Tuesday, February 24, 2015

NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA AFUNGUA SEMINA YA VIJANA MKOANI LINDI

Mgeni rasmi kwenye mafunzo ya stadi za kazi na utambuzi wa fursa za kiuchumi zilizopo mkoa wa Lindi Naibu waziri wa kazi na ajira mhe.Dr. Makongo Mahanga (MB) amewataka vijana wa mkoa wa Lindi kuyageuza mafunzo watakayoyapata ya stadi za maisha sanjari na kuzitambua fursa zilizopo ndani ya mkoa, waweze kujiajiri na kujikomboa kiuchumi,wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo ambapo jumla ya vijana 360 kutoka halmashauri sita zilizopo mkoani Lindi wameudhuria kwenye ukumbi wa kanisa katoliki Mt.Kagwa. Vijana 360 kutoka kwenye wilaya za Kilwa,Ruangwa,Liwale,Nachingwea,Lindi Mjini na Vijijini ambao ni washiriki wa mafunzo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi naibu waziri wa kazi na ajira Mhe.Dr.Mkaongoro Mahanga hayupo pichani.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza akiwaeleza washiriki wa mafunzo ya stadi za maisha sambamba na kufahamu fursa za kiuchumu ambapo mpango wa kuendesha mafunzo hayo umebuniwa na yeye mwenyewe,mbele ya mgeni rasmi,wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
baadhi ya wakuu wa taasisi mbalimbali wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza alipokuwa akijadiliana nao kuhusu umuhimu wa kuwapa elimu ya ufahamu wa mambo yanayotekelezwa na taasisi hizo mkoani lindi,kulia ni meneja wa shirika la nyumba bwn.M.Peter,anayefuata meneja wa CRDB(PLC) na mwenye miwani katikati ni Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Fortunata Kullaya.
Katibu tawala wa mkoa wa LindiNdg.Abdlla Chikot akijadiliana jambo na wakuu wa wilaya ya Kilwa kushoto mhe.Abdallah H. Ulega,kulia ni Mkuu wa wilaya ya Liwale mhe. Ephrem Mmbaga,nje ya ukumbi wa mafunzo wa Mt. Kagwa Lindi.
Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akitoa taarifa ya madhumuni ya ofisi ya mfuko kushiriki kwenye mafunzo hayo kwa waandishi wa habari,ambapo elimu ya faida na umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii.(CHF) itatolewa hapo kesho kwa washiriki vijana.
NA .Mwandishi wetu-LINDI

NAIBU Waziri wa kazi na Ajira, Makongoro Mahanga, amesena kuwa hali ya ukosefu wa ajira nchini mpaka hivi sasa kwa mujibu wa utafiti wa nguvu kazi uliofanyika mwaka 2006, jumla ya watu waliokuwa hawana kazi hapa nchini ni asilimia 11.7.

Hayo yamebainisha leo na Naibu huyo, kwenye ufunguzi wa semina ya vijana mkoa wa Lindi, na kusema kuwa utafiti huo ulionyesha kuwa takribani asilimia 13.4 ya vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 34 wa Tanzania hawana kazi kabisa.

Alisema ukosefu huo wa ajira kwa vijana ni kubwa zaidi asilimia 26.7 ukilinganisha na vijijini asilimia 7.9 ,imechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa kutofikiwa kikamilifu kwa malengo ya nchi ya kuinua uchumi katika sekta za kilimo, uzalishaji na viwanda.

“Wimbi la vijana ambalo ni nguvu kazi ukimbilia mijini na hivyo kupunguza uzalishaji wenye tija kwenye sekta ya kilimo,hivyo kuchangia ongezeko la ukosefu wa ajira mijini sambamba na ongezeko la wafanya biashara wa sekta isiyo rasmi maarufu kwa jina la machinga.

Kuendelea kupanuka kwa sekta isiyo rasmi kutoka asilimia 8.8 mwaka 1990/01 hadi asilimia 11.3 mwaka 2005 na kupungua kwa nguvu kazi katika sekta ya kilimo kutoka asilimia 83.7 hadi asilimia 74.6 ni dalili kuwa kuna uhamaji mkubwa wa nguvu kazi kutoka vijijini kwenda mijini.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza, alisema kuwa lengo la semina hiyo ni kuwawezesha vijana hao kupata ufahamu na uelewa wa nafasi yao katika jamii, wajibu wa kijana, haki zake na kuwajengea uwezo ambapo watapata stadi za namna ya kutambua fursa zilizowazunguka, na umuhimu wa  kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii hususani mfuko wa afya ya Jamii (CHF) kwani ndiyo mkombozi wa huduma za matibabu.

Mahiza alisema, katika semina hiyo ya siku tano, vijana watapata fursa ya kupitishwa katika mambo mbalimbali, ambapo taasisi mbalimbali zitapata fursa ya kutoa elimu kwa vijana kuhusu,usalama wa raia na mali zao, Katiba inayopendekezwa na kushiriki wa vijana katika kukuza uchumi.

No comments: