Thursday, March 12, 2015

Airtel yatoa msaada kwa wahanga wa mafuriko Kahama

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetembelea wahanga wa mfuriko ya mvua katika wilaya ya kahama mkoani shinyanga kwa kuwapatia msaada wa mahitaji muhimu yanayoitajika kwa sasa. Zaidi ya watu 35 walifariki na kuwaacha mamia wakiwa hawana makazi ya kukaa kufatia mvua kubwa iliyonyesha mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu

Akionge wakati wa makabithiano ya msaada huu, Meneja mauzo wa Airtel Shinyanga Bwana Ezekiel Nungwi alisema” Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia zilizopoteza marafiki na wanafamilia kutokana na mafuriko haya.

Tunatambua pia mafuriko haya yamewaacha wakazi wengi bila makazi, huku mazao yao kuharibiwa na mifugo yao kufa hivyo tunaungana kwa pamoja kutoa msaada kwa namna tutakayoweza . Leo kwa niaba ya Ofisi yetu ya kanda ya Shinyanga tunatoa msaada wa mabati, mablanketi, magodoro pamoja na chakula vyenye thamani ya shilingi milioni 3 na kuwaomba watanzania kuungana nasi kuwasaidia ndugu zetu wa kahama ili kuepuka milipuko ya magonjwa isitokee na kuwawezesha kurudi kufanya shughuli zao za kawaida mapema iwezekanavyo.

Sambamba na mchango huu, tunapenda kuzindua namba maalumu itakayowawezesha watanzania kuchangia. Tunachukua fulsa hii kuwaomba wateja wetu kuchangia kwa kutuma ujumbe wenye neno MAAFA kwenda namba 15626 , ujumbe huu utalipiwa shiling 256 na pesa hiyo itaingia kwenye mfuko wa kuchangia wahanga wa mafuriko mkoani Shinyanga,

Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Kahama helen Benjamin Alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu ulikuja wakati tunauhitaji zaidi, Tunawashukuru kwa kuanzisha namba itakayowapa fulsa watanzania kuchangia, napenda kuwaomba watanzania kushiriki kwa kuchagia na kwa makampuni mengine kujitolea na kutusaidia katika hali ngumu ambayo imetuweka kwenye hatari kupata milipuko ya magojwa na zaidi tumekosa makazi na shughuli zetu za kiuchumi zimeteketea. Tunawashukuru waliojitolea mpaka sasa na tunaomba muendelea na moyo huo wa kujitolea.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Mh. Benson Mpesya akisalimiana na Muwakilishi wa kampuni ya Airtel mkoa wa Shinyanga,Ezekiel Nungwi wakati Kampuni hiyo ilipofika kuwaona wahanga wa mafuriko na kuwapelekea Baadhi ya Vitu mbali mbali.kampuni hiyo ya Airtel imetoa,sabuni ,mabati ,maharange ,mchele ,mafuta kwa Wahanga hao.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Mh. Benson Mpesya akiwapongeza wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Aitel kwa moyo wao wa kuwasaidia waathilika wa mafuriko katika kijiji cha mwakata ambapo Wilayani Kahama yaliyotokea hivi karibuni.Airtel imetoa msaada wa vitu mbali mbali kama vile sabuni ,mabati ,maharange ,mchele ,mafuta.
Sehemu za Nyumba zilizoathiliwa na Mafuriko hayo.
Mmoja wa waathirika wa Mafuriko huko Kahama,Bi. Helen Benjamin akiongea juu ya hali halisi ya maafa hayo na kuomba serikali kuwapatia msaada.


No comments: