Mshinda wa kitita cha shilingi milioni 10/- kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Shamila Ramadhani(kushoto)akikabidhiwa hundi yake na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud ‘JayMillions’ baada ya kuipuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo katikati ni mume wa mshindi huyo Abdallah Mahoka.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Dar Live wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live lililofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Balozi wa promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary Daud ‘Jaymillions’akiwasomea tarakimu kwenye hundi iliyokuwa na thamani ya shilingi milioni 10/-wakazi wa mbagala waliofika katika tamasha la Mwana Dar live lililofanyaika katika ukumbi wa Dar live mbagala jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka,Hundi hiyo ilikabidhiwa kwa mshindi wa promosheni hiyo Shamila Ramadhani(kusho)akiambatana na mumewe Abdallah Mahoka(katikati) Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mshinda wa kitita cha shilingi milioni 10/- kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Shamila Ramadhani(kushoto)pamoja na mumewe Abdallah Mahoka wakiinua hundi yao juu ili wakazi wa mbagala waliohudhuria tamasha la Mwana Dar Live waione baada ya kukabidhiwa rasmi na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud(hayupo pichani) baada ya kuipuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Dar Live wakati wa Tamasha hilo lililofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba akiwapagawisha washabiki wa muziki wake waliofurika katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mamaa Aisha Mashauzi akitumbuza muziki wa Taarabu katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Msanii wa nyimbo za mchiriku Sueleman Jabiri”Msaga Sumu”akisaga sumu ipasavyo kwa washabiki wa muziki wake wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Wapenzi wa burudani ya muziki wa kizazi kipya na muziki wa taarabu wamepata burudani ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka kutoka kwa magwiji wa muziki wa kizazi kipya na taarabu katika matamasha ya burudani yaliyoandaliwa na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania yaliyofanyika Coco Beach na Dar Live ,Mbagala jijini Dar es Salaam.
Tamasha la wazi lililofanyika Coco beach liliwavutia wakazi wengi wa jiji hususani vijana pia kuhakikisha watoto hawaachwi nyuma nao waliandaliwa burudani zao ambapo waliweza kucheza na kufurahia sikukuu ya Pasaka.
Wasanii wa kizazi kipya Bob Junior na Shilole waliacha historia ya aina yake kwa mamia ya washabiki wa muziki wa kizazi kipya waliofika katika fukwe ya Coco kwa jinsi walivyoweza kukonga nyoyo zao na kudhihirisha kuwa muziki wao ni wa kiwango cha juu pia walikuwepo wasanii mbalimbali chipukizi ambao pia walimwaga burudani kwa mashabiki.
Funga kazi ilikuwa Dar live Mbagala ambapo msanii mahiri wa Bongofleva Ali Kiba kwa kushirikiana na mwanamama anayetamba katika muziki wa taarabu nchini Aisha Mashauzi walimwaga burudani za aina yake na kupagawisha washabiki waliofika katika tamasha la Mwana Dar Live ukumbini hapo kusherehekea sikuu ya Pasaka.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu amesema kuwa kampuni yao imeamua kuandaa na kudhamini matamasha haya kwa ajili ya kuwapatia furaha na burudani wateja wake na wananchi kwa ujumla katika msimu huu wa sikukuu ya Pasaka na kuweza kuwakutanisha washabiki na wanamuziki wawapendao na itaendelea kufanya hivyo kupitia promosheni ya Ishi Kistaa na aliwakumbusha wateja kutuma neno STAR kwenda namba 15670 ili wapate fursa ya kuwakutanisha na wasanii wawapendao.
“Kama ilivyo kauli mbiu yetu kuwa “ukiwa na Vodacom maisha ni murua”tunahakikisha mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wetu pia tunajua kuwa kuna muda wanahitaji kufurahi kwa burudani hivyo ndio maana tunaandaa na kudhamini matamasha ya aina hii na tutaendelea kufanya hivyo siku zote ikiwa ni moja ya njia ya kusema ahsante kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono”Alisema.
No comments:
Post a Comment