Saturday, March 28, 2015

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE NDANI YA JIMBO LA SAME MASHARIKI.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipata maelezp mafupi namna  Tangawizi inavyochakatwa na kusindikwa katika kiwanda hicho,ambapo Katibu Mkuu Ndugu Kinana alishuhudia kiwanda hicho kukabidhiwa mashine za kuchakata Tangawizi kutoka SIDO,Kulia ni Mbunge wa Same Mashariki,Mh.Anne Kilango Malecela.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi namna  Tangawizi inavyosindikwa katika kiwanda hicho,ambapo Katibu Mkuu Ndugu Kinana alishuhudia kiwanda hicho kukabidhiwa mashine za kuchakata Tangawizi kutoka SIDO.Kiwanda hicho kilizinduliwa na Rais Kikwete mnamo Oktoba,2012.Katika taarifa iliyosomwa kiwandani hapo inaeleza kuwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 500 zimetumika kwa ajili ya ujenzi pamoja na shughuli nyingine za kujenga uwezo ili kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi kwa ufanisi.
 Meneja wa SIDO mkoa wa Kilimajaro Bwa.Daniel Njowero akikabidhi nyaraka za mashine mpya za kuchakata Tangawizi kwa Mwenyekiti wa Bodi wa Kiwanda cha Tangawizi,Bwa.Yonaz Yohana Mgonja,huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakishuhudia
 Moja ya shamba la Tangawizi .
 Moja ya jengo la chuo cha VETA kilichopo katika kijiji Maore-Same Mashariki ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikagua na kujionea ujenzi wake,chuo hicho kinafadhiliwa na Kampuni ya Suzuki ya nchini JAPANI 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza kwenye mkutano mkuu wa jimbo la Same Mashariki,Ndugu Kinana pia alipokea taarifa ya kazi  za chama na taarifa ya Utekelezaji wa ilani.
 Wananchi wakishangilia jambo
  Sehemu ya umati wa Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakishangilia jambo katika mkutano huo wa hadhara.
 Mmoja wa watoto akiwa amebeba kipeperushi cha kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake ndani ya Jimbo la Same Mashariki
 Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakifuatilia mkutano huo wa hadhara
 Sehemu ya umati wa Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakifuatilia mkutano huo wa hadhara
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusuka nondo za nguzo za daraja la Mang’a Myamba wakati alipokagua ujenzi wa Daraji hilo Same Mashariki mkoani Kilimanjaro.Ujenzi wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais Kikwete kwa wananchi wa Same Mashariki katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
 Ujenzi wa daraja la Mang’a Myamba,Same Mashariki ukiendelea,Ujenzi wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais Kikwete kwa wananchi wa Same Mashariki katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010

No comments: