Tuesday, March 31, 2015

Ujumbe kutoka Chuo cha Kijeshi cha Nigeria watembelea Wizara ya Mambo ya Nje

Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw.Elibariki Maleko(katikati) akizungumza kuukaribisha Ujumbe kutoka Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha nchini Nigeria (hawapo pichani) ulipokutana na Watendaji wa Wizara kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu Sera ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa. Ujumbe huo unaongozwa na Brigedia Generali Jimoh (wa pili kushoto) na upo nchini kwa ziara ya mafunzo. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw.James Lugaganya ( kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Innocent Shiyo (wa pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi.Maulidah Hassan.

Mwenyeji wa Ujumbe huo kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Brigedia Jenerali Mwemnjudi (mwenye nguo nyeupe) pamoja na Mwambata wa Jeshi katika Ubalozi wa Nigeria hapa nchini Brigedia Jenerali Erick Angaye wakimsikiliza Bw. Maleko (hayupo pichani)
Sehemu ya Maafisa wa Jeshi kutoka Nigeria wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Bw. Maleko
Maofisa na Wanachuo wa Chuo cha Kijeshi cha Nigeria wakati wa mkutano huo
Mmoja wa wanachuo akiuliza swaliwakati wa mkutano huo
Kiongozi wa msafara wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha nchini Nigeria, Brigedia Jenerali Jimoh akimkabidhi zawadi ya nembo ya chuo hicho Bw. Maleko
Picha ya pamoja.
Picha na Reuben Mchome

No comments: