Mkurugenzi wa Kampuni ya Angels Moment, Naima
Malima akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi uliofanyika
Mkuranga mkoani Pwani. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Abdallah Kihato na Mkurugenzi wa
Mwang'amba Communication, James
Mwang'amba. (Picha na John Dande)
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Abdallah Kihato akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi lililofanyika Mkuranga mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa
Mwang'amba Communication, James
Mwang'amba akitoa mada kwa wanawake wajasiriamali.
Wanawake wajasiriamali wakiwa katika kampeni ya mwanamke na uchumi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Angels Moment, Naima
Malima (kulia) akipeana mkono na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Abdallah Kihato.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Abdallah Kihato(wa tatu kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Angels Moment, Naima
Malima.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI
kuu wa Angels Moment, Naima Malima, amesema utafiti mbalimbali
umethibitisha kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanawake wa Bara la Afrika
katika masuala ya fedha na fursa zinazowazunguuka ni ukosefu wa elimu.
Kauli hiyo aliitoa juzi wakati ufunguzi wa
Kampeni ya Mwanamke na Uchumi iliyofanyika wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Kampeni hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya
hiyo, Abdallah Kihato, Madiwani na maofisa maendeleo ya jamii, wawakilishi wa
taasisi mbalimbali.
Naima, alisema hali hiyo ya ukosefu wa elimu ya
kutosha imekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya wanawake wa Tanzania na Bara la Afrika katika mapambano dhidi ya
umasikini uliokithiri mwa jamii hizo.
“Hali hii inaamanisha kuwa, mwanamke akipatiwa
elimu ya msingi ya biashara, ataweza kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia fursa
nyingi zinazomzunguuka katika kubadili hali zao kiuchumi na kujisogezea
maendeleo,”alisema Naima.
Alisema kampeni hiyo inatoa elimu ya msingi
katika maeneo makuu ya kama vile ujasiriamali na fursa zilizopo na usimamizi
binafsi wa fedha na uwekaji akiba.
“Tunaweza kuchukulia mfano wa mikopo ya bidhaa
za akinamama kama vile mikoba, viatu na vipodozi,”aliasema.
Naima, alisema AMCL kwa kushirikiana na Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto waliandaa kampeni hiyo kwa jina la
Mwanamke na Uchumi ikiwa na lengo la kuwawezesha wanawake katika kujijengea
uwezo na ujuzi wa kusimamia masuala ya fedha zao.
“Kaulimbiu ya Kampeni yetu ni Ukimuelimisha
Mwanamke Umeelimisha Jamii Nzima,”alisema Naima.
Kampeni hiyo ilizinduliwa na Waziriri wa
Maendeleo ya Jamii, Sofia Simba, Oktoba
mwaka 2014 mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment