afisa mawasiliamo ya TGNP Bw Melikizedeck Karol
wakati akitoa mada ya uchaguzi mkuu
Na matukiodaimaBlog, Mbeya
WAKATI
vuguvugu la uchaguzi mkuu mwaka 2015 likiendelea kushika kasi
ndani ya vyama vya siasa kwa wanachama mbali mbali kujitokeza
kutangaza nia ,mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) umewataka wanawake
nchini kujitokeza kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais .
Wito
huo umetolewa afisa mawasiliamo ya TGNP Bw Melikizedeck Karol
wakati akitoa mada ya ushiriki wa wanawake kwenye uchaguzi mkuu
mwaka 2015 wakati wa mafunzo ya siku mbili ya wanahabari mikoa ya
nyanda za juu kusini yaliyomalizika leo jijini Mbeya.
Alisema
kuwa usawa katika nafasi za uongozi wa kutaka kuwa na asilimia 50
kwa 50 kati ya wanawake na wanaume ni lazima utimie katika
uchaguzi huu kwa wanawake kuanza kujitokeza kuwania nafasi mbali
mbali zikiwemo za juu kama Urais ,ubunge na udiwani .
Karol
alisema kuwa kasi ya wanawake na vijana kujitokeza katika nafasi
mbali mbali za uongozi inapaswa kuanza kujionyesha kuanzia sasa
ili ikiwezekana bunge la baada ya uchaguzi mkuu 2015 idadi ya vijana
na wanawake iongezeke zaidi bungeni.
"Hivi
wataka kusema hakuna mwanamke katika nchi hii ambae anaweza
kuongeza nchini kama Rais na kama wapo kwanini hawajitokezi kugombea
nafasi za juu kama Urais .....lazima wanawake wachangamkie nafasi
hiyo "
Kwani
alisema kuwa katika jamii mwanamke ndie anayekumbwa na
changamoto mbali mbali katika jamii na kuwa iwapo wanawake
wataendelea kuwa nyuma katika kuwania nafasi hizo bado changamoto
zilizopo zitaendelea kuwatesa wanawake .
Alisema
kwa mwaka 2005 kuwa akidi nzima ya bunge la jamhuri ya muungano wa
Tanzania ni wabunge 357 kwa mujibu wa katiba hata hivyo viti
maalum pekee ni 102 sawa na asilimia 28.6 vilivyogawanywa miongoni mwa
vyama vya siasa kwa kuzingatia matokeo ya uchaguzi kati ya viti 239
vya majimbo (vikiwemo kutoka Zanzibar) ni wanawake 21 tu sawa na
asilimia 8.8 ndio walipewa viti vya kuchaguliwa bungeni.
Huku
idadi ya madiwani wa kuchaguliwa asilimia 4 na wenyeviti wa
vijiji ni asilimia 2 wakati wenyeviti wa vitongoji ni asilimia 3 .
Hivyo
alisema ni wajibu kwa vyombo vya habari na wanawabari nchini
kuendelea kuhamasisha makundi ya vijana na wanawake kujitokeza
kwa wingi katika nafasi za udiwani ,ubunge na Urais katika uchaguzi
mkuu mwaka huu.
Alisema
kuwa sera ya Taifa ya vijana pamoja na mkataba wa vijana wa Afrika
unalitambua kundi la vijana kama ni rasilimili mojawapo muhimu sana
kwenye maendeleo na pia katika kulinda amani na utulivu kwenye bara
la afrika.
"Hata
hivyo pamoja na kwamba vijana ni zaidi ya asilimia 60 bado mchango na
thamani ya vijana haujulikani ipasavyo kwenye Demokrasia ya
Tanzania huku thamani yao ikionekana tu nyaraka za uchaguzi kwa
kutumiwa kama walinzi au wapambe wa wagombea"
Alisema
ni vema vijana kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu
la wapiga kura ili kuweza kutumia haki yao ya msingi ya
kuchaguliwa na kuchagua .
|
No comments:
Post a Comment