Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto
akimkaribisha Balozi wa Uingereza nchini Bi Dianna Melrose ofisini kwake
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kulia
akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Dianna Melrose ofisini
kwake jijini Dar es Salaam kujadiliana mambo mbalimbali yahusuyo
Miundombinu ya Barabara za juu flyovers, madaraja ya chuma mabey
bridges na suala zima la kupunguza msongamano katika jiji la Dar es
Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kulia
akisalimiana na Richard Boulter kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimatifa ya
Uingereza (Department for International Development) aliyeambatana na
Balozi wa Uingereza nchini Bi. Dianna Melrose.
Majadiliano yakiendelea kati ya Ujumbe wa Balozi wa
Uingereza nchini Bi Dianna Melrose pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Pombe Magufuli.
Ujumbe kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini, wakwanza
kulia ni Balozi wa Uingereza Dianna Melrose, anayefuatia ni Meneja wa
Masula ya Biashara na Maendeleo Marie Strain pamoja na Richard Boulter
kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimatifa ya Uingereza.Picha zote kwa
Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU)-Wizara ya Ujenzi
No comments:
Post a Comment