Sunday, February 22, 2015

SERIKALI YAAHIDI KUIPIGA JEKI NACTE

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto)akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela wakati alipokuwa akimfafanulia jambo alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani lililopo makao makuu ya ofisi hiyo Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela ( aliyesimama) akifafanua jambo mgeni rasmi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) wakati hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani lililopo makao makuu ya ofisi hiyo Mikocheni jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Consolata Mgimba.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati)akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa (NACTE) Dkt. Primus Nkwela,Kamishina wa Elimu Profesa Uestella Bhalalusesa,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara wa wizara hiyo Consolata Mgimba na Mwenyekiti wa barabaza la Taifa la Elimu ya Ufundi Mhandisi Steven Mlote.Hafla hiyo ya Uzinduzi ilifanyika katika makao makuu ya ofisi hizo Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Consolata Mgimba wakizinduzi jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) uzinduzi huo ulifanyika makao makuu ya NACTE Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Katibu Mkuu waWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Sifuni Mchome akinongonezwa jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani uliofanyika makao makuu ya ofisi hizo Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mhandisi Steven Mlote wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus Nkwela wakati alipokuwa akisoma lisala wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela, akisikilizwa jambo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) na wadau wengine wa elimu wakati alipokuwa akielezea jinsi walivyofanikiwa kujenga jengo hilo jengo hilo wakati wa uzinduzi wa jengo hilo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati) akimshukuru Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mhandisi Steven Mlote baada ya kumkabidhi zawadi katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus Nkwela.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa akionesha cheti halali cha matumizi ya jengo jipya alilolizindua la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) lililopo makao makuu ya Baraza hilo Mikocheni B jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus Nkwela na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mhandisi Steven Mlote.
Katibu Mkuu waWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Sifuni Mchome( kulia) akisikilizwa kwa makini na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa (kushoto ) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela (katikati)alipokuwa akifafanulia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani lililopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Serikali imesema itaendelea kusaidia upatikanaji wa rasilimali watu na fedha ili kuliwezesha Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kutekeleza malengo yake ya kukuza stadi na maarifa kwa idadi kubwa ya vijana wanaohitimu shule za msingi na za sekondari.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la mitihani la baraza hilo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa alisema sekta ya elimu hususani Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi inakuwa kwa kasi kubwa haswa ikizingatiwa kuwa wahitimu wa ngazi za elimu ya msingi na sekondari inaongezeka kila mwaka.

Waziri Kawambwa alieleza kuwa, wahitimu wengi hawapati fursa za kuendelea na masomo hadi ngazi ya vyuo vikuu. “Wahitimu hawa wanahitaji fursa mbali mbali za kukuza stadi na maarifa ambazo zitawasaidia kukabiliana na changamoto za maisha yao ya kila siku na kuingi katika soko la ushindani la ajira ndani nan je ya nchi,”  alielezaa

Kuhusu ongezeko la vyuo vinavyoendesha mafunzo ya Ufundi alisema inaonyesha kuwa hadi sasa kuna idadi ya vyuo takribani 501 na kozi zipatazo 1050 kuanzia ngazi ya Cheti hadi Shahada ya kwanza zinazoendeshwa katika vyuo kwa udhibiti wa  Baraza.

“Huu ni ushahidi tosha kuwa mahitaji ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa vijana wetu ni makubwa ukilinganisaha na uwezo wetu wa kutoa mafunzo hayo. Hivyo, ipo haja kwa baraza kuimarisha Ofisi za kanda ili ziweze kutoa huduma za karibu, kwa wakati na kwa grarama nafuu,” alieleza

Kwa upande wake mwenyekiti wa Braza hilo Injinia Steven Mlote alisema ili kuhakikisha vyuo vinazingatia masharti ya usajili wao na vinatoa elimu bora, Baraza limeweka nguvu kubwa katika kufuatilia na kusimamia ubora wa elimu unatolewa na vyuo vilivyosajiliwa na baraza

“Baraza limefungua ofisi katika kanda 6 kwa ajili ya kusogeza huduma mikoani na kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji. Aidha, kukamilika kwa jengo hili ni utekelezaji wa mkakati  wa kuimarisha huduma za kudhibiti ubora kwa vyuo na uendeshaji mitihani ulioanza kwa kununua mitambo ya kuchapisha mitihani,”


Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo alisema kuwa kutumia Sheria na Kanuni zake, Baraza limetoa notisi ya siku 30 kwa vyuo na taasisi 13 kufungiwa na kufutiwa usajili endapo havitakidhi vigezo vya baraza na pia aliatangaza kutolewa kwa notisi ya kuvishusha hadhi vyuo na taasisi 61.

No comments: