Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataiafa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani) waliopo hapa nchini kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea hapa nchini. Masuala hayo ni pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na mauaji ya Albino, Mkataba wa Makubaliano ya Chama cha SPLM cha Sudan Kusini na Hali katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu kama DRC. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa DRC hapa nchini, Mhe. Juma Khalfan Mpango na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam tarehe 03 Machi, 2015 |
No comments:
Post a Comment