumshukuru mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe
kwa msaada wa viti 100 vya
Plastiki na kinanda kanisani hapo .
Alisema kuwa kwa upande
wake hajapata kukutana ana
kwa ana na mbunge
Filikunjombe toka alipochangulia ila amekuwa
akukutana na shughuli mbali
mbali za kimaendeleo ambazo
zimefanywa na mbunge huyo na
kushuhudia utendaji kazi
wake mkubwa katika jimbo
hilo.
Hivyo alisema wana
nchi wa Ludewa wana
kila sababu ya kujivunia
kwa kuwa na mbunge kama huyo na
kama ingekuwa inaruhusiwa ndani ya kanisa kuweka picha
ya kiongozi wa wananchi basi angeweka bango
maalum ambalo limetolewa na mbunge Filikunjombe la kuwakumbusha
wananchi wa Ludewa
orodha ya wabunge waliopata kuongoza
jimbo hilo hadi mwaka huu 2015 .
“ Kwa utaratibu wetu
wa kanisa la Kirutheri ndani ya kanisa tunaweka
picha ya Yesu Kristo
pekee hata picha ya
askofu wetu hatuweki
ila kama ingekuwa
inaruhusiwa kuweka picha
za zaidi kanisani basi
tungeweka picha ya orodha ya
wabunge wetu lakini
haturuhusiwi kufanya hivyo ……lakini orodha
hiyo ya wabunge mheshimiwa
Filikunjombe ametuandalia na kila mmoja atapewa na ruksa kwenda
kuweka nyumbani kwake “ alisema
mchungaji huyo.
Hata hivyo alisema sherehe ya kuviombea
vitu hivyo vilivyotolewa na mbunge Filikunjombe na kumwombea mbunge
huyo ili azidi kupata baraka
zaidi ya kuongoza Ludewa wanapanga kuifanya
wakati wowote baada ya
sikukuu za Pasaka na kuwa siku
hiyo watamwalika na mbunge ili
waweze kumbariki pia.
Pia mchungaji
huyo aliwataka waumini
wa kanisa hilo
kujiepusha na ushiriki wa vurugu
zisizo na msingi katika
taifa letu hasa
wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu
na badala yake
kujikita zaidi katika maombi
kwa Taifa ili nchi
izidi kubarikiwa kwa amani na utulivu.
Huku Paroko ya Parokia ya Ludewa mjini Padre Cathbert Mlowe, alisema licha ya kuwa muumini katika
kanisa hilo, mbunge huyo amekuwa na kasumba ya kuwasaidia watu bila kujali
tofauti za imani na itikadi zao.
“Ninajua ninaweza kutafsiriwa kwa namna tofauti, lakini
nitasema tu ya kwamba Filikunjombe amekuwa mfano wa viongozi wanaowakumbuka
wahitaji kwa nyakati zote, na amekuwa mtu wa kurejea kwetu (Ludewa) mara kwa
mara, viongozi wa aina hii ndio wanaopaswa kushikwa mkono,”
Alisema wakati ambapo taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu,
wapo watu watakaijitokeza na kujinasibu kwa namna tofauti, ikiwa ni pamoja na
kukumbushia udugu uliopo kati yao na jamii za mahali wanapotoka ili
wachaguliwe.
“Watu wanaojitokeza kwenye jumuiya zetu na kujitambulisha
kwa familia na ukoo wanazotoka ili wachaguliwe, hawapaswi kupata nafasi hizo.
Tujiandaye kuwachagua viongozi wanaotokana na sisi, wale wanaokumbuka na kurudi
kuungana nasi katika kukabiliana na changamoto zetu kama anavyofanya huyu
mwenzetu,” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Anatoly Chowa,
alitumia misa hiyo kujitambulisha kutokana na kuhamishiwa wilayani humo
akitokea wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Chowa alisema Filikunjombe ni mbunge anayewatumikia wananchi
kwa ubunifu unaokidhi mahitaji ya umma, hali iliyo tofauti na wawakilishi
wengine.
Chowa aliyewahi kuwa Mbunge wa Biharamuro kwa miaka 10,
alisema katika kipindi chote cha ubunge wake hakuwahi kuwasaidia wapiga kura
wake kama anavyofanya Filikunjombe.
“Nimekuwa Mbunge kwa miaka 10, nimehudumu na Horace Kolimbe
(maremu), Stanley Haule na Stanley Kolimba, sijawahi kuyafanya mambo ama
kuwasikia wenzangu hao wakiyafanya kama anavyofanya Filikunjombe,” alisema.
No comments:
Post a Comment