Askari Polisi wa kike wa kitengo cha dawati la jinsia la Polisi wakisuburi kutoa elimu kwa wananchi kwenye maadhimisho ya kitaifa ya siku wa wanawake duniani.
Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa ya Taifa wa Bima ya Afya wakiwa eneo la banda lao.
Dawati la Jeshi la Magereza wakionesha namna wanavyohudumia wafungwa wanawake katika ujasiliamali.
Madaktari wa NHIF wakiwahudumia wateja kupima afya zao.
Meneja wa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF , Anjela Mziray akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, alipolitembelea banda hilo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Rajab Rutengwe ( kushoto) akitoa shukrani zake baada ya kusoma hotuba ya uzinduzi wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya wanawake duniani.
Mmoja wa wanawake wajasiliamali akipata maelezo ya elimu ya viwango vya ubora wa bidhaa katika banda la TBS.
Naibu Waziri Dk Pindi Chana akitoa salamu za wizara yake.
Ofisa mwandamizi wa ushauri wa wateja wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Joan Magori ( kushoto) akimfafanulia jambo mteja aliyetembelea banda hilo.
Ofisa uhusiano wa Idara ya Uhamiaji , Tatu Burhan ( wa kwanza kushoto ) akitoa maelezo kwa RC Moro ,Dk Rutengwe pamoja na Naibu Waziri , Dk Chana , namna ya passpoti zinayotolewa na Idara hiyo.
PICHA YA PAMOJA RC MORO NA NAIBU WAZIRI DK CHANA.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake kitafa akibonyeza kitufe katika kompyuta mpakato kwa ajili ya kupinga king'ora ili kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho hayo jana ( Machi 6) ambayo kilele chake ni machi 8, mwaka huu ,katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro ( anayepiga makofi) ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana ( kulia) ni Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa , upande wa Serikali za Mitaa, Noel Kazimoto.
VIONGOZI WAANDAMIZI
Na John Nditi, Morogoro
SERIKALI za awamu zote nne za uongozi wake imekuwa katika mstari wa mbele wa kuhakikisha kuwa inatoa kipaumbele katika masuala yanayohusu uwezeshaji wanawake kwenye nyanja zote ili kuleta uswa wa kijinsia.
Pamoja na kutambuliwa mchango mkubwa unaotolewa na wanawake wajasiliamali na wadau mbalimbali katika kuimarisha uchumi wa taifa , bado zinahitajika juhudi kubwa za kuhakikisha maendeleo ya wanawake yanaonekana na kuwa endelevu.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, katika hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe, Machi 6, mwaka huu wakati wa kuzindua maadhimisho ya kitaifa ya siku ya wanawake Duniani yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri wa mjini hapa ambayo kilele chake ni Machi 8, mwaka huu, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dk Jakaya Kikwete.
Katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, kitaifa kwa mwaka huu kaulimbiu yake ni ‘ Uwezeshaji Wanawake , Tekeleza wakati ni Sasa” .
Kwa mujibu wa Waziri Simba , katika kutimiza azma hiyo, serikali imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa masuala ya uwezeshaji wanawake yanaingizwa katika sera, sheria , mikakati , mipango na proramu mbalimbali za kitaifa na kisekta.
Hata hivyo alisema katika ngazi ya kitaifa na kikanda, serikali imesaini na kuridhia mikataba , itifaki, maazimio na matamko mbalimbali yanayihusu maendeleo , haki na ustawi wa wanawake ngazi ya kimataifa na kikanda .
“ Bado kuna mambo mengi ambayo tunapaswa kuyaangalia na kuyawekea mikakati mipya ya utekelezaji na huu ndiyo wakati mwafaka kwa kuwa sasa tupo katika kipindi cha kutathimini utekelezaji wa Azimio la Ulingo wa Beijing ( 1995-2015).
Pamoja na hayo alisema, serikali pia imehakikisha kuwa masuala ya jinsia na wanawake yanazingatiwa katika mikakati , mipango na program mbalimbali zikiwemo ya dira ya taifa ya mwaka 2015, Mpango wa Mkukuta na Mkuza sambamba na mpango wa taifa wa miaka mitano.
“ Kama taifa tumeansisha dawati la jinsia katika wizara, idara zinazojitegemea , wakala wa serikali , mikoa na halmashauri mbalimbali na katika NGOs na hata sekta binafsi ili kufuatilia na kuratibu masuala ya kuwezesha wanawake katika sekta hizi” alisema Waziri Simba .
Katika hatua nyingine , Waziri Simba kupitia hotuba hiyo iliyosomwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro kwa niaba yake , amewataka wanawake nchini kujitokeza kwa wingi kuipingia kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa ifikapo Aprili 30, mwaka huu.
Waziri Simba amewakubusha wanawake kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi mkuu , hivyo watumie fursa hiyo kuangalia ushiriki wao katika changuzi zilizipita zilikuwaje ili kubuni njia za kuhamasishana ili wajitokeza kupiga kura na pia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa ngazi zote .
“ Lengo hapa ni kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi zote za uongozi na maamuzi kwa nafasi ya udiwani, ubunge na urais “ alisema Waziri Simba.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Kibena Kingo, akitoa shukrani kwa niaba ya wanawake wa mkoa wa Morogoro, aliipongeza serikali kwa kuwapatia fursa mbalimbali za kiuchumi na kiuongozi wanawake wengi nchini.
Pia alisema , wanawake wa mkoa huo watakuwa bega kwa bega kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapingiwa kura nyingi za ndiyo kwa kuwa imekuwa na mambo ya msingi kwa makundi yote bila ubaguzi.
Mbali na hayo alisema kuwa, pia wanawake wanajitokeza kwa wingi katika kuwania nafasi za kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu katika nafasi ya udiwani, ubunge na hata urais.
No comments:
Post a Comment