Thursday, March 12, 2015

WAZIRI WA ARDHI AANZA ZIARA JIJINI MWANZA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akitoa maelezo ya hali ya migogoro ya Ardhi iliyopo Mkoani Mwanza kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi alipokutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa katika ziara yake Mkoani Mwanza.Picha na Muungano Saguya- Mwanza
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mh. Jaji Mfawidhi Makalamba alipokutana naye ofisini kwa Jaji huyo Jijini Mwanza ili kupata namna bora ambayo mhimili wa mahakama unaweza kusaidia kutatua migogoro ya ardhi nchini. Waziri Lukuvi yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Mwanza yenye nia ya kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Jijini Mwanza Mh. Makaramba na watendaji wa sekta ya ardhi na mahakama alipomaliza mazungumzo na Jaji huyo jana.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi akisiliza maelezo ya Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi kanda ya ziwa Bw.James Silas (hayupo pichani) alipotembelea Baraza hilo jana kuona namna wanavyoshughulikia mashauri ya ardhi na kutoa haki kwa wananchi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi akimkabidhi Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi kanda ya ziwa Bw.James Silasshilingi milioni moja(1000,000/=) ili kununua karatasi za kuwezesha utoaji wa hukumu za wananchi zinazohusu kesi za ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi akiwasalimia Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela alipowasili katika Halmashauri hiyo kukagua shughuli za ardhi na kusiliza moja kwa moja malalamiko ya wananchi na kutatua kero zao.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi akikagua utendaji wa watumishi wa Mipango Miji na Ardhi Wilayani Ilemela. Katika ukaguzi wa ghafla alioufanya katika masijala hiyo, Waziri Lukuvi aligundua mafaili kutofanyiwa kazi ipasavyo na watendaji hao hivyo kuwafanya baadhi ya wananchi kutopata haki zao kwa mika takribani 21.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi akitoa maelezo ya awali kwa wananchi wa Wilaya ya Ilemela (hawapo pichani) waliofika kueleza kero zao. Katika mkutano huo Waziri alisisitiza Maafisa Ardhi na Mipango Miji kufanya kazi kwa kufuata maadili na haki ili kuwaondolea wananchi wanyonge kero za ardhi.
Mmoja wa wananchi takribani 60 waliofika na kuwasilisha malalamiko ya kunyimwa haki ya ardhi na watendaji wa ardhi na mipango miji Wilayani Ilemela kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi jana.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willian Vangimembe Lukuvi akipokea rundo la malalamiko ya wananchikutoka kwa Wenyeviti wa Mitaa yahusuyo ardhi alipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Mwanza jana. Waziri Lukuvi kesho atakutana na wananchi wengine katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kusikiliza kero zao.

No comments: