Sunday, March 1, 2015

HAFLA YA TANZANIA BLOGGERS NETWORK YAFANA SANA,SERENA HOTEL JIJINI DAR

Sehemu ya Wamiliki wa Blogs mbali mbali hapa nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi katika hafla maalum ya mwaka kwa Tanzania Bloggers Network,ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT),Ndg. Kajubi Mukajanga pamoja na baadhi ya wadhamini waliofanikisha hafla hiyo,iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi katika hafla maalum ya mwaka kwa Tanzania Bloggers Network,Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT),Ndg. Kajubi Mukajanga (wa pili kulia) akizungumza jambo na baadhi ya Wamiliki wa Blogs Tanzania,waliokutana pamoja leo kwa lengo la kufahamina na kuunganisha vyema umoja wao.

Mkurugenzi wa Masoko kwa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu,Kelvin Twissa akizungumza machache katika hafla hiyo. 

 Mkongwe kwa maswala ya kublog hapa nchini,Ankal Issa Michuzi akifafanua jambo kwa wageni waalikwa toka Ubalozi wa Marekani juu ya kukutana kwao kwenye hafla hilo iliyofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja kwa baadhi ya Wanablog na wadhamini wa hafla hiyo.
Nadeem wa Aim Group (kulia) akiwa na maafisa kutoka ubalozi wa Marekani waliohudhuria

Suri na Kamera imo??
Ras Jhikoman akiimba wimbo wake mpya unaolaani mauaji ya Albino. Mwanamuziki mkongwe na blogger na MC wa siku hii Anko John Kitime anamshikia mike
Ras Jhikoman akilia na wauwaji wa Albino
Ankal akishusha mistari kwa wageni

Mgeni rasmi akisalimiana na Shafiq Mpanja wa Aim Group
Mike Mushi wa Jamii Forum (shati la draft) akiwa na Krantz Mwantepele (kulia) Shafiq Mpanja wa Aim Group (shoto) na mdau
Meza ya Jay Millions ya VODACOM
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa akiwa na vingunge wa Aim Group




















Mgeni Rasmi Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Mhe Kajubi Mukajanga (kati) akiwa na Ankal na Anko John Kitime
Kutoka kushoto ni Woinde Shizza, Othman Michuzi, Pam Mollel, Zainul Mzige  na Karim 
Mgeni Rasmi Mhe Kajubi Mukajanga akikata ndafu wa TBN. Kushoto kwake ni mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani na kulia ni Kelvin Twissa, Mdhamini mkuu wa Mnuso huo pamoja  na Rachel Pallangyo wa TBN
Mkuu wa ukumbi (floor manager) Monica Joseph Mara akiongoza wana TBN kuserebuka

 Ankal akiwa na ubavu wake (kulia) na ubavu wa Bongo Celebrity a.k.a Mama Amaya
 Nyota wa mchezo hapa ni Gadiola toka Arusha (mbele kati)
 Msoma risala mkuu wa TBN Henry Mdimu akiwa na bloggers wenzie 
 Wana TBN katika picha ya pamoja
 Ankal akiwa na Max wa Jamii Forums ambao wote ni waasisi wakuu wa TBN

 Nyota hapa ni blogger toka Bukoba Ruta (Blue T-shirt) akiwa na blogger wa Dar, Arusha  na Kilimanjaro
Mwanachama mkongwe wa TBN Kaka Omar Swai (wa pili kushoto) akiwa na wana libeneke toka Arusha Pam Mollel (shoto), Woinde Shizza (kulia) na Mama Ankal

No comments: