Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya mara baada ya kukagua barabara za
mkoa wa Rukwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Col.Ngemela Eslom
Lubinga akisoma taarifa ya mafanikio ya Serikali ya wilaya hiyo kwa Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Magufuli.
Sehemu ya barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75-
ambayo ujenzi wake umekamilika kwa zaidi ya asilimia 60.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiimba
pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Wilayani Nkasi mara baada ya kuwasalimia
alipokuwa njiani kukagua mradi wa barabara unaopita karibu na shule hiyo.
Sehemu
ya barabara ya Sumbawanga-Matai-Kasanga km 112 ambayo ujenzi wake unaendelea
kujengwa kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia
wakazi wa Kibaoni kuhusu kuwasimamia makandarasi wanaojenga barabara za
Kanazi-Kizi-Kibaoni kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na
wakazi wa Kibaoni Wilayani Mlele katika mkoa wa Katavi.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwa na
Mama mzazi wa Waziri Mkuu Mheshimiwa
Mizengo Pinda nyumbani kwake Kibaoni mkoani Katavi. Waziri wa Ujenzi alipita
kumsalimia mara baada ya kuwahutubia wakazi wa Kibaoni kuhusu masuala
mbalimbali ya barabara na nyumba za Serikali.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akihutubia
mamia ya wakazi wa Katavi kuhusu miradi mikubwa ya barabara katika mkoa huo.
Waziri wa Ujenzi akiagana na wananchi wa Katavi
mara baada ya kuwahutubia.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara
ya Ujenzi.
No comments:
Post a Comment