Na Mwandishi Maalum, New York
Kufuatia
ongezeko la makundi ya dini yenye itikadi , matukio ya kigaidi,
kukosekana kuvumiliana na
maridhiano, Katibu Mkuu wa wa
Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amewageukia viongozi wa madhebu ya mbalimbali
dini duniani akiomba busara zao
na uongozi wao.
Amesema,
busara na uongozi wa madhehebu hayo ya
dini unahitajika sana katika kuhubiri na kueneza kuvumiliana, maridhiano,
stahimili, kuheshimiana na
kujenga utamaduni wa kuzungumza miongoni wa
jamii bila ya kujali dini zao au rangi zao.
Ban
Ki Moon ametoa wito huo siku ya Jumatano hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa, wakati wa mkutano wa ngazi ya juu
uliojadili kwa kina kuhusu dhana ya
kukuza uvumilivu na maridhiano mkazo ukiwa katika kujenga jamii yenye
Amani, jumuishi na namna ya kukabiliana na vurugu zitokanazo na itikadi kali za
kidini.
Mkutano
huo ambao ulianza siku ya jumanne
uliandaliwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Sam Kutesa kwa kushirikiana na Taasisi ya
Muungano wa Ustaarabu ambapo washiriki mbalimbali wakiwamo
viongozi wa madhehebu ya dini walipata fursa ya kutoa tathmini ya hali ya
sasa na hatari inayoikabili dunia na
watu wake hasa kutokana na kukithiri kwa wimbi la machafuko na
mauaji kwa visingizio mbalimbmali.
Mwakilishi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi ni miongoni mwa washiriki waliochangia majadiliano hayo
ambapo alielezea uzoefu wa Tanzania juu
ya namna ambavyo madhehebu ya dini ya
kiislamu na kikristo yalivyoanzisha na
kuenzi misingi ya majadiliano katika kutafuta suluhu na maridhiano ya
changamoto mbalimbali.
Akizungumza siku hiyo ya jumatano ambapo viongozi wa
madhehebu ya dini walipata fursa ya kutoa maoni, mitizamo na mapandekezo yao.
Ban Ki Moon alisema:
“
Waheshimiwa viongozi wa dini, leo naomba
busara zenu na uongozi wenu, kuna maeneo mawili ambayo mnaweza
kuleta matokeo. Moja tunahitaji kueneza na kukuza majadiliano
miongoni mwa madhehebu ya dini ili
kupunguza sitofahamu na mihemuko baina ya waumini wa dini .” akasema Ban Ki
Moon
Jambo la pili ambalo amelieza kuwa viongozi wa
dini wanaweza kutekeleza ni kuzungumzia mazingira yanayotoa fursa
kwa vikundi vyenye itikadi kali ya
kushawishi na kuvutia wafuasi wapya.
Amesema
Ban ki Moon , viongozi
wa madhehebu ya dini, wanaupeo mkubwa wa kutambua viashiria vya uwepo wa vurugu na vuguvugu la
waumini wao kurubuniwa na kuwa na
mwelekeo wa itikadi kali za kidini.
“Ninawaomba mtumie ushawishi wenu wa kiroho na uadilifu , kupinga maelezo yao kwa kusimamia
katika kiasi na maelewano ya pamoja.
Na kuongeza. Sauti zenu ni muhimu sana katika kukemea kauli za kibaguzi na kutafuta msimamo
wa pamoja”. amesisitiza katibu Mkuu
Mkuu
huyo wa Umoja wa Mataifa, ameeleza
kwamba ni vema kila mmoja wetu akajiuliza
ni nini kinachoshawishi au vutia itikadi
kali na ukereketwa wa kupindukia.
Akasema
wengi wanaojiunga na makundi yenye itikadi kali ni vijana lakini hivi sasa
kuna wimbi la wanawake wanaojiunga jambo alilosema linatisha Zaidi.
Ban
Ki Moon amesema, makombora yanaweza kuwauwa magaidi. Lakini
anashawishika kuamini kwamba utawala bora ndio utakaomaliza ugaidi kwa
kusimamia misingi ya utawala wa sheria,
haki za binadamu, kumaliza umaskini, na kuondoa pengo la kati ya walio nacho na
wasionacho.
Katibu
Mkuu amewaeleza viongozi hao wa dini kwamba anakusudia kuunda Jopo la washauri
la viongozi wa dini na wengine litakalotoa mwongozo wa namna ya kushughulikia changamoto mbalimbali.
Aidha amebainisha kwamba baadaye mwaka huu
atawalisha Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kuzuia vurugu zinazosababishwa na ukereketwa wa kupindukia.
Viongozi
wa madhehebu ya dini waliozungumza
katika mkutano huo, walisisitiza sana kuhusu umuhimu wa utoaji wa elimu na mafunzo yanayozingatia au
kujielekeza katika kukuza misingi ya kustahimiliana na kuheshimiana kwa
misingi ya tofauti za kidini, kiimani, uhuru wa mtu kuabudu bila ya kujali tofauti ya rangi
yake au nchi anayotoka.
Wamesisitiza
kwamba elimu hiyo inapashwa kutolewa kuanzia katika shule za awali hadi vyuo
vikuu, jambo ambalo wanaamini kwamba kama likifanyika kwa umakini siyo tu
litawaepusha vijana kujiingiza
katika misimamo ya itikadi kali na
ukereketwa wa kupindukia lakini pia utaifanya dunia kuwa mahali salama.
Vile
vile wamesisitiza kuwa, hakuna dini yoyote inayohubiri chuki, kubaguana au
kuuana, bali dini zote na vitabu vya
dini vinasisitiza katika kuishi kwa
upendo, Amani, kuvumiliana na kuridhiana
kwa kuwa wote ni watoto wa mungu.
Vyombo
vya habari ikiwamo mitandao ya kijamii
pia viliguswa katika majadiliano hayo, ambapo wazungumzaji wengi
walivitaka viwe sehemu ya utoaji wa elimu na kujenga
misingi ya ustaarabu wa kuvumiliana na
kujiepusha kuwa vipaza sauti au wasemaji au wachochezi wa itikadi kali za kidini na ukereketwa wa
kupindukia.
No comments:
Post a Comment