Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wa tatu kulia na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya wa kwanza kushoto wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za makazi zinazojengwa na Shirikia la Nyumba la Taifa (NHC) katikati ya Manispaa ya Sumbawanga tarehe 26/03/2015. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Ndugu Nehemia Mchechu nyumba hizo ambazo ni za ghorofa moja zitauzwa baada ya kukamilika ujenzi wake kwa njia ya fedha taslimu na njia ya Mikopo ya benki.
Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi katikati akiweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za makazi zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa Mjini Sumbawanga kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama na Serikali Mkoani Rukwa tarehe 26/03/2015.
Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Ndugu Nehemia Mchechu katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za makazi za shirika hilo Mjini Sumbawanga.
Michoro ya mradi huo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi (hawapo pichani) wenye malalamiko mbalimbali yanayohusu migogoro ya ardhi Mkoani Rukwa katika ukumbi wa RDC Mjini Sumbawanga tarehe 26/03/2015. Mhe. Lukuvi aliwatangazia wananchi wenye malalamiko sugu wamuandikie wakiambatisha na vielelezo husika na kuviwasilisha kwake ili aweze kuvifanyia kazi, alisema kuwa "..ni muda sasa wa kuponya mioyo ya watu ambao wamezulumika kwa muda mrefu..." Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya.
Mzee Julius Nkana Mkazi wa Sumbawanga akiwasilisha malalamiko yake ya mdomo na maandishi kuhusu mgogoro wa ardhi kwa Mhe. William Lukuvi. Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya Migogoro takribani yote iliyowasilishwa ilionekana kuibuka kutokana na maeneo mengi yasiyo rasmi ambayo hayajapimwa na kupewa umiliki unaotambulika kisheria. Aliongeza kuwa ipo haja kubwa ya Serikali na mamlaka husika kuimarisha eneo la upimaji wa maeneo na kutoa umiliki wa ardhi kuazia viwanja vya makazi na mashamba kuepusha migogoro ya kuzulumiana ardhi ambayo imekua ikiua kwa kasi siku hadi siku.
Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi kulia akipokea malalamiko ya maandishi ya migogoro ya ardhi kutoka kwa wananchi wa Mkoa wa Rukwa waliopanga mstari katika ukumbi wa RDC.
Zoezi hilo liliambatana na mahojiano mbalimbali ambapo kwa wale wenye malalamiko ambayo kesi zake zipo mahakamani na hazijatolewa uamuzi walishauriwa kuendelea na kesi zao mpaka zitakapomalizika, Ama kwa wale ambao kesi zao zinatatulika zitafanyiwa kazi na Wizara ya ardhi ambapo Waziri husika Mhe. William Lukuvi aliahidi kujibu barua zao za malalamiko, Malalamiko hayo pia yatafanyiwa kazi na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi nyanda za juu kusini, Ofisi ya baraza la ardhi Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimuhoji diwani wa Kata ya Kizwite Ndugu Mavazi (kushoto) kuhusu malalamiko ya muwekezaji Ndugu Azizi Tawaqal (wa pili kushoto) kuhusu madai kuwa wananchi wanamtumia katika kuuza mashamba yaliyonunuliwa na ndungu Aziz Tawaqal licha ya kuwa walishalipwa fidia. Kesi hiyo bado ipo mahakamani na Mhe. Waziri amemuagiza Kamanda wa Polisi Wilaya ya Sumbawanga (OCD) kusimamia sheria kuhakikisha maeneo hayo hayauzwi na hakuna shughuli yeyote inayoendelea mpaka kesi iliyopo mahakamani ikamilike na kutoa uamuzi.
No comments:
Post a Comment