Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliekuwa Kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars), marehemu Sylvester Balunzi Mashishigulu ‘Marsh’, leo kwenye uwanja wa Shule ya msingi Mirongo,Jijini Mwanza.Marehemu Marsh amezikwa kwenye makaburi ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza.Picha zote na G Sengo Blog.
Familia ya Marehemu Sylvester Balunzi Mashishigulu ‘Marsh’, ikiwa kwenye huzuni kubwa baada ya kuondokewa na mpendwa wao,wakati wa ibada maalum ya kumuada ilitofanyika kwenye uwanja wa Shule ya msingi Mirongo,Jijini Mwanza.
Meya wa Jiji la Mwanza , Stanslaus Mabula alisema,jiji la Mwanza akielezea wasifu wa marehemu Marsh, ikimbukwe kuwa Mstahiki ndiye mlezi wa kituo cha soka cha Marsh Academy.
Mchezaji wa zamani wa Yanga na Timu ya Taifa (Taifa Stars), Edibily Jonas Lunyamila (kushoto) akielezea namna alivyomfahamu marehemu Marsh,wakati wa kuaga mwili wake leo kwenye kwenye uwanja wa Shule ya msingi Mirongo,Jijini Mwanza.kulia ni mchezaji wa zamani wa timu ya Pamba, Yanga na Taifa Stars, Fumo Felician akiwa na majonzi.
Huzuni kubwa ilitawaka kwa timu ya vijana wa U17 toka kituo cha Marsh Academy.
Sehemu ya umma uliofika kumuaga Marehemu Marsh.
Sehemu ya umati wa wadau wa soka jijini Mwanza ukiwa umelizunguka Kaburi la Marehemu Sylvester Balunzi Mashishigulu ‘Marsh’ kabla ya mazishi yake.
Sehemu ya vijana wa kituo cha soka cha Marsh Academy wakiwa kwenye mazonji makubwa kwa kuondokewa na mzezi wao.
Baadhi ya Viongozi na wadau wa soka Mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye Ibada ya kumuaga aliekuwa Kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars), marehemu Sylvester Balunzi Mashishigulu ‘Marsh’, aliezikwa leo kwenye makaburi ya uwanja wa Shule ya msingi Mirongo,Jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment