Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wa pili kushoto na viongozi wa Halmashauri wakikabidhiana daraja la mto Kitewaka kwa ajili ya kujengwa kisasa baada ya serikali kukabidhi fedha za ujenzi huo Tsh miloni 240
Mbunge Filikunjombe akilitazama daraja la mbao la mto Kitewaka ambalo litajengwa kisasa
Wannchi wa kijiji cha Maholong'wa wakimpongeza mbunge Filikunjombe kwa kutimiza ahadi yake
Waumini wa kanisa la Anglikana Maholong'wa Ludewa wakimkabidhi zawadi mbali mbali mbunge Filikunjombe baada ya kuwasaidia bati na saruji ya kutosha kujenga kanisa jipya
Viongozi wa kanisa la Anglikana na wa CCM Ludewa wakiongozana na mbunge Filikunjombe mwenye kofia
Mbunge Filikunjombe akisaidi kupalilia mahindi katika shamba la mchungaji wa kanisa la Anglicana Maholong'wa baada ya kufika kusaidia ujenzi wa kanisa hilo
Mkutano wa mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe na wanakijiji wa Maholong;wa
Mzee wa kanisa la E.A.G.T Maboga Ezekia Mhagama (kulia)akimwombea
dua mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe baada ya kutoa misaada mbali
mbali ya ujenzi na kujitolea kinanda kwa kanisa hilo vyote vikiwa
na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 11 wakati wa mkutano wa hadhara
uliofanyika kijiji cha Maholong'wa
Mkurugenzi Ludewa Bw Waziri akizungumza katika mkutano wa mbunge Filikunjombe |
Wananchi wa Maholong'wa wakimpokea mbunge wao
Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw Honoratus Mgaya akiwahutubia wananchi wa Maholong'wa
Na matukiodaimaBlog.
MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ametimiza ahadi yake ya ujenzi wa daraja la mto Kitewaka katika kijiji cha Maholong'wa kata hiyo ya Ludende baada ya serikali kumpatia kiasi cha Tsh milioni 2480 zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya ujezi wa daraja hilo .
Mbali
ya kutimiza ahadi hiyo ya daraja pia amechangia vifaa vya ujenzi
vyeye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 11 kwa ajili ya kusaidia ujenzi
wa nyumba ya mwalimu katika shule ya Msingi Maholong'wa na ujenzi
wa kanisa la Anglikana kijiji cha Maholong'wa kata ya Ludende wilayani
Ludewa mkoani Njombe .
Akizungumza na wananchi
hao leo mbunge Filikunjombe alisema kuwa kuwepo bungeni ni heshima
ya wana Ludewa na kuwa hata vurugu kubwa ambazo amekuwa
akizifanya bungeni si kwa maana nyingine zaidi ya kupigania
maendeleo ya wananchi wake.
Hata hivyo aliipongeza serikali kuwa kusaidia kutoa fedha hizo kwa wakati kwa ajili ya kuanza ujenzi hao na kuwa iwapo asingefuatilia kwa karibu serikalini ama angekuwa wa kulala bungeni yawezekana fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo zisingetolewa sasa.
“wapo wabunge wengine
ambao kazi yao ni kusinzia tu na wala haulizi swali …..ila huo pia
ndio uwakilishi wake ulipoishia …..mimi silali kule bungeni mimi
ninawatetea na kuwapiganieni kwa kulia nalia na kwenye kugombana
nagombana pia pale kwenye kunyenyekea nanyenyekea….. napenda
kuwaelezeni kuwa kazi ambayo mlinipa kuwawakilisha bungeni naitumia
vema hadi sasa sijakwama kuwatumikia ….nilisema mwanzoni mimi
navurugu bungeni ila ni vurugu za kimaendeleo”
Filikunjombe
alisema kuwa waakati akiomba kuwa mbunge wa Ludewa alitaka
kuwawakilisha bungeni na kushirikiana nao katika shughuli za
kimaendeleo hivyo angekuwa mbunge wa ajabu kama angekuwa mbali na
shughuli za kimaendeleo katika jimbo lake .
Alisema
wakati akigombea ubunge mwaka 2010 aliwaahidi wananchi wa kata la
Ludende kuwajengea daraja la kisasa zaidi katika kijiji cha
Maholong'wa ili kuchochea kasi ya maendeleo katika kata ya Ludende na
kata za jirani ,ahadi ambayo sasa anaitimiza kwa kumpata mkandarasi
atakayejenga daraja hilo kwa Tsh milioni 248 na ujenzi wake utaanza
mara moja baada ya mvua kutulia .
“
"Mimi nataka ujenzi huu uanze mara moja kwani
kama shida wananchi wangu mmetesema sana hivyo sasa nataka iwe
basi matesa na sitapenda kuona Halmashauri inaziweka pesa hizo
pasipo kutumika kwa kazi iliyokusudiwa fedha za ujenzi huu zimetoka
serikalini baada ya kuwabana zaidi"
Alivitja vifaa hivyo kuwa ni bati 200 na saruji 200 pia kinanda kwa kanisa la E.A.G.T na vifaa mbali mbali vya michezo pamoja na kuwakodia usafiri kutoka Dar es Salaam hadi kijijini hapo kwa ajili ya kusafirisha vifaa hivyo.
Awali viongozi wa madhehebu ya dini na vyama vya siasa katika kata ya Ludende wilaya ya Ludewa wamepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na kuwa hawahitaji kubadili tena wabunge kama nguo .
Huku mwenyewe akidai kuwa yeye si mbunge wa kusinzia bungeni ni makini katika kuwawakilishi wananchi wake na kuwa ana vurugu sana bungeni ila vurugu zake ni za kimaendeleo si vinginevyo.
Wakishukuru mara baada ya kuwakabidhi mkandarasi wa kuanza ujenzi wa daraja , pamoja na saruji na bati kwa ajili ya kuchangia miradi mbali mbali ya kimaendeleo katika kata hiyo na ujenzi wa kanisa jipya ya Anglicana kijiji cha Maholong’wa.
Viongozi hao akiwemo mzee wa kanisa la E.A.G.T Mboga Bw Ezekia Mhagama na mkuu wa shule ya msingi Maholong’wa Bw Damas Malihayi walisema kuwa maendeleo makubwa yanayoendelea kuonekana katika wilaya ya Ludewa ni jitihada kubwa ambazo zinafanywa na mbunge huyo na hivyo wao kama viongozi wa dini kazi kubwa ni kuzidi kumwombea afya njema ili aendelee kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi vingine zaidi.
Alisema mzee huyo wa kanisa la E.A.G.T kuwa matumaini ya wananchi wa Ludewa yamekuwa makubwa zaidi dhidi ya mbunge wao kutokana na sura ya Ludewa kwa sasa baada ya mateso ya miaka zaidi ya 50 ya Uhuru bila kuwepo kwa maendeleo yanayoonekana ila toka alipoingia mbunge Filikunjombe mwaka 2010 wananchi wa Ludewa ndipo walipata uhuru wao na kuwa wao wanajiona kama miaka hii mitano toka walipomchagua mbunge huyo kuwa mbunge wao ndipo wao walipopata uhuru wao.
“Tunatambua nchi yetu ilipata uhuru mwaka 1961 kwa maeneo mbali mbali ya nchi wananchi wake kusogezewa huduma mbali mbali zikiwemo barabara za lami ila sisi Ludewa lami tumeanza kuiona mwaka jana na kama huku Maholong’wa daraja ambalo ni tegemeo kubwa kwetu lilikuwa la mbao hadi sasa ambapo mbunge wetu ametusaidia kutafuta pesa ya kujenga daraja la kisasa na huu ndio uhuru wetu “
Mhagama alipongeza pia kwa msaada wa saruji na bati za kutosha kukamilkisha ujenzi wa kanisa la Anglicana na msaada wa kinanda kwa kanisa lake la E.A.G.T kuwa ni mbunge pekee kusaidia jamii nzima ya Ludewa pasipo kutazama masuala ya itikadi zao .
Hivyo allisema kwa wananchi wa Ludewa hawana sababu ya kuendelea kubadili badili wabunge kwa sasa kwani utendaji kazi wa mbunge Filikunjombe umewakuna wengi na hivyo kazi kubwa kwao ni kuendelea kumuunga mkono kwa kumpitisha tena na tena kuwa mbunge wao .
Mkuu wa shule ya Msingi Maholong’wa Bw Malihayi alisema kuwa kuna haja ya wana Ludewa kushikamana na kuona hawampotezi mbunge huyo na badala yake kuzidi kumpa ushirikiano zaidi.
Kwa upande wake Paschal Kayombo akizungumza kwa niaba ya vijana wa kata hiyo alisema kuwa kero kubwa ya vijana ilikuwa ni daraja hilo la mto Maholong’wa ambalo kwa sasa limekwisha patiwa ufumbuzi na kuwa vijana kwa sasa wanaimani kubwa na utendaji kazi wa mbunge huyo.
Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya akiwahutubia wananchi hao alisema kuwa CCM ni chama kizuri sana ila wanaofanya wananchi kukichukia chama ni baadhi ya viongozi wakiwemo wabunge ambao wameshindwa kuwatumikia vema wananchi wao.
Kwani alisema iwapo kila mbunge atafanya kazi kwa kujituma kama ilivyo kwa mbunge Filikunjombe uwezekano wa kata ama majimbo kuchukuliwa na vyama vya upinzani usingekuwepo ila wanaopigia kura wapinzani ni wana CCM ambao wamechoshwa na uwajibikaji mbovu wa wale waliowachagua.
No comments:
Post a Comment