Monday, March 30, 2015

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA WILAYA YA ROMBO

 Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wakirejesha kadi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo.
 Wakazi wa Tarakea wakifurahia jambo wakati katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihutubia
Pichani kushoto ni aliyekuwa Katibu Mwenezi na Katibu wa Mbunge wa CHADEMA,wilaya ya Rombo John Tarimo akitangaza rasmi kurejea chama cha CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimsikiliza.
 Mmoja wa Wakazi wa Rombo akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwa furaha kubwa kama aonekanavyo pichani
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vikundi vya utamaduni wakati akiwasili kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Rombo.
 Baadhi ya Vijana kwa niaba ya vijana zaidi ya 900 wa Boda boda wakiwa wamekabidhiwa  vyeti vya Bima ya Afya ya jamii.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana akiwahutubia wananchi wa Rombo kabla ya kufungua ofisi ya CCM wilaya ya Rombo ambapo aliwaambia wananchi hao kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo kwa wananchi na kutaka kuacha ushabiki wa kisiasa ambao hauwanufaishi wao zaidi ya wabunge waliowachagua ambao wanakaa madarakani bila kuwasaidia wananchi,alisema kuna wabunge hawafanyi mikutano,hawachangii maendeleo katika mfuko wa jimbo, wanapinga bajeti ya maendeleo hawatoi taarifa za huduma mbali mbali za kijamii ,wala hawasaidii katika miradi mbali mbali ya wananchi ikiwa umeme,maji ,barabara na afya ni vyema wakaachwa na kupisha kiongozi anayejua na kutambua matatizo ya wananchi.


  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Rombo nje ya ofisi ya CCM wilaya na kuwaambia CCM imejiimarisha zaidi na itaendelea kujiimarisha na kuwataka wananchi hao kuendelea kukiamini chama chao chenye sera inayoeleweka.
  Vikundi vya wajasiriamali kutoka wilaya ya Rombo katika picha ya pamoja wakiwa wameshikilia mikataba na hundi walizokabidhiwa leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akikata utepe kuzindua ofisi ya CCM wilaya ya Rombo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya namna uzalishaji unavyofanyika kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kutengeneza vinywaji ya Bellaview Fresh Fruits Processing Industry Ndugu Shanel John Ngowi.Kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na viongozi mbalimbali wa mkoa na Wilaya wakiondoka kwenye kaburi la Wanafunzi wa Shule ye Sekondari ya Shauri Tanga waliokufa baada ya kuungua moto na  kuzikwa kaburi  la pamoja ambapo pia waliweka mashada ya maua.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya na kupokea taarifa fupi ya kazi za chama na Utekelezaji wa Ilani.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuvuta waya wa umeme kwenye mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Kirongo Samanga ikiwa sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
Baadhi ya Wananchi wakimtazama Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiruka kukagua tanki la maji katika mradi wa maji safi na salama kijiji cha Kahe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji ikiwa sehemu ya uzinduzi wa huduma ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Kahe pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Lembris Marangushi Kipuyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi. Petronila Jakob kama ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma ya maji katika kijiji cha Kahe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Tarakea wilayani Rombo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Tarakea Polisi.

Katibu Mkuu wa CCM anaendelea na ziara za kujenga na kuimarisha Chama mkoani Kilimanjaro pamoja na kukagua, kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010. Katika ziara yake ya leo wilayani Rombo ,Katibu Mkuu alishiriki shughuli mbali mbali ,zikiwemo kufungua ofisi ya chama ya wilaya, kukabidhi Bima ya afya kwa vijana 900 wa boda boda,Kukabidhi mikataba na hundi ya vikundi 2o vya wanawake wajasiriamali. 
 Wakazi wa Tarakea wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya polisi Tarakea.
 Wakazi wa Tarakea wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya polisi Tarakea.
 Wakazi wa Tarakea wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya polisi Tarakea.

No comments: