Sunday, March 8, 2015

TASWIRA MBALI MBALI KWENYE MTANANGE WA SIMBA NA YANGA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO

Balozi wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (mwenye miwani) akiongozana na wadau mbali mbali wa IMETOSHA MOVMENT pamoja na wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakiingia Uwanjani,ikiwa ni katika muendelezo wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino yaliyobeba ujumbe wa IMETOSHA.
Sehemu ya Wachezaji timu za Simba na Yanga wakiwa wamevalia fulana zenye ujumbe wa IMETOSHA MAUAJI YA ALBINO,wakati wakiingia uwanjani.
Balozi wa kujitolea wa kampeni ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino, Henry Mdimu (wa tatu kushoto) akizungumza machache juu kampeni yake ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino iliyobeba ujumbe wa IMETOSHA MAUAJI YA ALBILO,kabla ya kuanza kwa kipute cha Simba na Yanga uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Kikosi cha Simba.
Kikosi cha Yanga.
 Beki wa Timu ya Simba,Kessy Ramadhan akiwania mpira na Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Danny Mrwanda wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Simba imeshinda bao 1 - 0 lililotiwa kimiani  kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji,Emmanuel Okwi mnamo dakika ya 52 ya mchezo.
 Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Danny Mrwanda akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Simba,Kessy Ramadhan wakati wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 Nyanda nambari moja wa timu ya Simba,Ivo Mapunda akiwa ametulia langoni kwake tayari kwa kuzuia shuti lililopigwa na Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva.
Wakati mtanage ukiendelea,ghafla likatokea zogo baina ya Nahodha wa Timu ya Yanga na Kiungo wa Simba,Abdi Banda na mambo yalikuwa hivi.
"Beki hasififiiiii lakini hapa anastahili sifa....",Beki wa Simba,Juuko Murshid akiruka juu kuondoa mpira uliokuwa ukielekea langoni kwake,mbele ya Washambuliaji wa Yanga.
Kipa wa Yanga,Ally Mustafa "Bartez" akiwa ameruka juu kuondoa hatari langoni kwake.
Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva akiangalia namna ya kumtoka Beki wa Simba.
Beki wa Simba,Kessy Ramadhan akimzungusha mshambuliaji wa Yanga.
Anacheza paleeeee Ivo Mapunda.
Haya nendeni kuleeeeee...... 
Wee kipa hili Taulo lako silitaki hapa,naliweka huku nje.
Mshambuliaji wa Yanga,Amis Tambwe akiachia nduki kali ambalo hata halikuzaa matunda.
Mashabiki wa Yanga wakijifariji.
Washabiki wa Simba wakiwabeza wenzao wa Yanga.
Wadau wa IMETOSHA wakiendelea kuwakilisha uwanjani.

Umati wa Washabiki wa Timu ya Simba ukiwa umefurika uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam kuipa sapoti timu yao ambayo haikuwaangusha leo,baada ya kuwatandika bao 1 - 0 watani zao wa jadi Yanga,lililotiwa kimiani  kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji,Emmanuel Okwi mnamo dakika ya 52 ya mchezo.
Ulinzi ulikuwa ni wa uhakika kabisa.
Hatari lakongoni mwa timu ya Simbaaaaa....
Kadi Nyekunduuuuu kwa Mchezaji wa Yanga,Haroun Niyonzimaaaaa.... baada ya kupiga mpira ulioingia wavuni baada ya refa kupiga filimbi kuwa ni faulo.
Niyonzima anamzonga Mwamuziii
Mshambuliaji wa Yanga,Amis Tambwe akizungumza na Mwamuzi juu ya Kadi aliyopewa Niyonzima.
Ukiangalia vyema utabaini kitu.




Furaha ya ushindi.

No comments: