Wednesday, March 11, 2015

BAN KI MOON ATAMBUA MCHANGO WA RAIS JAKAYA KIKWETE

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza siku ya Jumanne, wakati wa uzinduzi wa ripoti mpya kuhusu mkakati wa kimataifa wa kila mwanamke, kila mtoto ambao Ban Ki Moon aliuanzisha mwaka 2010. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa vuguvugu hilo ambalo kwa ushirikiano baina ya wadau mbalimbali zikiwamo serikali, mashirika ya kimataifa, asasi zisizo za kiserikali, wasomi, wanaharakati na sekta binafsi zimewezesha kuokoa maisha ya wanawake na watoto 2.4 milioni.
katika picha hii ya maktaba wanaonekana Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu Ban Ki Moon, wakifurahia jambo walipokuta katika moja ya mikutano ya kimataifa. Akielezea nini kilichosababaisha vuguvugu hilo la kila mwanamke, kila mtoto kuwa na mafanikio makubwa.Ban Ki Moon alisema utashi wa kisiasa na utayari ulioonyeshwa na viongozi mbalimbali akiwamo Rais Jakaya Kikwete ndio baadhi ya sababu zilizochangia kufanikiwa kwa mkakati huo. Rais Kikwete akiwa mwenyekiti mwenza na Waziri Mkuu wa Canada walisimamia Kamisheni ya Habari na Uwajibikaji baada ya kuombwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, jukumu ambalo wamelitekeleza kwa ukamilifu na kutoa mchango mkubwa katika uboreshaji wa afya ya mama na mtoto kupitia vuguvugu hilo la kila mwanamke, kila mtoto.

Na Mwandishi Maalum.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban ki Moon,  amesema kama si utashi wa kisiasa,  kujituma, na kujitolea kulikofanywa na  viongozi mbalimbali aliowaomba kufanya naye kazi kwa karibu huku wengine wakijitolea wenyewe,  uhai wa  wanawake na watoto  2.4 milioni  usingeokolewa.

Ban Ki Moon ameyasema hayo siku ya  Jummane wakati wa uzinduzi wa  ripoti mpya  kuhusu mkakati wa kimataifa kuhusu vuguvugu la  kila  mwananamke, kile mtoto, ( every woman, every child) mkakati ambao Ban Ki Moon  aliuratibu mwaka 2010 .

“ Siri kubwa ya mafanikio ya  mkakati huu ni  uwajibikaji.  Nilipoanzisha mkakati huu niliwaomba baadhi ya viongozi wanisaidie, wapo waliosaidia katika uhamasishaji wa  raslimali fedha,  wapo kama Rais Jakaya  Kikwete wa Tanzania na waziri Mkuu wa Canada ambao walisimamia suala zima la  habari  na uwajibikaji,  mchango wao, kujituma kwao na uthubutu wao ndiyo umetufikisha hapa , tumeweza kuokoa maisha ya wanawake  na watoto wengi na kazi bado inaendelea” ameeleza  Katibu Mkuu.

Akasema   mkakati huo aliouzisha   wa  kila mwanamke, kila mtoto  na ambao chimbuko lake ni lengo namba  nne na tano la maendeleo  ya millennia  ni  mkakati ambao si tu   umekuwa wa mafanikio makubwa lakini umegusa  hisia za wadau mbalimbali za watu wengi .

Malengo namba nne na  tano ya maendeleo ya millennia na ambayo yanafikia ukingoni  mwisho mwa  mwaka huu  yanajikita katika kupunguza idaidi ya vifo vya wanawake na idadi ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

“Nilianzisha mkakati huu kwa sababu mimi mwenyewe nimeguswa katika maisha yangu utoto wangu kwa kuondokewa( kufariki) kwa kaka na dada zangu kwa matatizo ambayo yangeweza kuzuilika.  Simulizi  alizokuwa akisimuliwa na mama yake   juu  hofu kuu wanayokuwa nayo wanawake wanapokwenda kujifungua vile vile ni moja ya hamasa iliyonifanya nianzishe mkakati huu.  Lakini pia katika utekelezaji wa majukumu yangu nimekutana na visa vingi vilivyoongea  nia  na ari   kuwa na mkakati huu” ameeleza Ban Ki Moon.

Ripoti hiyo ambayo uzinduzi wake umekwenda sambamba na mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu hadhi ya wanawake,  inabainisha kwa kina mafanikio na changamoto mbalimbali za utekelezaji wa  katika eneo hilo linalohusu afya ya mama na mtoto.

Ban Ki Moon amesema amefarijika na kutiwa moyo sana

Kwa mfano Makati huo ambao umegusa hisia wa wadu  mbalimali wakiwamo  viongozi wakuu wan chi na serikali,  asasi zisizo za kiraia, wanaharakati  na  makampuni binafsi.
taarif yasingeushirikiano wa karibu baina yake na Viongozi wakuu wa mataifa mbalimbali umesaidia kuokoa maisha ya  …………….., ambao wangepoteza maisha yao wakati wa kujifungua.

No comments: