Wednesday, February 4, 2015

VIONGOZI WA BENKI YA NBC WAPANGA MIKAKATI YA MAENDELEO MWAKA 2015 NA KUZAWADIA WAFANYAKAZI WAKE BORA

 Mkurugenzi wa Muda wa Benki  ya NBC , Bw. Pius Tibazarwa akizungumza na wafanyakazi wa NBC katika warsha ya siku moja kuzungumzia maendeleo na mikakati ya benki hiyo kwa mwaka 2015. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi, ilijumuisha wakurugenzi wote wa benki hiyo, wakuu wa vitengo na mameneja wa matawi ya NBC nchi nzima.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Hazina cha Benki ya NBC, Barton Hamisi,  akisisitiza jambo wakati wa warsha ya siku moja kuzungumzia maendeleo na mikakati ya benki hiyo kwa mwaka 2015. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi ilijumuisha wakurugenzi wote wa benki hiyo, wakuu wa vitengo na mameneja wa matawi ya NBC nchi nzima.
 Mkurugenzi wa Mauzo ya Reja Reja wa NBC ,Musa Jallow akimkabidhi cheti cha mtoa huduma bora wa mwaka 2014 Columba Kambi wa NBC Tawi la Dodoma katika hafla ya kupongeza wafanyakazi bora katika kitengo cha mauzo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. 
 Wakuu wa vitengo mbalimbali vya Mauzo ya Reja Reja vya NBC Limited, wakimkabidhi tuzo Kemibaro Omuteku  (wa tatu kushoto) katika hafla ya kupongeza wafanyakazi bora katika kitengo cha mauzo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
 Mkurugenzi wa Mauzo Wa NBC Musa Jallow, akimfunika shuka  ya Kimasai Meneja wa Tawi la Kahama Martin Nkanda baada ya kuibuka kuwa Meneja wa Tawi bora wa mwaka 2014 katika hafla ya kupongeza wafanyakazi bora katika kitengo cha mauzo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
 Meneja wa tawi la NBC la Muhimbili Fatma Gulamsood (kulia) akipokea tuzo ya jumla katika ukusanyaji madeni kw amwaka 2014. Akimkabidhi tuzo hiyo ni Andrew Massawe Mkuu wa Kitengo cha  Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa katika hafla ya kupongeza wafanyakazi bora katika kitengo cha mauzo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano Mahusiano wa NBC Rukia Mtingwa akiongea na wafanyakazi wenzake (hawapo pichani) katika warsha ya siku moja kuzungumzia maendeleo na mikakati ya benki hiyo kwa mwaka 2015. Warsha hiyo ilijumuisha wakurugenzi wote wa benki hiyo, wakuu wa vitengo na mameneja wa matawi ya NBC nchi nzima, akimsikiliza kwa makini ni Eddi Mhina Meneja wa Mauzo kitengo cha Imani Banking cha NBC.
Sehemu ya wafanyakazi wa NBC wakipasha misuli kujiweka imara tayari kwa mikakati ya 2015 katika kuendeleza benki yao wakati wa warsha ya siku moja iliyojumuisha wakurugenzi wote wa benki hiyo, wakuu wa vitengo na mameneja wa matawi ya NBC nchi nzima.

No comments: