Inocent Melleck akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kumchangia fedha kwa ajili ya kuchukulia fomu za kuwania Ubunge katika jimbo la Vunjo.
Innocent Melleck akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi hao waliojitokeza kumchangi fedha kwa ajili ya kugombea Ubunge katika jimbo la Vunjo.
Baadhi ya wananchi katika Jimbo la Vunjo wakimsikiliza Innocent Melleck waliyemchangia fedha kwa ajili ya kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
WANANCHI wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro wakiwamo wajasiliamali wadogo wamechangishana shilingi milioni tisa na kumkabidhi Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Innocent Melleck kwa ajili ya kuchukulia fomu ya kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye mji mdogo wa himo baadhi ya wananchi hao Halid Msango,Jonas Mamuya na Aisha Mkwizu walisema kwa pamoja wananchi wa jimbo la Vunjo bila kujali itikadi zao za vyama wamemchangia kiasi hicho cha fedha ili kimsaidie kuchukulia fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda utakapofika
Katika tukio hili tumeshiriki wananchi wa jimbo hili la Vunjo kwa umoja wetu bila kujali itikadi za kisiasa ambapo hapa pia wapo wanachama wa vyama vya NCCR Mageuzi,TLP,CHADEMA na CCM soote tumeshiriki katika kuchanga fedha hizi lakini pia wapo makundi mbalimbali kama vile mama lishe, madereva wa Bodaboda, wauza mboga, na vijana wengine wanaofanya biashara ndogondogo na wapiga debe kwenye vituo vya mabasi ya daladala.
Aidsha wananchi wao waliafikiana kuunda kamati ya kuzunguka jimbo zima kuhakikisha kuwa wanakusanya fedha za michango na kuhamasishana kwaajili ya kuhakikisha Melleck anapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Katika kamati hiyo mwenyekiti ni Mzee shayo na katibu wa mwika kuwa katibu huku katibu kata kata ya kilema kusini Shabani Kwezi kuwa mjumbe na wajumbe wawili toka kila kata za jimbo hilo hivyo kuwa na jumla ya wajumbe 36 katika kamati hiyo ambayo ilianza majukumu yake mara moja.
Alisema zoezi hilo liliongozwa na zaidi ya wajumbe 1000 wa nyumba 10 wa CCM na kumtaka, Melleck kuchukua fomu ya kuwani nafasi hiyo ya uwakilishi katika uchaguzi ujao.
Kwa upande wake Bwana Melleck aliwashukuru wananchi hao kwa ujasiri mkubwa na Imani kubwa walioonyesha kwake , nimefarijika sana kuona wananchi wenye kipato kidogo cha fedha wanachanga kiasi hiki cha fedha na kunikabidhi ili nichukulie fomu na mimi naahidi kutowaangusha kwa hilo, nitafanya hivyo muda ukifika," alisema
Alisema jimbo la Vunjo linakabiliwa na changamoto nyingi hususan ukosefu wa ajira kwa vijana na kukosa mtetezi wa asilimia tano ya mapato yatokanayo na Mlima Kilimanjaro ili yarudi kwa wananchi, Matatizo ya kielimu na maslahi ya walimu,Migogoro ya ardhi na miundombinu kuwa itakuwa kipaumbele chanya mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo mapema mwezi octoba mwaka huu.
Melleck ambaye ni kijana alisema kwa umoja ulioonyeshwa na wana Vunjo anaamini kwamba utaendelea hivyo hivyo mpaka uchaguzi utakapomalizika na kuhakikisha CCM inashinda.
Alisema amejiandaa kufanya mengi katika jimbo la Vunjo na kwamba njia pekee ya kupita ili kupata ushindi ni kuwashirikisha wananchi wote kwa kuwa anaamini kwamba jimbo hilo litakuwa huru kufungua fursa za kuichumi ikiwa atakuwa mwakilishi wake bungeni.
"Vunjo kuna utajiri mwingi na kinachotakiwa ni mtu mwenye maono ya kuona fursa ili aweze kuwashirikisha wananchi kuzifikia kwa ajili ya maendeleio yao na watoto wao," alisema
Melleck aliongeza kuwa wananchi wanayo nafasi ya kuona na kuwachuja wagombea wote ili waweze kupata mtu sahihi atakayeweza kuwavusha hapo walipo na kusonga mbele kwa manufaa ya wana Vunjo wote.
No comments:
Post a Comment