Baadhi
ya vijana wanaofanya utapeli kwa kutumia vipande vya sabuni wakikimbia
baada ya kunaswa na kamera ya bloger wetu wakiwa katika jitihada za
kumwibia mmoja wapita njia katika mtaa wa Uhuru Dar es Salaam leo
asubuhi.
Kwa
Mujibu wa shuhuda vijana hao huwa kundi na baadhi huangalia mwenzao
akitekeleza uhalifu wakati wao wakihakikisha wanampa ishara ya
kufuatiliwa na kutoa ishara waonapo mazingira ya mchakato kushindikana
ama hali kuwa tete kwa mwenzao iwapo mnunuzi wa simu atakuwa ameshtukia
njama zao mbovu za kutaka kutenda uhalifu.
Mmoja
wa wakazi wa Dar es Salaam alikumbwa na mkasa wa kuibiwa shilingi laki
moja alivutiwa na mhalifu mmoja kwa kumwonesha simu yenye gharama ya sh
200,000 huku akimsihi anunue kwa sh 100,000.
Alipokubali
kununua simu hiyo, walimbadilishia wakati akitoa hela na alipoikabidhi
na kwenda hatua chache aligundua kuwa amepewa kipande cha sabuni kwenye
bahasha wakati mhalifu huyo na wenzake wameshatokea kusikojulikana.
Jambo
la kusikitisha ni kwamba askari polisi wameshapokea malamiko ya mikasa
kama hiyo lakini hakuna jitihada za makusudi zilizochukuliwa kuwanasa na
kuwatia hatiani wahalifu hao.Tahadhari inatolewa kwa wananchi kutonunua
bidha kama hizo mkononi kwa watu hasa katika mazingira ya ushawishi
mkubwa na kufanya manunuzi kwenye maduka yenye kutoa risiti kwa bidhaa
walizonunua. |
No comments:
Post a Comment